DOKEZO Kuna chuo Kikuu cha Umma hivi karibuni kimeajiri walimu watano bila Ushindani, kipo Morogoro

DOKEZO Kuna chuo Kikuu cha Umma hivi karibuni kimeajiri walimu watano bila Ushindani, kipo Morogoro

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mwanamwaiche

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2022
Posts
665
Reaction score
968
Ni masikitiko makubwa sana vijana wanapambana kupata gpa ila kuna wahuni wachache wanaamua wa kumuajiri wamtakaye, kwanza Mkuu wa Idara mmoja aliwakusanya hao watano Kwa nafasi Tano, wakapewa maswali na majibu ya oral, na wakafanya presentation za slides akawarekebisha kisha wakaingia interview wakapita.

Inaleta aibu na hasira, waliwachomoa applications za vijana wenye gpa kali wakaandaq wanaowataka wao nafsi Tano na wakaandaq hao hao watano na wakawajiri hao watano.

Wakati wa Magufuli kila nafasi kulikuwa na mtu wa utumishi anaelinda usawa, haki na demokrasia ya kumpata mshindi, alikuwepo msimamizi wa utumishi Kwa kila nafasi ya ajira inayoshindaniwa.

Serikali chunguzeni hizi ajira, na shortlist ya mchujo wa kwenda Oral usimamiwa Kwa haki na ikiwezekana usimamiwe na watu wa utumishi.

Hii ya kuwaachia wahuni wa idara, faculty, school, college kufanya fitina inaangamiza taifa.

Mchujo nafasi moja walau Oral wasipungua washindani watano (5) ikiwezekana hadi 10, unawaita watu 90 na oral unachukuwa watu watatu (3) ni uhuni mbaya sana.

Naomba sana utumishi ajira za walimu wa vyuou vikuu hata kama interview itafanyika mazingira ya vyuo husika hakikisha zoezi hili mlisimamie nyie hao wahuni wa vyuo husika wawe watazamaji tu. Kikubwa vigezo vya kumpata mshindi viwekwe wazi.

Iwe marufuku wakuu wa idara husika, faculty husika, skuli husika na college husika kushiriki kumpata mshindi.

Utumishi fuatilieni hili swala ni hatari sana sana. Huwezi kuwapitisha watu kwenye nafasi bila kuwashindanisha na wengine wenye sifa tena wenye sifa zaidi hamuwapi nafasi.

Narudia chuo kikuu hicho Cha Umma kipo Morogoro.

Wakuu wa vyuo husika vya Morogoro mjichunguze na fuatilieni ajira za juzi mwezi wa Tisa michakato ya kuanzia August chunguzeni kwenye kila skuli, idara, na Ndaki mtajua ukweli na hio Ndaki iliyofanya/zilizofanya uhuni huu mtengue hizo ajira.

Nawaaga huku nikipeperuka kiuwenda wazimu.

Mpiga mbiu haogopi bali anaishi uzalendo zaidi.

Taifa ni letu sote.
 
SUA au Mzumbe.sema unaficha nn na hao 5 madem wako wangap?i
 
Back
Top Bottom