Ni mada nzuri sana, lakini chuki dhidi ya madam president Samia Suluhu Hassan waliyonayo wachawi fulani humu imeshaanza kuharibu radha. Kama ingelikuwa mada hii inajadiliwa kwa kina, hasara na faida zake zinawekwa mezani, kwa mifano kamili isiyo na shaka, basi mada ingeliwafaa hata ndugu zetu wanaosoma.......lakini ndo hivyo tena, hapa tusubirie tu hoja za sijui kupanda basi, ushungi, kuwa na wajomba Oman, atatajwa JK hapa kama kawaida; Makamba akikosa kutajwa hapa leo basi itakuwa ameamka vizuri sana.
Kuna wakati ukiufikiria huo unaoitwa ugreat thinker, unaweza kujikuta unaisapoti mada ile iliyoanzishwa jana inayosema bora wazungu wazaane zaidi isije dunia ikabaki na wzjinga watupu.