Kuna chuki naanza kuiona inachomoza Tanzania

Ni Uzi wa kujaribu kuomba Nia ovu iliyopo moyoni mwa haters iwe kweli.....yaani nchi iharibike kama wanavyotaka wasiompenda mama Samia.

Suala la utekaji nchi hii halijaanza Leo, lilikuwepo miaka mingi tu katika tawala za nyuma. Kilele kilikuwa pale ilipofikia Hadi mtu kupigwa risasi nyiiingi mchana kweupeee. Hakukuwa na maandamano Wala nyimbo za kumkashifu kiongozi wa kipindi hicho. Sikusikia au niseme sikubahatika kuisikia kauli ya kiongozi mkuu akiagiza vyombo vifanye uchunguzi au hata kukemea tu.

Sasa hivi inaonekana yanaendelea mambo hayo yapo, ajabu kelele zimechukua mkondo tofauti.......mama anatukanwa na propaganda ya kuagiza kuteka inasambazwa kwa kasi ya mafuta ya petrol. Kama inavyofahamika, wingi wa wajinga na wapumbavu weeengi katika taifa hili basi wapo wanayoyashika.

Ukweli Kuna mawimbi makubwa kweli kweli anaandaliwa huyu mama...yampasa kusimama imara. Issue hapa Wala sio utekaji (ingawa Kuna mauaji mbalimbali yanaendelea kwa raia n.k); Bali hoja iliyopo ni kuhakikisha anaharibikiwa. Uanamke wake, dini yake na uzanzibari wake ndiyo vyanzo vikuu....zingine hizi ni 'tutoke vipi' zao tu.
 
Magufuli hajawai kumtetea mnyonge au maskini yeyote bali alitumia wanyonge kujijenga kisiasa. Kama ni kutetea wanyonge alipaswa kuwafidia wale wananchi wa Kimara- Kibaha aliowavunjia nyumba kupisha barabara.

Angekuwa mtetezi wa wanyonge asingetumia mabilioni kujenga Chato kijijini kwao miundombinu inayostahili kuwa makao makuu ya Mkoa wa Geita. Huku watoto wa Watanzania wanasoma kwenye kwenye miti na wengine hawana madawati. Au kununua madreamliner wakati 80% ya Watanzania hawapati maji safi.

Magufuli ilikuwa ni LAANA, na Mungu ametuepushia, tujenge Tanzania yetu nzuri isiyo na ubaguzi wa kiitikadi, kikabila na kikanda

Ni upumnavu kukubali kuitwa MNYONGE. Mungu alituumba binadamu na akatuwezesha kwa kutupatia ubongo. Ukitumia ubongo wako vizuri unaweza ukajinasua kimaisha.

Magufuli alikuwa añatamba kuwa ana uwezo wankumfanya tajiri aishi ka shetani. Kwangu hii haikuwa sawa. Alipaswa aseme ana uwezo wa kumfanya maskini aishi kama tajiri ndiyo ange make sense.

Muacheni Samia atuongezee matajiri na wafanyabiashara wakubwa. Hawa wakiongezeka ndiyo watawaajiri maskini na maskini wanaweza kutoka kimaisha kupitia matajiri. Kamwe umaskini na unyonge siyo kitu cha kujivunia
 
Chura kiziwi anasema kuteka na kutekwa ni drama
Vile vile amesema kuwa kifo ni kifo tu!😳

Ina maana kuwa kwake yeye kifo Cha Medy Kibao hakimuumi kabisa, ndiyo maana Hadi leo hajamwajibisha kiongozi yeyote, kuhusiana na mkasa huo, vile vile hajaunda Tume huru ya kuchunguza kifo hicho!

Vile vile hata waliotekwa, kina Soka na wenzake, hafanyi juhudi zozote zile za kuwarejesha uraiani, utadhani waliopotea si binadamu, Bali ni sisimizi!😭
 

Na hii yote imesababishwa na kupotea kwa watu na Serikali kushindwa kuwapa wananchi majibu ya kujitosheleza wamekuwa na hasira sana na kujiona wao kama ni kundi la watu wa kupuuzwa📌🔨
 

Ni kwamba tu akili huna, Mara kibao kwenye dini zote kuna wakati chuki za watu na ugomvi ulileta ukombozi, ni kwamba tu umejifungia kwenye mtazamo mmoja, listen you lazy thinker:

“Kuna wakati ugomvi na chuki unamtoa mtu kwenye ajira moja ngumu na kuteseka kwa mda na yeye kupata kazi nyingine better, pasingekuwa na huo ugomvi then asingekuwa na ujasiri wa kutoka, wakati mwingine Mungu utumia haya mazingira Kubariki watu”

Unaelewa how far Ccm can fight and damage people kwa Sababu za ku remain kwenye power ? Unajua wakati wanafanya hayo watu wanaumia? Unajua huyo Mungu unayemwomba aondoe chuki a naona watu wanaonewa?

Ni nini unafikiri ni matokea ya uonevu wa mtu kwa mda mrefu asiyeweza kujitetea? Si chuki? Kwa nini usilalamikia uonevu unalalamikia chuki? Wakati chuki ni matokeo ya uonevu?
 
Huwezi kusimama na kusema mitano tena kwa mama watu wamelipa kiingilio kisa wewe unapewa rushwa umsifie huyo mama ako, haikuwa sehemu sahihi kwa kampeni hapo.
 
Na hii yote imesababishwa na kupotea kwa watu na Serikali kushindwa kuwapa wananchi majibu ya kujitosheleza wamekuwa na hasira sana na kujiona wao kama ni kundi la watu wa kupuuzwa📌🔨
Mbona familia za viongozi na wanaccm hawapotei?
 
Kama chuki hiyo inakuwa na kustawi dhidi ya CCM na serkali yake basi itakuwa kheri sana kwa watanzania manake kweli kama kuna mzigo watanzania wanabeba saa hii ni CCM.
 
EEEeeeeenHeEEEEeeeeeEE!
Sasa wewe hapa katika maneno yooote uliyo andika kuna kipi ambacho unaweza kuonyesha kwamba umetumia akili sawasawa!

EEEeeeenHEEEee1
Hizi bangi nyingine muwe mnakaa nazo wenyewe huko huko bila ya kuzileta humu jukwaani. JF sasa kimekuwa kijiwe cha kila aina ya vilaza na wavuta bangi kama wewe.
 
Na hii yote imesababishwa na kupotea kwa watu na Serikali kushindwa kuwapa wananchi majibu ya kujitosheleza wamekuwa na hasira sana na kujiona wao kama ni kundi la watu wa kupuuzwa

Tumuombe Mungu tusifike huko kwani tunakoelekea ni kubaya
wapi?
 
Chuki zimezalishwa na Tanganyika kukosa Rais wao, katiba Yao, Baraza la mawaziri lao.
Huo ndio ukweli na chuki hii,inakuwa Kila siku.
Mwambieni bibi ukweli
 
A
Acha iendelee kunyesha tuone panapovuja
 
Na hii yote imesababishwa na kupotea kwa watu na Serikali kushindwa kuwapa wananchi majibu ya kujitosheleza wamekuwa na hasira sana na kujiona wao kama ni kundi la watu wa kupuuzwa📌🔨
Huwa nakukubali sana
 
Tulisha ambiwa kuteka na kutekwa ni Drama na Kifo ni kifo tu.
Na bado tukaambiwa Chura kiziwi hasikilizi na bado akasisitiza kuna mbwa ambao tunaonea wivu maendeleo flani flani ambayo hatuyajui.

Kizazi chetu ni cha hovyo tu na maza anakipeleka anavotaka kwasababu anajua hizo chuki zetu hatuna cha kumfanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…