Kuna dada katumiwa kadi ya mwaliko wa harusi na mwanaume aliekuwa na malengo nae/future almanusra ajitie kitanzi

Kuna dada katumiwa kadi ya mwaliko wa harusi na mwanaume aliekuwa na malengo nae/future almanusra ajitie kitanzi

Sahv inabidi afunge ndoa kimya kimya askilizie kwanza kama miaka miwili akiona hali ni shwari ndo aibuke kutangaza
Na kwann atangaze?
akifany hivyo lazima kimlambe tena
 
Dc lazima atataka kuja kum-prove wrong mama zuri, afu anaweza rudia kosa la kwanza la kutafuta pisi kali ya kumringishia mama zuri
akianza mambo ya revenge atazingua kinoma
 
Hapo utakuta alikuwa ana cheat anadhani jamaa ajui kumbe alikuwa ana mchora tu miaka yote minne waliokuwa kwenye mahusiano

Siku hiz style yao wanakuwa na wanaume watatu watatu anakula huku na huku kwa kuzani haujui kumbe unajua na umeshachukua namba mpaka za hao madanga wake unamlia timing tu.. umpige tukio

Ukigundua ana cheat usimuache kula mzigo kama kawaida ila wakati wa kuoa unatafuta mwanamke bikra tu.. wasikisumbue kichwa
Wewe ndio huyo bwana nini maana umeelezq kinagaubaga sababu ya dada kuachwa. Ila ilikuwa lazima kumtumia kadi?
 
Wewe ndio huyo bwana nini maana umeelezq kinagaubaga sababu ya dada kuachwa. Ila ilikuwa lazima kumtumia kadi?
Ndiyo,kulipiza maumivu,mdogo wangu alikua na Dem,huyo Dem wakienda mitaa ya kwao mabibo anamtambulisha kama kaka yake,dogo alupojipata akaoa Dem mwingine
Dem aliduwaa
 
Wewe ndio huyo bwana nini maana umeelezq kinagaubaga sababu ya dada kuachwa. Ila ilikuwa lazima kumtumia kadi?
Sasa si ni michezo yao ya kisasa hiyo na inajulikana hapa natoa code ili wanaume tushtuke tusikae na mtu ambaye siyo
 
Jamaa kamfinyia huyu dada vitendo vya kilusifa kamtumia kadi ya mwaliko wa harusi kwamba anaoa mwanamke mwingine.


dada kawahiwa na marafiki zake kidogo ajitie kitanzi.
haikua sahihi hata kidogo kwa huyo muungwana kufanya hivyo gentleman,

hata hivyo,
Laumu ya kiroho na kisasi cha kimwili alichonacho alietumiwa kadi,
dhidi ya alie tuma kadi, hakitamuacha salama kwenye ndoa yake šŸ’
 
Hiyo inauma sana ndugu omba isikukute .
Nikamkumbuka mchumba wa advance na viapo vyetu vya kukatana na wembe ,katu nikajiapiza huyu ndiye mke .

Viunga vya jiji wakati wa likizo ni mimi na yeye ,si tution wala kwenye makasino ambako mimi sikuambatana naye .

Sikuwa na ugeni kwao wala yeye hakuwa na ugeni kwa wanangu wa keko ,ila sasa mchumba baba yake balozi nchi fulani na muda huo mrembo anatakiwa kwenda huko kusoma .

Ningekataa katu nisingeweza mimi ila mawazo yakanituma au nijisalimishe nyumbani walau niombe na mimi niende kusoma nchi hiyo ili soulmate wangu asipeperuke ila moyo wa kiume ukagoma kuwa kama ni wako atarudi nigga ,vunga usijisalimishe kwa wazee kama ulishaamua mbwai basi iache iwe mbwai .

Chap kwa haraka ,visiting na mitoko mimi na mchuchu ni nyingi si unajua tena anaondoka muda wowote ? Nakutana na brother big ,LEMUTUZ(R.I.P) nampa mkanda mzima wa mchuchu wangu ,brother ananipa moyo na kusema nikaze kama wangu atageuka tu .

Sasa kawaida maniga uwa hatusalitiani .mrembo baada ya majuma kadhaa kakwea pipa mpaka huko ,mwamba nikaendelea kusubiri ipo siku atarudi nimweke ndani wa ubani .

Zawadi na barua sio vitu vya kuuliza kwa miezi ya mwanzo ila kadri muda unavyotembea mrembo mawasiliano yanakuwa hafifu kweli kweli .

Baada ya miaka miwili napata nafasi ya kuruka kwenda kusoma nje huko ila nchi tofauti ,mrembo bado mawasiliano ni ngumu sana .
Nikiomba nikamtembelee sababu ni nyingi naona basi wacha nitulie kidogo .

Mzee wake si mgeni na mimi ananijua sana na wazee wangu ,naamua wacha nimcheki mzee dingi nimchane simsomi mwanaye ila ndiyo vile ujasiri sina kila nikimpata naishia kuomba hela ya matumizi maana mgogoro wangu na wazee wangu anaujua ila kumbe mimi shida sio mshiko ila shida ni binti yake kumuelezq nitaanzaje mimi muhuni wa keko niliyeletwa nje na kudra za marafiki wa mzee ?

Akiniuliza habari za kuwasiliana na mwanaye nasema tunawasiliana ila kusema ananizingua naogopa .

Namaliza mitikasi yangu narudi zangu bongo ,naendelea na kisomo kingine ila mchuchu no zawadi ,no barua no kila kitu kinachohusu mawasiliano .

Finally ajirani ndani ya miezi miwili ,nakumbuka kama mazuri nikiwa UDSM _COET huko nilienda kumdrop mwanangu flani by then ,ile ameshuka napigiwa simu na mwanangu wa damu (R.I.P) Salimu kidevu anasema oya kuna sister mmoja kaja masikani hapa anadhani bado unaishi huku kaleta bahasha ila kasema tukupe wewe .

Nakanyaga wese mpaka keko kwa mwanangu mwenyewe ,nafungua bahasha nakuta zawadi kedekede ila katika mzigo ule kunayo kadi ya harusi na inafanyika hapa hapa bongo ila mchuchu wangu anaolewa na Gabachori fulani hivi posta back in days ila ndiyo vile alishasepa anaishi kwao huko .

Jasho ni jingi mwanenu ,na vile nilikuwa bado mgeni wa gambe ,nadrive na mwanangu mwenyewe mpaka King palace ,navuta muwine mkubwa nakunywa ila silewi ,roho inauma kichizi ,natamani kulia ila naona aibu ,wanangu watanionaje .

Safari za maliwato haziishi naenda huko nafuta tumachozi narudi nadunda kama sio mimi ,wanangu wanaulizq uko sawa nasema mapenzi hayawezi kunidrive wanangu relax niko gado mwanenu 😜

Ila moyo unawaka moto ,ziliponikaa pombe haswa machozi yakaamua yotoke tu haikuwa na namna nikalia sana ,wanangu wakacheka sana ila baadye ikabidi wanibembeleze msela wao .

Natamani nimpigie bi mkubwa nimshitakie labda aongee na wazazi wake yaishe asiniache ila sasa nitaanzia wapi bi mdashi mwenyewe hatupo sawa ?

Hivyo mwanenu nikaomba ruhusa ya bila malipo nikakimbilia huko Sumbawanga kirando ,kulikuwa na mwanangu fulani alienda kulinda mpaka wa bongo na Congo ila ni kama mdogo wangu wa damu ikabidi nikapoze moyo huko kwa kula migebuka na sangara na ugali wa muhogo baada ya kuona kama nitakufa muda wowote .

Mapenzi ni hatari sana ikiwa utapenda kweli .
MHESHIMIWA R najua utapita hapa na utakumbuka mbali ila jua mbali na yote ila mimi msela nilikupenda sana binti ila ndiyo vile ukaamua kulipenda hilo dude .
Much respect sana aisee
Hili ā˜ļøandiko pia alisome Mzee mwenzangu Dr am 4 real PhD.
 
Back
Top Bottom