DOKEZO Kuna Course imeanzishwa mwaka 2025, ya Higher Diploma in Mental Health Nursing, lakini hii course haijulikani kama ipo chini ya NACTE au Wizara

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna kozi ya Higher Diploma in Mental Health Nursing iliyoanzishwa mwaka 2025, lakini hadi sasa haijafahamika wazi kama iko chini ya usimamizi wa NACTE au Wizara husika.

Tumejaribu kupata ufafanuzi kutoka kwa wahadhiri wa kozi hiyo, lakini nao hawajatoa majibu ya uhakika kuhusu hatma na utambulisho wa programu hiyo. Pia tuliomba kukutana na Mkurugenzi wa Mafunzo kwa kuandika barua kupitia Mkuu wa Chuo cha DIHAS-Dodoma, lakini hadi sasa hatujapata majibu yoyote na barua yetu haijapatiwa ufumbuzi.

Kwa taarifa tulizonazo, Mkurugenzi wa Mafunzo aliwahi kufika chuoni hapo na kuomba kukutana na wanafunzi wanaosoma kozi hiyo, lakini aliambiwa kuwa wanafunzi walikuwa na majukumu mengi na hawakuweza kukutana naye, jambo ambalo si sahihi kwa mujibu wa taarifa tulizonazo.

Tunaiomba serikali na mamlaka husika kutoa ufafanuzi kuhusu hadhi ya kozi hii, ikiwa ni pamoja na usajili wake, utambuzi wake na mwelekeo wa wahitimu wake baada ya kumaliza masomo.

Aidha, tunaomba kuanzishwa kwa ngazi ya Level 8 ya Mental Health Nursing kabla ya mwaka 2027, kwa kuwa kwa sasa kuna ngazi ya Level 7 pekee.

Tunaomba wahusika walifanyie kazi suala hili kwa haraka, kwani wanafunzi wanaendelea kusoma na kulipia gharama za masomo bila kuwa na uhakika wa hatma ya kozi wanayoisomea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…