Kwa kweli haka kajitabia sio kazuri kwa sisi wanawake ambao tumechumbiwa
Umechumbiwa, kila hatua imefanyika na harusi imepangwa bado tu humuachi boyfriend wako
Na hii tabia ya kumuaga boyfriend wako kwa kumpa papuchi na huku kesho au siku mbili zijazo utakuwa kwa mumeo si tabia nzuri hakika kwa kisingizio cha kuagana ni ujinga
Ukichumbiwa achana na boyfriend, wengine watakuharibia ndoa yako
Wengine wakisha olewa wanapanga ratiba ya kwenda nyumbani kwao kisingizio cha kwenda kumsalimia mama kumbe anaenda kwa boyfriend wake wa huko nyumbani kwao
Hii inawahusu wale wenye wachumba ambao wanakaa (Distance) mkoa kwa mkoa,mji kwa mji au nchi kwa nchi,kijiji kwa mji,kijiji kwa kijiji,hii tabia ni mbaya
Jifunze kuacha