Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Mimi nawashauri viongozi wa vyama vya CHADEMA,NCCR na CUF wasiwe na matumaini kwamba Raisi Kikwete atawasikiliza na kwamba hatasaini muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba.
Raisi Kikwete ndie mwenyekiti wa CCM taifa na huu ni mkakati wa CCM kwahiyo wanachofanya wabunge wa CCM ni kutekeleza tu mkakati wa chama chao na hivyo Kikwete kutosaini itakuwa ni sawa na kuwasaliti wana CCM wenzake wakiwemo hao wabunge wa CCM waliopitisha muswaada huo.
Pia ifahamike kuwa serikali ya Kikwete imekuwa ikitegemea wabunge wa CCM kupitisha mambo yake ndani ya bunge na kwa maana hiyo si rahisi kwa Raisi Kikwete kuwaudhi wabunge ambao siku zote ndio tegemeo lake ndani ya bunge.
Atakachofanya Kikwete sana sana ni labda kuwaita wapinzani Ikulu kama ushahidi tu na kuwaridhisha licha ya kauli ya Wassira kwamba hatutawaita tena wapinzani Ikulu.Atakaa nao Ikulu wataongea lakini mwisho wa siku atasaini tu kama alivyowahi kufanya siku za nyuma juu ya swala hilo hilo la Katiba alipokutana na CHADEMA.
Raisi Kikwete siku zote ni mtu wa kuangalia upepo na huu muungano wa wapinzani juu ya katiba si wa kuupuza na hivyo ile kauli ya waziri Wassira haitafanyiwa kazi.Na pia naamini ile kauli ya Wassira ni kauli ya Kikwete.
Tusijdanganye,hakuna tofauti kati ya Kikwete na wabunge wa CCM katika swala la katiba.Kama ni kutosaini ni lazima Kikwete ashauriane na chama chake na si vinginevyo hata ikibidi kwa siri.