Are you sure?FYI iam confident but not over confident.Arrogance?I dont really care!Uncalled-for hubris!
Are sure?FYI iam confident but not over confident.Arrogance?I dont really care!
Back to the point,changia mada na ujibu accordingly,vijembe vipo,unaumizwa sana,i wonder why.Dont bring emotions once again.Hilli si jukwaa lake.
Unaumizwa watu flani flani wakipigwa vijembe kidogo tu.Ndo jukwaa la siasa hakuna mapenzi humu.Rudi kwenye hoja na unieleze ni kwanini JK hatakiwi kuulizwa issue ya umeme.We Meku na wewe bana...sasa naumizwa sana na nini au na nani?
WOS,
First off i do respect you.
Howevernadhani una ujuzi zaidi kwenye yale majukwaa mengine.(You know what i am talking about)
Thread yako hii inaonyesha kutokuelewa masuala ya kiutawala na siasa.Soma katiba kidogo utagunduwa ni kwanini the bucks stops with Mkulu/Rais.
Hata hivyo nimesikitika kwa uliyosema na kupitisha hukumu kuwa sielewi siasa au hata Katiba - lol nimecheka hadi machozi yakanitoka!The bolded part ndio imeniacha hoi!Labda ungekuwa more specific Mkuu.
Mada hii haijanikera kwasababu kutokuelewa kwako si kubaya sana,utaweza kueleweshwa tu kwasababu kuna tutakaofanya hivyo.We know you are a smart lady,you just need a little bit of brushin' in this arena.
Is it?? Nitasubiri huo msasa basi ndugu yangu.
Tatizo letu ni kwamba hatuna katiba ya kuwabana.Tunaweza kuweka ultmatum kwamba if you can't fix this problem,then we will fire you right away!Rais ni lazima aulizwe kila kitu,si kazi rahisi kuwa rais wa nchi masikini.Ni dedication,unaweza kufa kwa presha kama kweli umeingia madarakani kwa dhumuni la kuiongoza nchi yetu na kuindoa kwenye umasikini.
Hapo kwenye bold, nadhani ungevuta subira ukanisoma kwenye jibu langu kwa MwanaFalsafa ungeona ndicho i alluded to.
Imenisikitisha wewe kuja na kauli kuwa it is fair enough for the president to say that he is not capable of asking God to provide us with rain.Hii si caliber ya great thinking.Nasikitika kwamba ulianza kuwa defensive na kudai watu wasiweke maneno yasiyo ya lazima.I hope you will be patient and read what you dont like without getting personal.
I believe if you had practiced what you preach basi ungekuwa na subira na wala usingeweza kuwa judgemental. Pls read once more so that you can discover the "mischief" behind the thread!
Narudia tena dada yangu,hii issue si ya vyama vya siasa kama unavyotaka kuiweka.Tafadhali elewa kuwa tatizo si kutokuweza kwa JK kumwuliza Mungu kuhusu mvua(Tafadhali elewa hilo)
R u sure umenisoma na kunielewa au hata umewasoma waliochangia walionielewa?
Wewe unapoamini kuwa rais hatakiwi kuwa na majibu ya kila tatizo,unakuwa kama na wewe una tatizo la kuelewa kuwa issue ya umeme si just "Kila tatizo"
Mkuu, iweje unaniwekea maneno mdomoni? Please exercise your comprehension skills kabla ya ku attack wengine. Usilazimishe uelewa wako kuwa ni universal knowledge/understanding.
.Kwa kumalizia,naomba usijali kuhusu baadhi ya maneno niliyoyatumia kama utakuwa hujayapenda
Unaumizwa watu flani flani wakipigwa vijembe kidogo tu.Ndo jukwaa la siasa hakuna mapenzi humu.Rudi kwenye hoja na unieleze ni kwanini JK hatakiwi kuulizwa issue ya umeme.
Msome vyema WOS mkuu na bila cherry picking just because you wanna back her up.Nimekupata hata hivyo inawezekana hujampata..Hahahaaaa Meku bana...haya basi naumizwa watu flani flani wakipigwa vijembe.
JK hatakiwi kuulizwa peke yake issue ya umeme kwa sababu there is plenty of blame to go around. Matatizo ya uhaba wa umeme hayajaanza leo. Ni ya muda mrefu sana. Nakumbuka kwenye mwanzoni mwa miaka ya 90 mzee Mwinyi akiwa raisi mgao wa umeme ulikuwepo.
Nakumbuka kwa uzuri kabisa kwa sababu kipindi hicho mimi nilikuwa naishi Chuo Kikuu (la hasha sikuwa mwanafunzi kwa hiyo msianze ku imagine umri wangu lol) na tulikuwa tunapata 'preferential treatment' kwa sababu chuo kikuu kilihesabika kuwa kama moja ya sehemu muhimu ambazo zilistahili kuwa na umeme muda wote na hivyo adha ya mgao hatukuwa tunaipata kama ilivyokuwa kwa wengine. Kwa waliokuwa wakiishi chuo kikuu enzi hizo kama wana kumbukumbu nzuri basi watakubaliana nami kuhusiana na hili.
Sasa kwa mtaji huo utaona kuwa hili tatizo la umeme limekuwa tatizo lililowashinda wengi sana na hivyo haitakuwa haki kumnyooshea kidole mtu mmoja tu na kusema wewe ndiyo sababu ya yote haya yahusianayo na huu umeme wa mgao. Lakini pia naelewa kuwa lawama au pongezi they come and go with the territory kwa hiyo itakuwa vigumu sana kwa Kikwete kama raisi kuepuka kubebeshwa lawama hapa.
Jambo la msingi ni wadau wote (kwa hapa namaanisha wananchi wote) kukuna vichwa vyetu na kuja na ufumbuzi wa tatizo. Tusikilizane na tusibezane. Sote ni wadau kwenye hili. Na kuanza kunyoosheana vidole hakutatatua tatizo. Hebu fikiria mwenyewe, ukianza kunyoosha vidole vya lawama utaanzia wapi na kuishia wapi na mwishowe manufaa yake yatakuwa ni yapi?
Msome vyema WOS mkuu na bila cherry picking just because you wanna back her up.Nimekupata hata hivyo inawezekana hujampata..
Nakuhakikishia Mkuu NN kanipata bila chenga kabisa! Msome pia Mwanafalsafa1. Wewe ndio umemiss my point by far nahani umesoma ukiwa biased kuhusu uelewa wangu.Hint: read pia between the lines utanielewa vizuri.
.Na mkuu wangu narudia tena,huyu dada amefanya makosa makubwa sana kusema umeme ni just another tatizo.Hili ni tatizo la kimsingi na kuulizwa Mh Rais ni lazima aulizwe.Akikubali hilo tutakuwa msitari mmoja
Nakuhakikishia tena kwa mara nyingine sijakosea.Lakini kisomi wanasema " everybody is enttled to their opinion" kwa msingi huo u could be right kuona nimekosea.
However unaonekana umemesema zaidi na kama vile you have put words in her mouth.Sijali hilo kwa kuwa nilimweleza hapo awali kuwa atapata msaada.
He has not, and i dont want to believe that he has put words in my mouth.
Tuendelee na mjadala.
Sis WOS,Jmushi,
My compliments and respect to you as well!
Siwezi kujali bali nimekusahihisha pale nilipoona nawe umekosea hivyo nawe take it easy!
Nimekusoma na nimekupata vyema sana tu kuwa you are partially wrong.Ngoja nisubiri wachangiaji wengine.I am standing by my points tho, kwamba you are wrong kutaka ku conclude kuwa kulitakiwa kuwepo ushirikiano wa vyama ili kuweza kuliondoa tatizo la umeme.Nikakupa mfano kuwa vyama vingi vimeanza tu recently.Na kwa hivyo kublame kutokushirikiana kwa vyma ni upotofu.Na wengi wa wapinzani walikuwa CCM before.Sera za CCM hazijaweza kutuondolea tatizo tulilonalo.Ni kwamba hawajawa serious.Hawahitaji ushirikiano wa upinzani kama wana agenda ya kutosheleza.Na kukutoa wasiwasi kuhusu uelewa wangu nakuomba soma post yangu namba 9 utanielewa.
Thanks!
Ok sis,Tuko pamoja ndugu yangu JMushi1
WoS,
Nishati ni nyenzo muhimu sana katika maendeleo ya nchi. Nchi zote zilizopiga hatua zinalichukulia suala la nishati kama usalama wa taifa.
Tangu tatizo lilipoanza unaweza nchi imeathirika sana kiuchumi. Kama tungelikuwa na idara za uchumi na takwimu independently tungeona data za kutisha sana. TRA peke yake wanapoteza mabilioni , pesa zinazohitajika kuendesha serikali na kukabili nakisi inayozibwa na wafadhili.
Maisha ya wananchi yamebadilika sana kijamii na kiuchumi kuanzia inflation, employment n.k. Uwekezaji unaopigiwa debe sasa umekwama, nani atawekeza mahali pasipo na nishati ya uhakika? Tunaona makampuni yanakimbilia nchi jirani n.k. Kwa muktadha huu suala la nishati huwezi kulitenga na usalama wa taifa kiuchumi na ni hapo linaangukia mikononi mwa Rais na serikali yake.
Katiba iliyopo Rais ana mamlaka yote kuliko chombo kingine. Mfano, alipotakiwa kuwawajibisha walioshiriki kuhujumu nishati ,kwa mamlaka yake aliwaacha wastaafu na wengine hawakuchukuliwa hatua. Kumbuka yeye ndiye mwenyekiti wa baraza la mawaziri linaloidhinisha miradi mikubwa kama ya nishati na yeye ndiye anayeidhinisha malipo au madeni ya nchi. Inaweza kuwa siye anayesaini lakini afanyaye hivyo ana baraka zake zote. Hili linajibu swali la awali kuwa nani alaumiwe kwa tatizo.
Alipochaguliwa alijua tatizo na alikuwa na majibu ambayo wananchi wanayataka(rejea ilani ya uchaguzi). Hakuchaguliwa kutueleza chanzo cha tatizo bali suluhisho. Inapotokea nchi yenye upepo, natural gas, coal na wind inaingia gizani na jibu la Rais ni kumlaumu mungu inasikitisha. Yaani kwa mamlaka na uwezo wake wote aliopewa na katiba anashindwa kutumia rasilimali za mungu badala yake anakimbilia kumlaumu !hapo kuna tatizo, tena kubwa.
Ushirikiano wanaotoa wapinzani haupokelewi. Wanaposema wezi na wahujumu wa nishati wafikishwe mbele ya sheria na ikiwezekana wafilisiwe, serikali na rais wanatumia siasa kuwakejeli.
Kwa nchi za wenzetu mawazo ya wapinzani huchukuliwa na kufanyiwa kazi,hapa kwetu hilo litahatarisha uwepo wa baadhi ya watu mjengoni Dodoma, hivyo ni bora kuwakabili wapinzani na si kutatua matatizo ya umeme.
Mikataba ya nishati inapofanywa siri ili kuwalinda wahalifu tutarajie wapinzani wafanye nini zaidi? Ndio, ushirikiano unahitajika lakini hakuna utayari wa kushirikiana kama Rais alivyomkejeli Mnyika na waziri wake kumkejeli Mbowe.
Lazima tukiri kuwa hapa tulipo ingawa bado tupo porini, vyama vya siasa kama Chadema vimesaidia sana kupaza sauti na kuamsha CCM. Sakata la Jairo na Ngeleja limeungwa mkono na CCM kwa hofu ya upinzani kulifanya ajenda. Ni kweli safari yetu hasa ya vyama vya upinzani ni ndefu lakini tuwashukuru kwa kile kidogo wanachokifanya kwa uchache wao chini ya ubabe wa bunge la CCM na spika wake.
Rais wa nchi hapaswi kulalamika au kutoa visingizio kwa kushindwa kutatua tatizo. Hakuchaguliwa kuwa kiongozi wa kidini anayetukumbusha kazi ya mwenyezi mungu. Amechaguliwa kutatua matatizo ya wananchi kwa kushirikiana na wenzake.
Kama Kenya kuna ukame na umeme upo, kwanini tumlaumu Mwenyezi mungu kwa ututusa wetu?
Katiba yetu inampa mamlaka yote na anabeba dhima kubwa ya kututatulia matatizo kwa heshima aliyopewa. Heshima inaambatana na kuwajibika na majukumu sio ving'ora, kwa hili la umeme hana jinsi ya kukwepa lawama na kushindwa kwake. Ni failure ya Rais kiuchumi, kisiasa na kijamii bila kumsingizia mwenyezi mungu.
Hata mimi nakubaliana nawe kuwa suala la umeme ni nyeti na siyo tatizo la kawaida.Linalenga kwenye usalama wa nchi kwa maana halisi. Kukosekana umeme kunahatarisha maisha ya watanzania.
Je rais wetu hawezi kuchukua hatua za dharura ikibidi hata kupunguza vifungu vya bajeti za wizara na kuelekeza nyenzo zote kuhakikisha tunapata umeme tunusuru uchumi na mengi yaliyomo hatarini?
Rais kasema tumpe mapendekezo ya jinsi gani kutatua tatizo. Nadhani moja ya pendekezo ni hili!
This is the saddest fact....nadhani viongozi wetu wafike mahali waone aibu!Kibaya zaidi wataalamu wamewekwa pembeni ili siasa ikidhi matakwa ya wahitaji.
Kumbuka pia tuna wasomi waliobobea katika uchumi, nishati, biashara n.k kutoka katika rasilimali watu na academicians. Rais hajawatumia hawa.
Kamati za bunge, shirikisho la wenye viwanda, wawekezaji kila mara wamekuwa na ushauri. Jambo la kusikitisha ni kuwa ushauri na maoni yao yanapofika mezani kwa mheshimiwa hukutana na nguvu kubwa ya kisiasa na huwekwa pembeni.
Hili nalo neno! Nakumbuka hata hapa JF kuna mada iliwahi kuanzishwa na tukampata Eng.Nsiande mwana JF mwenzetu akatoa insights nzuri sana kama mtaalamu ndani ya TANESCO kuonyesha kwamba kuna zaidi ya yanayozungumzwa na wanasiasa.Sasa Mh.Rais anataka muujiza gani tena kama hataki kutuma wataalam au hata kusikiliza ushauri unaotolewa na wadau mbalimbali?
Rais anatakiwa atoke mbele, atangaze hali ya dharura, akutane na wadau wa sekta ya nishati, wanataaluma,wanasiasa makini na wafanyabiashara wenye nia njema walizungumze tatizo na kupata ufumbuzi wa muda mfupi na muda mrefu.
Atafanikiwa tu endapo atakubali kuweka siasa pembeni, kuacha wapambe na kuwa tayari kuchukua maamuzi magumu.
Laiti kama angesikia na kuchukua hatua za dharura maana wananchi sasa tumechoka na tunapoteza subira.
Hamna mshikamano kwenye jamii ya sasa. Dikteta na muwongo mkubwa Kikwete anadai kwenye mahojiano yake na BBC eti mwenye idea ya solution aljitokeze Serikali yake ipo tayari kusikiliza. Lakini ukweli ni kwamba kina Mufuruki wanaowakilisha sekta binafsi wamepiga kelele wee kuonyesha umuhimu wa Serikali kuwajumuisha wadau mbalimbali kwenye jamii kutafuta suluhisho la dharura la tatizo la umeme lakini hakuna dalili kuwa hilo limefanyika.
Sijui kama hajawasikiliza wadau hawa wenye uelewa mpana wa tatizo, anataka nani tena amshauri!
WoS,
OUr Dear leader has no clue about nothing!
MHH! Yangu macho na masikio tu...... sina la kusema
Hata sijaona swali hapo zaidi ya maelezo mareeeeefu yaliyopindapinda kama Mizengo