Kumwelewa Mbowe au CHADEMA si kwa kila mtu

Kumwelewa Mbowe au CHADEMA si kwa kila mtu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Wamesikika chawa wa Mama wakijinasibu na tafsiri zao kuhusiana na alichosema Mbowe Mwanza.

Kwamba Mbowe kalazimika kusema kushughulika na CCM ni kama hivi:

FnDpVh9XoAAQkab.jpeg

Na bado chawa wa Mama wanakenua?

Wanaelewa uzito wa kauli kama hii ukizingatia Mbowe ni mtu mzima mwenye familia yake?

Si kuwa kauli hii inalenga kuonyesha ma CCM ni watu wa namna gani yanapokuja maslahi ya taifa?

Kwamba Mbowe kasema anayaheshimu sana maoni ya wengine japo msimamo wake ni kama alivyouweka wazi, na bado chawa wa Mama wanakenua?

Kumbe demokrasia maana yake nini? Au si kuwa kumbe katika CHADEMA uchawa hauna nafasi?

Kwamba Mbowe anasema ni lazima tuachane na mapande mapande ya uvyama katika kuwakabili CCM, na bado chawa wa Mama wanakenua?

Kwamba Mbowe kawasifia Samia na jeshi la polisi na Chawa wanakenua? Kwani haikuandikwa adui yako mpende?

Chawa hawa wanaelewa uzito wa kauli kama hizi kutoka kwa mtu mzima?

Chawa wa Mama wanajua kushindana kwa hoja ndiyo ulio msingi mkuu wa chama hiki ambako kumbe uchawa ni machukizo kwao?

Chawa hawa si kumbe ni kama nyani tu, washingiliao kuungua kwa miti porini?
 
Kichawa chawa wenyewe sasa watagutuka kudhani wametukanwa.

Zingatia Mbowe kama mtu mzima itakuwa imemuwia vigumu mno kuutumia mfano huo kuwaelezea ndugu hawa wasiojali maslahi ya taifa.
 
Siasa ni mazungumzo na mazungumzo, yanahitaji ushawishi, dalili zozote za kutaka kukimbia mazungumzo ni uoga usiokuwa na maana, kuwa mwanasiasa kamili lazima uwe na mbinu zaidi ya moja za kukuwezesha kuyafikia malengo uliyojiwekea.
 
Duh!

Hizi 'spin' zitakuwa nyingi sana nyakati hizi.

Kila mtu atapenda kutia maana ya aliyosikia yakisemwa anavyoona inampendeza yeye hata kama haileti maana yoyote!

Yaliyotamkwa na Mbowe katika hotuba zake za hivi karibuni hadi wakati huu haihitaji utaalam maalum kuonyesha jinsi gani CHADEMA inavyotoka kwenye reli taratibu.

Zitatolewa 'sipn' za kila aina, lakini hizo hazitabadili mwelekeo huo wa chama, kama ndio watakaokubaliana nao.
 
Ninakazia:

"Chawa wa Mama wanaelewa uzito wa kauli kama hii ukizingatia Mh. Mbowe ni mtu mzima mwenye familia yake?"

Hiiiiiii bagosha!
 
Duh!

Hizi 'spin' zitakuwa nyingi sana nyakati hizi.

Kila mtu atapenda kutia maana ya aliyosikia yakisemwa anavyoona inampendeza yeye hata kama haileti maana yoyote!

Yaliyotamkwa na Mbowe katika hotuba zake za hivi karibuni hadi wakati huu haihitaji utaalam maalum kuonyesha jinsi gani CHADEMA inavyotoka kwenye reli taratibu.

Zitatolewa 'sipn' za kila aina, lakini hizo hazitabadili mwelekeo huo wa chama, kama ndio watakaokubaliana nao.

Unasomeka ila nikuombe kuiona tafsiri hii kwani bila ya tahmini yakinifu, mengine ni kelele za chura tu.

"Tathmini yakinifu uzinduzi wa mikutano ya siasa Mwanza"​

https://www.jamiiforums.com/threads/tathmini-yakinifu-uzinduzi-wa-mikutano-ya-siasa-mwanza.2058702/
 
Unasubiri fadhira ya CCM, 'mkuu mcharo son'? Huipati.
Kwa hiyo niandamane kuidai? Ndio mlitaka Mbowe afanye siasa hizi zilizoshindikana za kutishia maandamano na watanganyika nyie!!
Mboe yupo sawa na kama unaona si sawa, basi ujue ni sawa sawa
 
Unasubiri fadhira ya CCM, 'mkuu mcharo son'? Huipati.

Mkuu unasoma wapi inaposubiriwa fadhila ya CCM na nani?

Kwani karata, chess au draft linavyochezwa si ndiyo hivi alivyosema Mbowe?

FnDpVh9XoAAQkab.jpeg
 
Siasa ni mazungumzo na mazungumzo, yanahitaji ushawishi, dalili zozote za kutaka kukimbia mazungumzo ni uoga usiokuwa na maana, kuwa mwanasiasa kamili lazima uwe na mbinu zaidi ya moja za kukuwezesha kuyafikia malengo uliyojiwekea.

Hotuba ya Mbowe ilijikita kwenye kuelezea mikutano ya maridhiano, hali ya washiriki na njia za kupata ushindi.

Kutokea kwenye hotuba yake sasa tunajua:

1. CCM ni wagumu na hawataki maridhiano.
2. Tulipo ashukuriwe Samia siyo CCM.
3. Ushindi wetu utahitaji mashirikiano na vyama vingine.
4. Kwenye mapambano tuwe tayari kukubali kutokubaliana.

Itakuwa ajabu kama chawa wa Mama hawakuyaelewa hayo.

Cc: Kalamu
 
Kwa hiyo niandamane kuidai? Ndio mlitaka Mbowe afanye siasa hizi zilizoshindikana za kutishia maandamano na watanganyika nyie!!
Mboe yupo sawa na kama unaona si sawa, basi ujue ni sawa sawa
Sijasema chochote kuhusu "kuandamana", kama hiyo ndiyo njia unayoiona wewe kuwa mbadala wa hayo anayofanya Mbowe sasa, mimi sioni hivyo.

Natumaini akili zitamrudia hivi karibuni, kwani asitegemee chama chake kupata fadhira toka kwa CCM; hata hii CCM ya Samia.

Ataambulia mipasho tu, na vizawadi vya hapa na pale, basi!
 
Mkuu unasoma wapi inaposubiriwa fadhila ya CCM na nani?

Kwani karata, chess au draft linavyochezwa si ndiyo hivi alivyosema Mbowe?

View attachment 2491914
Mkuu, hii nimeiona leo, na bado haijanishawishi juu ya chochote kuhusu "mapambano" kama anavyoyaita Mwenyekiti kuwa anazo njia mbadala za kutongoza demu ambaye alishaota usugu kwa kusikia maneno matamu mengi maishani mwake.
 
Mkuu demu mbona kaingia kingi na ndiyo maana anasifiwa.

Misahafu si inasema adui mpende? Uswahilini wanasema adui yako akikusifu ujue umeuvaa mkenge?

Kwanini hatuoni kutokana na maridhiano mikutano iliyokuwa imezuiliwa kinyume cha sheria sasa imeruhusiwa.

Waliokuwa wanashikiliwa wameachiwa.

Waliokuwa uhamishoni wanarudi.

Polisi waliokuwa hostile sasa hivi wanatoka vingine

Nk nk.

Kwani ushindi ni nini kumbe?
 
Hotuba ya Mbowe ilijikita kwenye kuelezea mikutano ya maridhiano, hali ya washiriki na njia za kupata ushindi.

Kutokea kwenye hotuba yake sasa tunajua...
Sasa unanifanya nikiamini nilichowahi kudhani kitatokea kwenye haya tunayoshuhudia sasa.

Kwamba siasa za Kenya zimeingia Tanzania, kwa kuanza na CCM ya Samia kuungwa mkono na CHADEMA ya Mbowe, wanaungana kutafuta kura 2025 kwa pamoja.

Hayo mabaki ya CCM ya Magufuli, siyaoni yakijisogeza kwa CHADEMA aliyoiacha Mbowe nyuma.

Huu ndio uelewa ninaoupata ktokana na hayo uliyoyaeleza hapo juu.

Hata hivyo, nimekwishagusia huko nyuma jinsi Samia alivyomnyang'anya ajenda Mbowe, kiasi kwamba hakuna sababu wala hoja pinzani anayoweza kuitumia Mbowe dhidi ya Samia.

Kwa hali hiyo, kwa nini asiungane naye?
 
Sijasema chochote kuhusu "kuandamana", kama hiyo ndiyo njia unayoiona wewe kuwa mbadala wa hayo anayofanya Mbowe sasa, mimi sioni hivyo.

Natumaini akili zitamrudia hivi karibuni, kwani asitegemee chama chake kupata fadhira toka kwa CCM; hata hii CCM ya Samia.

Ataambulia mipasho tu, na vizawadi vya hapa na pale, basi!

..kuna juhudi kubwa sana toka kwa wapambambe wa Ccm kuwakatisha tamaa Chadema.

..Chadema wanapaswa kuwa makini na zaidi kuwa wamoja ktk kipindi hiki.

..Mpaka sasa hivi sijaona chama chochote chenye hoja mbadala wa zile zilizotolewa na Chadema.
 
Mkuu demu mbona kaingia kingi na ndiyo maana anasifiwa.

Misahafu si inasema adui mpende? Uswahilini wanasema adui yako akikusifu ujue umeuvaa mkenge?

Kwanini hatuoni kutokana na maridhiano mikutano iliyokuwa imezuiliwa kinyume cha sheria sasa imeruhusiwa.

Waliokuwa wanashikiliwa wameachiwa.

Waliokuwa uhamishoni wanarudi.

Polisi waliokuwa hostile sasa hivi wanatoka vingine

Nk nk.

Kwani ushindi ni nini kumbe?
Imenilazimu nicheke kwa haya uliyoweka hapa.

Kwa hiyo CHADEMA weshapata ushindi kwa kuwa na HAKI yao iliyoporwa kinyume cha sheria?

Mtu anakukandamiza, kwa maksudi kabisa, halafu anakwambia, haya sasa nakupumzisha maumivu yako. Wewe hapo unadai umepata ushindi?

Nadhani kuna kitu tunapishana hapa bila kujua/kukusudia.

Naomba usinielewe kwamba CHADEMA wasiwe na shukrani kwa hayo yanayotendwa na Samia; lakini hiyo haina maana ya wao kutoka kwenye mipango yao kichama, malengo yao kichama kwa vile tu wametendewa wema.

Na wala sipendekezi chochote kwa CHADEMA wafanye siasa za vurugu wakati hakuna sababu tena za kufanya hivyo.

Lakini, kama kweli wao kama chama wanajiona kwamba wana ajenda muhimu zaidi kwa waTanzania, ajenda ambazo CCM imeshindwa kuzitimiza, kwa nini wasizifikishe kwa wananchi wapewe ridhaa na wananchi wenyewe.
 
Swali nalojiuliza wale waliyokuwepo kwenye ule mkusanyiko wa ule mkutano nao walielewa au nao walitoka kapa?
 
Back
Top Bottom