Baada ya kuzuka minong'ono fulani kumhusu mtu huyu kuhusiana na kikao cha charura cha NEC kilichoitishwa bila agenda yake kutangazwa hadharani, namtafakari kwa makini mtu huyo, huku nikijiuliza kama kweli hii minong'ono inaweza kuwa kweli?, nikajijibu mwenyewe, minongono hiyo ni uongo na uzushi!, haiwezekani mtu anayemsaidia hivi bosi wake, kukisaidia hivi chama chake, kuisaidia hivi nchi yake, na kuwasaidia hivi Watanzania, halafu kakikundi cha watu, wanaoitwa chama chake, wakakutana na kutumulia Watanzania!.
Hiyo minong'ono hiyo ni uongo na uzushi kutaka tuu kutuletea taharuki, lakini hakuna kitu kama hicho!.
Mzee Pasco