Uchaguzi 2020 Kuna dalili CCM itawakata wengi walioongoza na hawataweza kwenda upinzani

Uchaguzi 2020 Kuna dalili CCM itawakata wengi walioongoza na hawataweza kwenda upinzani

Sio dawa bado watakuwa na muda.
Siku wakikatwa siku hiyo wanateuliwa na upinzani wanaenda kuchukua form NEC katika muda ule ule ambao na hao wateule wa CCM watakakuwa wanachukuwa form hizo.
Hili linawezekana kabisa!
 
Inawezekana kabisa majina ya wateule wa CCM yakawa ya mwisho kabisa kufikishwa Tume ya Uchaguzi ili kuepusha wale ambao hawatakiwi wakishakata wasihamie upinzani.

Kuna nijadala inaendelea kuwa hao watakaokosa na huku wameongoza upinzani wameshajiwekea mazingira mazuri ya kuhamia upinzani na wanasubiri tu CCM itoe majina.

Ndugu yangu anayefanya kazi Kyela amenitonya aliyeongoza kwa Mwakyembe anasubiri tu CCM imrudishe Mwakyembe yeye ahamia CHADEMA.

Tayari ameshaandaliwa mpango mzima na Sugu na ameshaongea na mteule wa CHADEMA Kyela. Wengi watashangazwa!

Kuliona hilo tayari CCM inachukua tahadhari na inacheoenda kukifanya ni kutoa majina ya wateule wake siku mbili kabla ya Tume ya Uchaguzi kufunga mapokezi ya Fomu hizo ili kuepusha watu hao kuhamia upande wa pili.

Uwezekano ni mkubwa CCM kutoa majina yake tarehe 24 au Tar 25 ili kujihami na wahamaji. Stay tuned!
Mwaka huu ccm imetaitiwa kila upande...imabanwa mbavu zote haina pa kupumulia haina pa kutokea
 
Hili ni muhimu kutungiwa sheria kuepeku huku kuviziana. Sheria iweke wazi ukishaamua kuomba ridhaa ya kupitishwa kugombea chama flani katika uchaguzi "xyxy" wa mwaka x, hurusiwi tena mwaka huo kwenda kuomba ridhaa hiyo kwa chama kingine.
 
Back
Top Bottom