Kuna chuki naanza kuiona inachomoza Tanzania

Weka vizuri mkuu;

Msingi wa hizi CHUKI na HASIRA ni utawala m'bovu!
 
Mkuu,
JPMAGUFULI atabaki kuwa ALAMA ya kiongozi bora aliye wahi kuwepo Tz.kisha Mz.MKAPA na babu NYERERE.
Huyu mama ni ALAMA ya kiongozi m'baya kuwepo Tz.ikifuatia awamu ya 4. Huyu mama hana mpango na hali wala hisia za watu/wananchi wake, badala yake yupo busy kupambania madaraka kwa kuwatumia waalimu kuwaandikisha watoto wetu kuwa wana ccm.
HAYA TULIYARUHUSU WENYEWE,ACHA TUVUNE TULICHO KIPANDA.
 
Mbona umechelewa sana kuiona?
 
Kwani huko Mbeya kumetokea nini ndugu..?

Je, una maana tukio la yule mwanamziki Zuchu kurushiwa mawe na chupa cha maji jukwaani ambaye badala apande aimbe nyimbo zake na kukata viuono, yeye akaanza kumpamba Chura Kiziwi au kuleta mambo mengine ya ki - CCM...?

Yes, kama ni huyo bila shaka alistahili kufanyiwa hivyo. Watu hawataki kuona wala kusikia mambo ya Chura Kiziwi aitwaye Samia Suluhu Hassan au u - CCM wowote ule...
 
Sijui unazungumzia kitu gani mahsusi mkuu 'cumbamalema', maanake umebaki kuzunguka zunguka tu bila kuwa wazi.

Ninakubaliana nawe kwa uwepo wa chuki inayojengeka kwa nguvu sana katika jamii wakati huu; kwa sababu viongozi waliopo, ambao ndio wangekuwa mstari wa mbele kuzuia hali hiyo; wao ndio wamekuwa watu wa kuirutubisha.

Kiongozi anapo kwambia "kifo ni kifo tu", wakati kifo husika kimetokea siyo kwa ajali au ugonjwa, bali kikihusishwa na vyombo vinavyo takiwa kuzuia kifo cha namna hiyo; kama huko siyo kujenga chuki ndani ya jamii, tukiiteje?

Ipo mifano mingi sasa hivi inayo onyesha chuki inatokana na matendo ya viongozi tulio nao madarakani sasa hivi.
 
Hii mbegu iliyopandwa na CCM na Serikali yake ikianza kuzaa matunda wahanga wakubwa watakuwa wanaCCM wenyewe.
Wao (CCM), wanaamini wanao polisi na mitutu ya bunduki; kama ulivyoona wakishangilia maandamano ya CHADEMA yalivyo zimwa.

Hawa hakuna chochote kinacho wastua sasa hivi.
Wakati huu wanajuwa kazi kubwa wanayotakiwa kuikamilisha ni kuwatumia polisi vilevile walivyofanya hapo chaguzi zitakapo wadia. Wao hawana shida tena na wananchi watafanya nini.
 
Jeuri yao inatokana na uhakika wa kushinda uchaguzi kwa mbinu za wizi kama alivyosema Nape na Ng'umbi, nk
 
Naomba tufike huko maana tumechelewa sana
Hapana.
Mimi ninatofautiana nawe katika hili bila ya kusita kabisa.

Hatuhitaji kujengeana chuki baina yetu sisi kwa sisi kwa sababu tu ya viongozi wabovu tulio nao. Ni jukumu letu kuwashughulikia hawa hawa viongozi.

Njia zipo nyingi sana za kuwakomesha hawa.
 
Lakini walipopigwa mabomu na virungu siku ya Vijana Duniani haikuwa chuki.
 
Wewe ndio unapanda mbegu za chuki, na mmetumwa kuharibu
 
Chuki zilianza kitambo sana! Hiki kinachofanyika leo ni mkolezo tu!
Na chanzo ni ccm kulewa madaraka.
 
Wewe ndio unapanda mbegu za chuki, na mmetumwa kuharibu
Kwa hiyo wewe unaona watu wanaupendo na vyombo vya dora, na viongozi, au wanachama wa Chadema wanaupendo na wa CCM au wasani wanaoshabikia CCM na watu wa vya vya upinzani kuna upendo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…