Kuna aina ngapi za misuli?

Kuna aina ngapi za misuli?

Aurora

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2014
Posts
7,308
Reaction score
5,272
Habari zenu.

Hivi inakuwaje kila shule ina vitabu vyake vya kufundishia wakati syllabus ni moja? Unakuta hata shule ziko jirani lakini wanafunzi wanatumia vitabu tofauti hawawezi hata kuazimana vitabu?

Hivi Elimu yetu inaelekea wapi?At the end of the day wanafunzi wanasemwa kwa kufeli wakati wanasoma vitabu tofauti lakini wanatakiwa kujibu mtihani mmoja?

Au hivi vitabu ni mradi wa mtu? KAZI IPO

Ni hayo tu.
 
Me kitabu changu kunasema kuna msuli milia tu😎
Ndio Bongo hii
 
Baby all bubble, have a lil chat a small huddle
Time to make money and more trouble
And we all hungry and all hustle
And we all humble, but together we got more
muscle
 
Baby all bubble, have a lil chat a small huddle
Time to make money and more trouble
And we all hungry and all hustle
And we all humble, but together we got more
muscle

naona kipaji kinakuja kwa kasi
 
haya matangazo yamehamia hadi huku! Haki ya elimu! Kwa mfano vile...!
 
  • Thanks
Reactions: lin
Yule Teacher yupo fresh sana kwa comedy hata kitaani ni mchekeshaji tu!!
 
[color=#ff804222]unaulinza swali?? au unatoa nduku nduku kuhusu mfumo wa elimu ya Kitanzania
sijakuelewa mkuu,


Heading Iko tofouti na main body [/color]
 
[COLOR=#ff804222]unaulinza swali?? au unatoa nduku nduku kuhusu mfumo wa elimu ya Kitanzania
sijakuelewa mkuu,


Heading Iko tofouti na main body [/COLOR]

vyote kwa pamoja,natoa dukuduku la mfumo mbovu wa elimu hapa TZ na mfano mzuri ni hilo tangazo la misuli lililoleta confusion darasani
 
1.Msuli ule wa kuvaa watu wa pwani
2.Msuli wa mwilini iko mingi hiyo
3. Msuli ya kusoma
 
Wadau wa JF nimefurahishwa na tangazo linalo rushwa na haki elimu dhidi ya mkanganyiko wa vitabu mashuleni.

"Kuna aina ngapi za misuli? "

Elimu yetu na kizazi kinachofuata imevamiwa. Huwa nashindwa kuelewa kama PhD zinatolewa kihalali hapa nchini au ni za kutunukiwa (sifa ).

Kampuni kama za Nyambari Nyangwine zinawashushia heshima wasomi wetu. Kudhihirisha hili unaweza kuangalia vitabu alivyotoa Nyambari Kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne hasa Science na hisabati.

Ukilinganisha vitabu hivi na vingine kama Principal of physics, aboot, nelkon, Lambert, artikson, understanding maths nk utaona mapungufu yanayosababishwa na waandishi wa kitanzania.

Ajabu ni kwamba pamoja vitabu hivyo kuwa chini ya kiwango lakini vina mkono na baraka za serikali. Wakuu wa shule wanalazimishwa kuvigharimia hivi vitabu ili vipelekwe mashuleni. Swali hapa ni je haya yote yanafanywa kwa maslahi ya nani ?

Kituko kingine kuondoa hadithi zote zenye kuhimiza uzalendo na mshikamano kwenye vitabu vya elimu ya msingi. Hadithi zinazo wamulika wala rushwa, mafisadi zimeondolewa kwenye mitaala.

Zamani mtoto alikuwa anajua kuwa rushwa ni adui wa haki, ukweli daima, uongo ni mwiko. Leo hii hakuna uzalendo. Elimu imechakachuliwa. Ualimu sio wito tena.

Na serikali inaamini kwa kuwabana waalimu kwa kuwaletea form za OPRAS na kuwalazimisha kwa kila hali huku wakiendelea kupata mishahara kiduchu, itaibuka na BRN ya kuchakachua.

Watanzania tuwe macho, elimu yetu inapelekwa kubaya.


Tumekwisha, ukisoma web ya wizara ya Elimu utaona pendekezo la kubadili michepuko kwa kidato cha kwanza mpaka cha sita. Kukuta HKP (history, Kiswahili, Physics) . CLF (chemistry, Language ,French ). HBK (history, biology, Kiswahili ) KLM (Kiswahili, Language, Maths ) na nyingine za aina hii.

Hiyo itakuwa Michepuko/combination mpya za BRN kuficha fedhuli ya masomo ya science kufanya vibaya
 
Kila ninapotaka kutoa hoja ya lile tangazo naishia kusa post za wengine kama nimelogwa vile lakini nashukuru kwako ndugu kuweka hapa.
message iwafikie

cc: waziri wa elimu shukuru kawambwa
 
Kila ninapotaka kutoa hoja ya lile tangazo naishia kusa post za wengine kama nimelogwa vile lakini nashukuru kwako ndugu kuweka hapa.
message iwafikie

cc: waziri wa elimu shukuru kawambwa


Tumekwisha, ukisoma web ya wizara ya Elimu utaona pendekezo la kubadili michepuko kwa kidato cha kwanza mpaka cha sita.

Kukuta HKP (history, Kiswahili, Physics) . CLF (chemistry, Language ,French ). HBK (history, biology, Kiswahili ) KLM (Kiswahili, Language, Maths ) na nyingine za aina hii.
 
What should be done?

Kingine tunaogopa mabadiriko.

Kuhusu vitabu, kila kitabu kina ubora wake, ukitaka kitabu bora, nunua kitabu cha aina ya Nelkon nk,

Taasisi inayo husika na masuala ya elimu Tz may be wamechoka, na suala la maslahi katika kampuni husika nalo linachangia.

Kitu kingine ni kwamba, mara nyingi huwa hatujari hata ubora wa uandishi wetu, tukiona kama unaeleweka basi tunafanya, mfano wewe hapo PHD umeiandika ndivyo sivyo, na hujali, you take it simple, sababu tumekuelewa ulitaka uandike nini, Phd.

Mfano mwingine, sisi watu wa sayansi, pH sacale huandikwa kwa herufi ndogo ya "p" na kubwa kwa "H" yaani hivi pH, lakini ukiangalia watu wengi wanavyo iandika utashangaa, and they dont care, si umeelewa?

Binafsi vitabu vya nyambari Nyangwine nilikuwa sipendi kabisaa kuvisoma, ila ndio vilivyopo na ndio vitabu vilivyo ruhusiwa na T.I.E, tufanyaje?

Tangazo la haki elimu liko sahihi, linatusaidia kujua mapungufu yetu katika sekta nzima ya elimu.
 
Back
Top Bottom