Jibu sahihi ni hapana; huwezi kuendesha bila ufunguo kwa sababu hutaweza kuliwasha na kuanzisha njia zote za umeme unatumika ndani ya gari.
Kuna ufundi wa kuvuta waya tatu kutoka kwenye engine compartment kwa kupitia kwenye firewall ambazo unaweza kuzinganisha ukiwa ndani ya gari na hivyo kuliwasha na kuliendesha; hiyo ni njia haramu ya kuweka ufunguo, ukifanya hivyo, hata kama inaonekana kuwa hakuna ufunguo, ukweli ni kuwa umeweka ufungua kwa njia ya mkato ya kuunganisha waya hizo. Kuanzia mwaka 2010, magari mengi yanatumia wireless keys ambazo dereva anakuwa nazo mfukoni ila kuliwasha anabonyeza kitufe tu ndani ya gari na kuanza kuendesha. Ingawa inaonekana kama vile hakuna ufunguo, ukweli ni kuwa kuna ufunguo ambao umeunganishwa kwa wireless. Dereva lazima awe na ufunguo huo mfukoni.
Jibu la mwisho ni kuwa Huwezi kuenedsha bila ufungua, ingawa ufunguo wenyewe unaweza kuwa ni physical au virtual.