Kumwelewa Mbowe au CHADEMA si kwa kila mtu

..kuna juhudi kubwa sana toka kwa wapambambe wa Ccm kuwakatisha tamaa Chadema.

..Chadema wanapaswa kuwa makini na zaidi kuwa wamoja ktk kipindi hiki.

..Mpaka sasa hivi sijaona chama chochote chenye hoja mbadala wa zile zilizotolewa na Chadema.
Ninakubaliana nawe juu ya "juhudi toka kwa wapambe wa ccm", hili lipo wazi na lenye kutegemewa liwepo.

Lakini wakati huo huo, CHADEMA, na hasa Mwenyekiti wao nao inawalazimu kuchukua tahadhari, wasijikute wameingizwa chakani bila ya kutegemea.
 
Binafsi nimeandika nyuzi mbili kuhusiana na hotuba ya mheshimiwa huyu.

Mmoja ni huu wenye kuyaweka maneno yake tu kama yalivyo katika kuonyesha kuelewa yahitaji kuwa angalau zaidi ya Tom, Dick na Harry.

Uzi mwingine ulihusika na tahmini yakinifu kuhusiana na hotuba hiyo.

Ninakazia, bila ya tahmini yakinifu, mengine yatakuwa ni kelele za chura tu. Ndiyo maana usipoangalia waweza kujikuta ukicheka bure:

"Tathmini yakinifu uzinduzi wa mikutano ya siasa Mwanza"​

https://www.jamiiforums.com/threads/tathmini-yakinifu-uzinduzi-wa-mikutano-ya-siasa-mwanza.2058702/

Nikuombe tens kuupitia uzi wa pili huu, ambapo ninakubaliana nawe na pia Mh. Mbowe kuwa katika demokrasia tufike mahali tukubali kutokubaliana.

Niweke angalizo:

Hata miye binafsi kuna niliyo na matatizo nayo na hotuba yake.

Ikumbukwe uchawa ni machukizo kwetu.
 
..kuna juhudi kubwa sana toka kwa wapambambe wa Ccm kuwakatisha tamaa Chadema.

..Chadema wanapaswa kuwa makini na zaidi kuwa wamoja ktk kipindi hiki.

..Mpaka sasa hivi sijaona chama chochote chenye hoja mbadala wa zile zilizotolewa na Chadema.
Ninakazia:

Bila ya tahmini yakinifu, mengine ni kelele za chura tu.

"Tathmini yakinifu uzinduzi wa mikutano ya siasa Mwanza"​

https://www.jamiiforums.com/threads/tathmini-yakinifu-uzinduzi-wa-mikutano-ya-siasa-mwanza.2058702/
 
Nitakusoma mkuu, nitakapopata nafasi.
Lakini sioni mahala popote zinapopigwa "kelele za chura", sijui una maana gani na hayo maneno.
 
Nitakusoma mkuu, nitakapopata nafasi.
Lakini sioni mahala popote zinapopigwa "kelele za chura", sijui una maana gani na hayo maneno.
Kelele za chura ni usemi ulio na maana Ile Ile na ule usemao maneno matupu hayavunji mfupa.

Kwamba kuna yaliyo tangible aliyopata Mbowe dhidi ya mengine asemayo awaye yote, ndipo ilipo tofauti ya kelele za chura.

Au wewe huoni hivyo mkuu?
 
Kelele za chura ni usemi ulio na maana Ile Ile na ule usemao maneno matupu hayavunji mfupa.

Kwamba kuna yaliyo tangibles alizopata Mbowe dhidi ya mengine asemayo awaye yote, ndipo ilipo tofauti ya kelele za chura.

Au wewe huoni hivyo mkuu?
Lugha yako ni ngumu; au uandishi wako unaniwia vigumu kukuelewa, na mimi siyo mtu asiyekuwa na uwezo wa kuelewa jambo ninalosoma au kusikia. Ninajiamini sana kwa hilo.

Nimesoma mara mbili hiyo unayoiita wewe kuwa ni "tathmini...".

Sikuona kitu cha kunishawishi kwamba kweli hiyo ni tathmini" ya hotuba aliyoitoa Mbowe mjini Mwanza.

Ni kama nilivyosema hapo mwanzo, pengine ni staili ya uandishndiyoi inayoniwia ngumu.

"Kwamba kuna yaliyo 'tangibles'alizopata Mbowe dhidi ya mengine asemayo wawye yote, ndipo ilipo tofauti ya kelele za chura"??
 
Ungekuwa umeweka japo mifano ulipo ugumu wa maandiko yangu, ninaamini ningefafanua. Sina ninachoficha katika maandiko yangu kwani ninaamini katika ninachokiandika kwa dhati ya moyo wangu.

Nikiazima maneno ya Prof. Shivji, "mimi pia si mwana muziki."

Kumbuka ni mwana muziki pekee anayeweza kutegemea kushangiliwa Kwa kila jambo.

Hata kwa bandiko linalo wachoma watu kumoyo kama ndiyo ulio ukweli wenyewe huwa sina simile.

Msema ukweli si ni mpenzi wa Mungu?

Ni hayo tu mkuu.
 
Naona ulirejea kuedit reply yako baada ya majibu yangu. Una maana na miye nirejee ku edit nilichokuwa nimeandika?

NB: Paragraph yako hii ya mwisho sasa ni after thought.
 
"Msema kweli si ni mpenzi wa Mungu?"

Sijui nani aliyeyasema haya maneno. Najua msemo huu umekuzwa sana na Magufuli.

Lakini sina uhakika na ukweli juu ya "Mungu kuwa na hawa wapenzi."

Na pia, siamini kamwe, kwamba "...ni mwanamziki pekee anayeweza kutegemea kushangiliwa kwa kila jambo". Msemo huu hauna ukweli wowote ndani yake.

Nikubaliane nawe kwenye hili la kutokuwa na "simile"jambo ambalo ninaweza kukubali mfanano kati yetu.
 
Naona ulirejea kuedit reply yako baada ya majibu yangu. Una maana na miye nirejee ku edit nilichokuwa nimeandika?

NB: Paragraph yako hii ya mwisho sasa ni after thought.
Hapana, niliongeza tu huo mstari wa 'quote'; na hii ilifanyika kabla hujabandika mengine yaliyofuata.
Hakuna maana yoyote iliyobadilika katika niliyowasilisha mwanzo.
 
Nikujibu kwa nukuu kutokea kwa hotuba ya Mh. Mbowe.

"Tufike mahali tukubali kutokukubaliana."

Na huo ndiyo ulio ustaarabu.

NB: "Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu" si usemi ulioasisiwa na Magufuli.

Kwamba Mungu hana wapenzi yahitaji mrejesho kutoka kwake yeye mwenyewe.

Kwamba ni mwana muziki pekee anayetegemea kushangiliwa kwa kila jambo - mimi sijasema hivyo. Kulikoni kuwekeana maneno mdomoni?

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
 
Hapana, niliongeza tu huo mstari wa 'quote'; na hii ilifanyika kabla hujabandika mengine yaliyofuata.
Hakuna maana yoyote iliyobadilika katika niliyowasilisha mwanzo.
Hapana. Paragraph hiyo ingekuwapo kabla sijabandika ningekuwa nimeijibu na ingekuwa sehemu kwenye "quote" yako ambayo iliambatana na majibu yangu.

Ni wazi kuwa paragraph hiyo haikuwapo awali.
 
Kesho nitakuwa ni miongoni mwa tutakaofika nyumbani kwa Mbowe kumsikiliza.
P.
 
Utaanzaje kuelewa watu wasio na itikadi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…