wana jamvi tusaidiane hii scenario,nimekua nina mpenzi kwa muda wa miaka 2 sasa huu waenda 3,katika muda wote huo nimekua nikiona mapungufu mengi lakini mengine nimeyamezea na kuyavumilia kwani ndio kwanza tulikua katika take off now sasa ndo tuko highway kuelekea kule kwa sahihi yaani ndoa.
Sasa kinachonitisha kati yangu na huyu mdada ni kua hayuko aggressive katika mambo yaani amepoa sana.Yeye kila kitu kinachohitaji effort anakua hawezi au sio makini.Example baada ya kumaliza shule yake amekua katika mchakato wa kusaka ajira lakini cha kushangaza ni kua uombaji wake huambatana na makosa ya hapa na pale mpaka binafsi niamue aidha kuedit au kutuma cv yake kwa kampuni husika.Kwa sasa anafanya kazi katika kampuni moja ambayo kila kukicha analalamika hawajampa ajira nimekua nikijitahidi kumtumia matangazo ya kazi ili awe anaomba lakini amekua haombi hizo kazi kwa kisingizio cha kua amesahau au eti ana mambo mengi kiasi cha kushindwa kuapply.
Kilichoniudhi zaidi ni pale alipofikia hatua ya kupoteza cheti chake cha kuzaliwa wakati ni muhimu sana katika maombi ya fursa mbali mbali.
MBAYA ZAIDI haonyeshi kuappreciate kile nikifanyacho ili aweze kupata kazi nzuri anadai siko supportive to her while matangazo yote mie ndo nayatafuta,kazi zingine mie ndo ninaziomba kwa niaba yake,pia mie ndo natuma appliation zote kwa njia ya posta etc.
JE HUYU NI MWANAMKE ANAEFAA KWA MTU AMBAE NI AGGRESSIVE KATIKA MAISHA YA KILA SIKU?
Kwani haeleweki kabisa kiperformance nikimaanisha kua kila utakachomwagiza afanye then wasi wasi hunijia kama atafanya kwa usahihi kama inavyopaswa,kwa mfano unamwagiza aombe kazi anaweza tuma cv na covering letter akasahau vyeti.
Je ni sahihi kama nikijitoa katika maisha yake?as tukiachana kwani binafsi ni mtu ambae nahitaji mwanamke ambae ni mpiganaji kweli sio ambae kila kitu anahitaji monitoring au usimamizi.
Wadau nikwamueni/.