Hata mimi nakubaliana nawe kuwa suala la umeme ni nyeti na siyo tatizo la kawaida.Linalenga kwenye usalama wa nchi kwa maana halisi. Kukosekana umeme kunahatarisha maisha ya watanzania.
Je rais wetu hawezi kuchukua hatua za dharura ikibidi hata kupunguza vifungu vya bajeti za wizara na kuelekeza nyenzo zote kuhakikisha tunapata umeme tunusuru uchumi na mengi yaliyomo hatarini?
Rais kasema tumpe mapendekezo ya jinsi gani kutatua tatizo. Nadhani moja ya pendekezo ni hili!
WoS, Rais anapewa mamlaka na katiba kutangaza hali ya dharura, na vitu kama
presidential decree. Nguvu hizo zinamwezesha yeye kuchukua hatua za dharura kwa manufaa ya nchi, ikiwa ni pamoja na kuelekeza
resource bila ruhusa ya mamlaka nyingine ikibidi. Kwahiyo tatizo sio pesa au nyenzo nyingine ila kitu kinaitwa
political will.
Suala la umeme limekuwa la kisiasa zaidi kuliko utaalamu ndio maana kuna mwingiliano wa kamati za bunge, wizara n.k. Hakuna anayejua nani mwenye kauli zaidi ya mwingine. Kibaya zaidi wataalamu wamewekwa pembeni ili siasa ikidhi matakwa ya wahitaji.
Richmond ilingia kwa nguvu za siasa na sio wataalam. Na kibaya zaidi wanasiasa wanaofanya hivyo 'wanamamlaka' yasiyo rasimi ndani ya serikali lakini yenye nguvu sana.Hawa ndio wanoifunga serikali na Rais mikono ya kuchukua hatua za dharura, wakilinda masilahi yao. Sidhani Dowans a.k.a Symbion au IPTL wangependa mgao upungue!!
Rais anapoomba mawazo ni dalili nyingine ya kushindwa kazi. Hivi mwanakijiji anayewania mhogo wa siku au yule mama aliyebeba ndoo ya maji km 5, au mfanyakazi anayekata mbuga kutoka ubungo kwenda posta kwa mguu,kweli anaweza kuwa na wazo la kumpa mheshimiwa. Hawa wana mizigo mizito inayowasubiri.
Mbowe ametoa ushauri iundwe kamati ya wataalamu wanaoweza kuja na
solution. Kumbuka pia tuna wasomi waliobobea katika uchumi, nishati, biashara n.k kutoka katika rasilimali watu na
academicians. Rais hajawatumia hawa.
Kamati za bunge, shirikisho la wenye viwanda, wawekezaji kila mara wamekuwa na ushauri. Jambo la kusikitisha ni kuwa ushauri na maoni yao yanapofika mezani kwa mheshimiwa hukutana na nguvu kubwa ya kisiasa na huwekwa pembeni.
Rais anatakiwa atoke mbele, atangaze hali ya dharura, akutane na wadau wa sekta ya nishati, wanataaluma,wanasiasa makini na wafanyabiashara wenye nia njema walizungumze tatizo na kupata ufumbuzi wa muda mfupi na muda mrefu.
Atafanikiwa tu endapo atakubali kuweka siasa pembeni, kuacha wapambe na kuwa tayari kuchukua maamuzi magumu.
Kazi ya Rais ni ku
mobilise resources ili zitoe majibu ya matatizo, inapofika mahali yeye hawezi kutumia
resources zote kama
human resource,
natural resource,
political and executive power anasubiri kusikia kutoka mitaani inasikitisha!!
Majibu ya tatizo yapo, shida inakuwa nani wa ku
mobilize resource za kiutaalamu, kiutendaji ili zitoe majibu? Kama kumfukuza Jairo ilisubiri Rais akiwa nje, na kwa mwendo wa safari za nje nani anaweza kusimamia zoezi la umeme lenye nguvu za kisiasa na kiushawishi kama si yeye.