Wadau wa JF nimefurahishwa na tangazo linalo rushwa na haki elimu dhidi ya mkanganyiko wa vitabu mashuleni.
"Kuna aina ngapi za misuli? "
Elimu yetu na kizazi kinachofuata imevamiwa. Huwa nashindwa kuelewa kama PhD zinatolewa kihalali hapa nchini au ni za kutunukiwa (sifa ).
Kampuni kama za Nyambari Nyangwine zinawashushia heshima wasomi wetu. Kudhihirisha hili unaweza kuangalia vitabu alivyotoa Nyambari Kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne hasa Science na hisabati.
Ukilinganisha vitabu hivi na vingine kama Principal of physics, aboot, nelkon, Lambert, artikson, understanding maths nk utaona mapungufu yanayosababishwa na waandishi wa kitanzania.
Ajabu ni kwamba pamoja vitabu hivyo kuwa chini ya kiwango lakini vina mkono na baraka za serikali. Wakuu wa shule wanalazimishwa kuvigharimia hivi vitabu ili vipelekwe mashuleni. Swali hapa ni je haya yote yanafanywa kwa maslahi ya nani ?
Kituko kingine kuondoa hadithi zote zenye kuhimiza uzalendo na mshikamano kwenye vitabu vya elimu ya msingi. Hadithi zinazo wamulika wala rushwa, mafisadi zimeondolewa kwenye mitaala.
Zamani mtoto alikuwa anajua kuwa rushwa ni adui wa haki, ukweli daima, uongo ni mwiko. Leo hii hakuna uzalendo. Elimu imechakachuliwa. Ualimu sio wito tena.
Na serikali inaamini kwa kuwabana waalimu kwa kuwaletea form za OPRAS na kuwalazimisha kwa kila hali huku wakiendelea kupata mishahara kiduchu, itaibuka na BRN ya kuchakachua.
Watanzania tuwe macho, elimu yetu inapelekwa kubaya.
Tumekwisha, ukisoma web ya wizara ya Elimu utaona pendekezo la kubadili michepuko kwa kidato cha kwanza mpaka cha sita. Kukuta HKP (history, Kiswahili, Physics) . CLF (chemistry, Language ,French ). HBK (history, biology, Kiswahili ) KLM (Kiswahili, Language, Maths ) na nyingine za aina hii.
Hiyo itakuwa Michepuko/combination mpya za BRN kuficha fedhuli ya masomo ya science kufanya vibaya