Kuna askari wa Ukraine walivuka mto Dnipro waliko warusi halafu wakacheka kwa upumbavu wao

Kuna askari wa Ukraine walivuka mto Dnipro waliko warusi halafu wakacheka kwa upumbavu wao

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kikosi kidogo cha askari wa Ukraine hivi karibuni kilifanikiwa kuvuka mto Dnipro oblast ya Kherson kutoka upande wa Magharibi na kuingia Mashariki ambako ndiko ziliko ngome za jeshi la Urusi tangu walipoamua kuachia eneo hilo la mashariki ambalo halina umuhimu kwao kiulinzi.

Kikosi hicho mwanzoni kilikuwa tukio kubwa kwa jeshi la Ukraine linalokaribia kushindwa vita na habari zake kutajwa sana na raisi Zelensky wa nchi hiyo.

Ili kuendelea kuwepo eneo hilo inabidi waendelee kupata nyongeza ya mahitaji yao kila mara kama vile chakula,maji na mafuta kwa ajili ya majenereta. Kila aina ya msaada wanaohitja kuwafikia huwa unapigwa na kuzamishwa na jeshi la Urusi.

Kama kwamba Urusi iliwaachia wafike eneo hilo kwa makusudi wamejikuta wamezingirwa kutokea pande zote na kuishiwa na mahitaji huku adui akipiga maeneo yote yanayowazunguka na kushindwa kusonga mbele huku wakiwa hawana namna yoyote ya kurudi walikotokea.

Imebidi wakati mwengine watoe gharama zao kwenda kusaka mahitaji kwa kificho kwenye vijiji vya jirani.

Katika malalamiko yao wanasema karibu wote waliofika eneo hilo ni askari walioingizwa jeshini siku za karibuni na wangependa wapate msaada kutoka askari wenye uzoefu zaidi wa vita kuliko wao na ambao hawawaoni.

Wanashangaa kuona viongozi wa juu wa Ukraine wakiendelea kutangaza habari zao kama ni ushujaa lakini makamanda wao wameshindwa kabisa kuwapa msaada wala kuwaokoa.

Kutokana na hali hiyo wamepata fikra kuwa katika hatua hii jiliyofikiwa ya vita hakuna mawasiliano tena baina ya makamanda wa ngazi za jini na majenerali wa kivita ili kumpa taarifa kamili raisi Zelensky juu ya hali waliyonayo.

Ukraine war: Soldier tells BBC of front-line 'hell'

1701749763053.png
 
Mwanzo wa mwisho wa SMO unakaribia ila ukraine wakifanya ujinga wakutosalimu mpaka kufikia mwakani mwezi kama huu basi kauli za kina Medvedev zinaenda kutimia
Nanukuu alisema mpaka kufikia miaka mitatu ijayo hakutakua na taifa linaitwa ukraine
Elensky endelea kukamatia hapo hapo maana mabwana zako washaona hufadhiliki hubebeki wanaanza kukutelekeza mmoja mmoja tena kidogo kidoooogo
 
Back
Top Bottom