Tetesi: Kuna anguko kubwa la CHADEMA?

 
Bk 7 zawafanya muandike hata njozi hewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijuavyo Mimi
Watanzania wengi hasa wa hali ya chini hawana utamaduni wa kusoma vitabu, Ilani wala kuzijadili Sera za chama chochote kile hawana muda huo kabisa!.

Kwa sasa wamekata tamaa na wanachotamani ni kuiondoa CCM madarakani tu walau waangalie chama kingine mbadala kitafanya nini!!
Haijialishi upinzani kasimamishwa fisadi, mwizi au mwenye maadili, wawe na sera wasiwe na sera wanachotaka Ccm itoke kwanza madarakani!.

Hakika wameichoka sana CCM
Ndio maana walijitokeza kwa wingi kumpigia kura LOWASA bila kujali background yake.
Lakn wananyong'onyea zaidi pale juhudi zao znapokutana na bao la mkono mfano halisi ni hizi chaguzi ndogo zilizopita.

Ninachozani mimi, milango ikiendelea hivi hivi kufungwa hipo cku unyonge utawatoka na wataamua kutaka kuingia kwa kupitia madirishani.

Mungu ibariki Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…