Kumuangalia vyema mtoto wako

Kumuangalia vyema mtoto wako

aisee is true mie kabla sijakuwa na mtoto sikujua
kama mtoto anakuwa na value kubwa hivvyo lakini sasa
lahaula namaliza vocha kumpigia dada wa kazi
is like im crazy fo her .babake cina mda nae kwakweli
upendo wa mama unakuja automatical nimekuja ku realize hakuna kama mama
 
aisee is true mie kabla sijakuwa na mtoto sikujua
kama mtoto anakuwa na value kubwa hivvyo lakini sasa
lahaula namaliza vocha kumpigia dada wa kazi
is like im crazy fo her .babake cina mda nae kwakweli

Jitahidi kuwa karibu naye usije ukafanya kosa la kumweka kando hao ni watoto wako wawili tayari mmoja mkubwa mwingine mdogo
 
Kumuona Daktari

Kuchagua daktari wa mtoto



Unatakiwa kumchagua daktari wa mtoto wako kama ungali mja mzito miezi 3 kabla ya kujifungua. Waulize marafiki, jamaa au daktari wako. Waweza kupata matibabu ya bure kwa watoto wachanga kutoka kwa hospitali za mikowa au kliniki za jamii, kwa malipo ya chini katika hospitali za serikali. Mchaguwe daktari uliye na imani naye aliyemzuri mwenye kuelewa na maono tofauti na pana.

Uchunguzi wa mara kwa mara

Mtoto wako anahitaji kuonekana na daktari kila mara ili akuwe kwa raha na afya. Watoto wana ratiba yao ya kupelekwa kwa daktari.

Kati ya masaa 24 baada ya kuzaliwa
Siku 2-4 baada ya kuzaliwa ikiwa mtoto atapelekwa nyumbani chini ya masaa 48 baada ya kuzaliwa.
Wiki 2-4
Miezi 2
Miezi 4
Miezi 6
Miezi 9
Miezi 12.

Unachotarajia kwa uchunguzi wa kila mara

Kila uchunguzi daktari hutizama urefu wa motto,uzito,na kichwa cha mtoto ili kufahamu jinsi motto anvyokuwa.Daktari pia atachunguza macho ya mtoto, masikio, mapafu, moyo, mdomo, sehemu nyeti na tumbo. Katika muda wa mwaka mmoja mtoto wako antakiwa kukaa,kugaagaa na kujivuta mwenyewe hadi asimame.

Chanjo:

Mtoto kupelekwa kupata chanjo ni muhimu, inapendekezwa watoto wapate chanjo hizi kuzuia maradhi kuhatarisha maisha yao.

Homa ya manjano B (Hepatitis)
Dondakoo, Pepopunda na Pertussis – Diptheria, Tetanus, Pertussis (DTP)
Polio
Surua, matumbwitumbwi, Rubella – Measles, Mumps, Rubella (MMR)
Haemophilus influenzae type B (HIB)
Varicella, Tetewanga – Chicken Pox

Kumpeleka mwanao nyumbani
Mtoto aliyezaliwa anajiratibisha na ulimwengu ulio tofauti na joto na usalama wa tumbo la mamake. Watoto hawa wanastahili kupendwa,kulishwa, kuwekwa safi na wakiwa na joto inayofaa. Kuna mambo mengi mapya wazazi wanapaswa kujua.

Afya ya mwanao

Unafaa kumwita/kumpigia simu daktari wako kama utaona uafuatayo kwa mwanao:

Kukosa kula/kukataa chakula
Kuwa na rangi isiyostahili
Nguvu kidogo
Joto la juu ya 380c chini ya kwapa
Ghasia/fujo zisio za kawaida
Kulala zaidi ya kawaida
Kutapika au kuhara
Shida za kupumua

Kuwaelewa Watoto

Kumuelewa mtoto wako ni muhimu sana, ili kushughulikia mahitaji yake. Watoto ni tofauti kuelewa ishara zake kutaendelea katika kila kiwango. Ikiwa una haja ya kufahamu tabia za mwanao, muite daktari wa watoto au nenda katika kliniki ya jamii.

Mtoto wako anvyokua na kubadilika hata ishara zake zitabadilika, lakini miezi michache ya kwanza kulia kutakuwa ndio njia ya pekee ya mawasiliano.

Kumliwaza mtoto wako anapolia

Hata kama mtoto haumwi na tumbo , kumnyamazisha motto anayelia ni vigumu sana . Kama umejaribu kila mbinu na hujafaulu , jaribu yafuatayo:


Mfunge mtoto kwenye vitambaa au blanketi ili ahisi joto kiasi na atulie.
Jaribu kucheza muziki muororo au muimbie nyimbo za kumbembeleza.

Mbebe kwa makini au nenda matembezi naye katika gari lako na hakikisha umemkalisha nyuma.
Kumkanda mgongoni au tumboni kwa weza kumliwaza hasa kama ana hewa tumboni.

Kumnyonyesha
kwa weza kutuliza mdundo wa roho yake kutuliza tumbo lake na viungo pia.
Habari njema ni kuwa watoto hupita hatua hii wanapokuwa. Mtoto wako anapokuwa wiki 6 au 8 watakuwa katika hali ya kuweza kujiliwaza na kulia kwingi kutakwisha.

Kwa Nini watoto Hulia?

Njaa:
Mtoto anaweza kuwa njaa.Watoto hula kama mara 8 hadi 12 kwa siku wanaponyonya,na mara 6 hadi 10 kwa siku anaponyonya chupa.

Nepi chafu: Mtoto hana raha anapokuwa kwa nepi chafu, akiachwa kwa muda mrefu ataambukizwa vipele.Mbadilishe nepi kila wakati.

Baridi au joto: Watoto wana ngozi nyororo na hupata baridi haraka.Wanahitaji kufunikwa vyema lakini sio kupita kiasi.
Umakinifu: Watoto wanachoka watalia.Mchukuwe na umpapase mgongoni ili afahamu upo.

Ugonjwa: Mtoto wako anaweza kuwa mgonjwa ,mtizame joto la mwili na wasiliana na daktari.
Hewa tumboni: Watoto wachanga huhitaji kukandwa kila mara au la hewa humjaa tumboni na kumpotezea starehe.

Usingizi: Mtoto akiwa amechoka na ana usingizi atalia,jaribu kumlaza apate usingizi.
Nitafanya nini ikiwa mwanangu bado yuwalia?

Pengine hutagunduwa kwa haraka shida zake, umejaribu mbinu zote na hajanyamaza. Anaweza kuwa na msokoto wa tumbo kwa masaa 2 au 3 kwa siku mara tatu kwa wiki. Msokoto wa tumbo humuondokea mtoto anapotimiza miezi 4.
Mtoto mchanga kupata tabu wakati wa kulia sauti haitoki ipasavyo na inakuwa kama inakatikia njiani tatzo ni non?
 
Back
Top Bottom