Kuna awamu ilikaa miaka 4 na zaidi bila kuongeza mishara ya watumishi na pasipo kutoa nyongeza ya mishahara ya kila mwaka?

Kuna awamu ilikaa miaka 4 na zaidi bila kuongeza mishara ya watumishi na pasipo kutoa nyongeza ya mishahara ya kila mwaka?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Hivi tangu enzi za Mzee Mwinyi kuna awamu kweli iliwahi kutelekeza watumishi wa umma kwa kiwango hiki tunachokiona katika awamu hii?

Yaani wakati mishahara serikalini ikifahamika kuwa ni midogo,mtu unaamua kuifanya iwe duni zaidi kwa kutoa hata annual increment?

Je,huku sio kukosa ubinadamu na kutojali hali ya maisha ya watu wengine?

Kama haitoshi,bado ukaongeza makato kwa ajili ya kulipia mikopo ya Bodi ya Mikopo kutoka asilimia 8 mpaka 15!!!!

Kwa hakika huku ni kutokujali maisha ya watu kwa kiwango kikbubwa sana!!
 
Awamu hii kuna kukundi cha watu wachache Sana ndicho wanachojaliwa na kuthaminiwa.
Hao wanachukuliwa kuwa wazalendo halisi na wachapakazi waliotukuka.
Hao swala la maslahi sio tatizo kwao maana ndio wajenzi halisi wa hii Nchi.
Wengine fungeni mikanda tunaijenga Nchi Hadi Barabara na madaraja yote yakamilike awamu hii na Sio nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom