Kuna chochote cha kutarajia kwenye mkutano wa kilele kati ya Marekani na Afrika?

Kuna chochote cha kutarajia kwenye mkutano wa kilele kati ya Marekani na Afrika?

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111414176310.jpg
Mkutano wa kilele kati ya Marekani na Afrika umepangwa kufanyika kuanzia tarehe 13 hadi 15 Desemba 2022, ikiwa ni moja ya juhudi za Marekani kutekeleza sera yake ya kurudisha uwepo wake barani Afrika, baada ya aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump kuiweka Afrika pembeni kwenye sera za Marekani.

Kinachotajwa na Marekani kuhusu mkutano huu, ni kuwa lengo lakini ni kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi, utawala bora, amani na usalama, sekta ya afya, usalama wa chakula, mwitikio wa msukosuko wa mabadiliko ya tabia nchi, na kuhimiza mahusiano ya diaspora ya Afrika.

Kwa kuangalia jina la mkutano huu, bila shaka tunaweza kuutaja kuwa ni mkutano mkubwa, ambao bila shaka kwa nchi za Afrika itakuwa ni moja ya fursa nyingine duniani za kutafuta njia za kujiendeleza, na kuinua uchumi. Lakini kwa upande wa Marekani mkutano huu utakuwa ni moja ya majukwaa muhimu ya kutafuta uungaji mkono katika kutekeleza sera yake ya mambo ya nje.

Hata hivyo kati ya mikutano yote kati ya Afrika na nchi za magharibi, huu ni mkutano ambao unaonekana hauna hamasa yoyote, na matarajio ya upande wa Afrika kuvuna chochote kwenye mkutano huo ni madogo sana. Hili linatokana na ukweli kwamba ufuatiliaji wa Marekani kwa sasa kwenye siasa za kimataifa umeelekezwa nchini Ukraine huko ndiko sera, fedha, na raslimali nyingine zinaelekezwa.

Kuna dalili kidogo sana kwa Marekani kubadilisha mwelekeo huo kwa sababu tu ya mkutano wa kilele kati yake na nchi za Afrika, zaidi kinachoweza kukadiriwa ni kuwa Marekani itatumia mkutano huo kama jukwaa la kuvutia uungaji mkono wa nchi za Afrika kwenye suala la Ukraine.

Uzoefu ulioonekana kwa muda wote wa Rais Joe Biden kuwepo madarakani, unaonesha kuwa kauli zinazotolewa na Marekani kuhusu kurudisha uwepo wake barani Afrika, zimekuwa ni maneno mazuri ya kuonesha urafiki wa Marekani kwa nchi za Afrika, tofauti na wakati wa Rais Trump aliyefikia hata kutumia lugha za matusi.

Lakini undani wa kisera unaonesha kuwa, kuna mabadiliko kidogo sana yenye manufaa kwa nchi za Afrika. Inawezekana pia kuwa mkutano huu itakuwa ni fursa nyingine ya kukutana na kupiga picha, na isiwe na fursa kubwa kiuchumi kwa maendeleo ya nchi za Afrika.

Changamoto kubwa iliyopo kwa Marekani kwa sasa, ni kwamba China imeweka kigezo cha juu sana kuhusu hii mikutano ya kilele. Mara nyingi viongozi wa Afrika wanapokwenda kwenye mikutano hii ya kilele, si kama wanatafuta fursa ya kupiga picha au kuonekana kwenye televisheni, kikubwa wanachotafuta ni fursa za maendeleo kwa nchi zao.

Mkutano wowote kati ya China na Afrika, uwe ni wa ngazi marais au ngazi ya mawaziri, fursa za kiuchumi kwa pande zote huwekwa mezani. Kwa hiyo tofauti na fursa za maana za kiuchumi kwa nchi za Afrika, mkutano huo utakuwa ni wa kukatisha tamaa.

Lugha iliyotumika safari hii kwenye kuutangaza mkutano huo imetaja fursa za kiuchumi, lakini pia imerudia mambo yaleyale yaliyokuwepo kwenye miaka ya nyuma. Utawala bora, usalama, sekta ya afya, usalama wa chakula, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, na kuhimiza mahusiano ya diaspora.

Bila shaka haya ni mambo ya thamani ambayo nchi nyingi za Afrika zinayathamini, lakini ukweli umeonesha kuwa uwekezaji wenye kuongeza uzalishaji, biashara na hata miundombinu, vimekuwa ni vichocheo vikubwa kwa maendeleo ya nchi za Afrika.
 
Mada nzuri mkuu ila kama kawaida haitapata wachangiaji wengi humu maana ipo mbali na ngono na wakata viuno, Africa ilitakiwa mikutano ya aina hii iwe ya two way traffic, yaani ni muhimu Africa nayo inakwenda kwenye meeting table na kitu mkononi cha ku offer kwa USA sio kila wakati kuwa na ma faili mengi ya kuombea msaada, nchi nyingi za kiafrika zimeshakua huru more than 50yrs ilitakiwa nasi tuwe tunajitegemea kwa budget zetu na kujilisha, Rushwa, greed kwa politicians wetu wamei let down Africa, binafsi naona Zambia 🇿🇲 wanachanua vema.
 
Tuna kiazi kimoja kinaona raha sana kusafiri safari zisizo na tija
Fanya kazi wewe, utapasuka kwa kijiba cha roho. Ulitaka ajifungie ndani ili iweje? Dunia ni kijiji, huwezi kuongoza nchi kwa kuchutama ndani kama mwanamwali. Acha akutane na wenzake kwa ajili ya kushare experience na kufungua fursa za uwekezaji.
 
View attachment 2445993
Mkutano wa kilele kati ya Marekani na Afrika umepangwa kufanyika kuanzia tarehe 13 hadi 15 Desemba 2022, ikiwa ni moja ya juhudi za Marekani kutekeleza sera yake ya kurudisha uwepo wake barani Afrika...

Kuwekwa kwenye Bus, kupigwa picha na kuja kuendelea kutunyonya
 
Fanya kazi wewe, utapasuka kwa kijiba cha roho. Ulitaka ajifungie ndani ili iweje? Dunia ni kijiji, huwezi kuongoza nchi kwa kuchutama ndani kama mwanamwali. Acha akutane na wenzake kwa ajili ya kushare experience na kufungua fursa za uwekezaji.
Nimeongelea kiazi, unataka kusemaje?
Kiazi kinaongoza nchi? Je hicho ndicho unachotaka kumaanisha?
Nime bold quote yako
 
Mada nzuri mkuu ila kama kawaida haitapata wachangiaji wengi humu maana ipo mbali na ngono na wakata viuno, Africa ilitakiwa mikutano ya aina hii iwe ya two way traffic, yaani ni muhimu Africa nayo inakwenda kwenye meeting table na kitu mkononi cha ku offer kwa USA sio kila wakati kuwa na ma faili mengi ya kuombea msaada, nchi nyingi za kiafrika zimeshakua huru more than 50yrs ilitakiwa nasi tuwe tunajitegemea kwa budget zetu na kujilisha, Rushwa, greed kwa politicians wetu wamei let down Africa, binafsi naona Zambia 🇿🇲 wanachanua vema.
Kwa hiyo umewabebea watu wote akili zao?Acha kuwaza ujingaujinga.
 
Zambia wanachanua vipi?

Sent from my MHA-L29 using JamiiForums mobile app
Democracy, freedom of expression imeongezeka,corruptions imeanza kudhibitiwa (elewa hapa kwetu police, mahakama ndio vinara wa rushwa),uchumi wao umeanza kusimama wima including local currency yao imeimarika na hii inasaidia ununuzi wa bidhaa kama petrol/diesel kuwa rahisi zaidi, chakula wanajitegemea hasa mahindi, miundo mbinu yao inaboreshwa vema,Kafue hadi kazungula border post ile barabara ni top class,T2 nayo inajengwa upya (hii imejengwa kwa wakati mmoja na T1 yetu, na sisi tunaitia viraka sio kuijenga upya),utalii wa ndani unakua mzuri na kuna kampeni nzuri ya kuutangaza
 
Kwa hiyo umewabebea watu wote akili zao?Acha kuwaza ujingaujinga.
Huu ni upumbavu mkubwa kutokea kwako, ungekua ni ujinga ungeelimika, hii ni mada na kila mtu anaijadili kwa hoja sio matusi, prove me wrong kwa hoja sio matusi, anyway never mind haya ni matokeo ya UPE na shule za kata, debate hoja iliyopo mbele yetu
 
Ni mada nzuri sana, lakini chuki dhidi ya madam president Samia Suluhu Hassan waliyonayo wachawi fulani humu imeshaanza kuharibu radha. Kama ingelikuwa mada hii inajadiliwa kwa kina, hasara na faida zake zinawekwa mezani.

Kwa mifano kamili isiyo na shaka, basi mada ingeliwafaa hata ndugu zetu wanaosoma lakini ndo hivyo tena, hapa tusubirie tu hoja za sijui kupanda basi, ushungi, kuwa na wajomba Oman, atatajwa JK hapa kama kawaida; Makamba akikosa kutajwa hapa leo basi itakuwa ameamka vizuri sana.

Kuna wakati ukiufikiria huo unaoitwa ugreat thinker, unaweza kujikuta unaisapoti mada ile iliyoanzishwa jana inayosema bora wazungu wazaane zaidi isije dunia ikabaki na wzjinga watupu.
 
Back
Top Bottom