Dada WoS,
Kama kawaida heshima mbele. Natumai umzima na unaendelea vyema na shughuli zako. Mimi nitakujibu kama ifuatavyo.
Kwa Tanzania ndiyo. Kuna msemo wa Kiingereza usemao "With great power comes great responsibility." Nchi kama Tanzania hatuna checks and balances. Raisi anauwezo wa kuteua watu wake toka juu (waziri mkuu, mawaziri nk) mpaka chini (Wakuu wa wilaya nk). Pia Bunge linaongozwa na chama chake ambacho kila siku tunaona sera za serikali zikipitishwa kwa "Ndiyooo, nakubaliana kwa asilimia 100". Sasa dada WoS kwenye nchi ambayo raisi ana nguvu zote hizo tumuulize nani? Kila ambae anapaswa kuulizwa kateuliwa na raisi tena bila vetting yoyote ya Bunge. Sasa kama una nguvu ya kuteua watu wako from top to bottom iweje usiwe na majibu?
Waziri wake mwenyewe wa Nishati na Madini alisema tatizo la umeme litakua historia ifikapo June mwaka huu. Akabadilisha tena tena na kusema ni mpaka 2015. Sasa wakati serikali yake ilivyo kuwa inatuambia tatizo la umeme litakua historia ilikua inajua raisi wake si wingu? Ahadi wanazitoa wenyewe. Kumbuka dada ahadi ni deni.
Sijawahi ona upinzani wowote duniani unaosifia sifia serikali wala chama kilichopo madarakani. Nia na madhumuni ya kuwa mpinzani ni kuonyesha kwamba wewe unaweza fanya kazi nzuri zaidi ukipewa nafasi. Sasa ukisifia sifia ina maana una kubali kazi inayofanywa na chama tawala kwa hiyo wananchi hawana haja ya kukukabidhi wewe madaraka. Pia kazi ya upinzani ni kuipa serikali changamoto na changamoto hizi ni kutoa njia mbadala kwa kusema hata kama umefanya hivi ungefanya hivi ingekua vizuri zaidi. Lakini pia CCM isiwe wanafiki. Ni wao lini wamekubali mazuri ya upinzani? Ni mara ngapi wabunge wa upinzani wanatoa hoja nzuri lakini hupingwa kisa tu imetolewa na upinzani? Wao kusifia hawataki lakini kusifiwa wanapenda???
Kila chama ni kwa manufaa ya wanachama sijui kwa nini hii tunaona haiapply kwa vyama vya siasa? Kwa mfano chama cha wafanyakazi kipo kwa ajili ya kina nani? Chama cha walemavu? Chama cha walimu? Ukichunguza vyama vyote vipo kwa manufaa ya wanachama wake. Huo ndiyo ukweli.