Kuna dalili yoyote tajiri namba moja akapewa wizara huko Marekani?

Kwa mtazamo wangu tajiri alibeti, kuingia na kujitangawa wazi kwamba anasimama na Trump ilikua ni mbinu ya kibiashara apate faida kubwa sana ama hasara.
Kitendo cha Trump kushinda kimemfanya tajiri kutengeneza faida maradufu ndani ya siku 2/3, hisa za makampuni yake zimenunuliwa na zimepanda maradufu.
Kwasasa sioni kama tajiri atakubali ofa ya teuzi in USA.
Matajiri wa USA sio sawa na akina Kishimba au Msukuma. Siamini kama ana mpango wa kuacha biashara afanye siasa.
 
Elon musk asije kuwa kama Rostam Aziz ambaye, baada ya kuwa mbunge wa Igunga, aliona nafasi ile ni miyeyusho kwake (nafasi ya ubunge haimlipi) ukichanganya na kelelle za akina nape zisizokuwa na mashiko kwake. Rostam akaamua kubwaga manyanga ili ajikite na biashara zake.

Kwa hiyo, Elon musk, Kwa Sasa, inawezekana akatamani kupewa cheo na swahiba wake Trump, lakini itafika kipindi ataona cheo alichopewa ni miyeyusho kwake, ataona ni Bora aachie ngazi ili ajikite na biashara zake tu.
 
Hatachukua nafasi yoyote ila agenda zake zitakuwa zinapitishwa tu fasta..

mfano Tanzania ilikataa starlink mda siyo mrefu starlink itaanza kufanya kazi Tanzania...

Nchi ambazo zitakataa kufanya nae biashara zitapigwa vikwazo na serikal ya trump..

Hutaskia kuna nchi imeifungia twitter (x)
 
Kutokana na tajiri namba moja duniani kuwa kwenye timu ya kampeni, na hatimaye kushinda; Je kuna dalili yoyote ya yeye kupewa wizara? Na kama atapewa, itakuwa ni wizara gani?

Ingawa wapo wanao hisi kwamba, kutokana na yeye kushiriki kwenye siasa inawezekana anapalilia njia ya kuwania nafasi ya urais kipindi kijacho.

Wachambuzi, mnalisemeaje hili?​
Naona umewaza kwa akili fupi fupi za kitanzania kabisa.

Chadema walimteua mama Lowassa kuwa mbunge viti maalumu akakataa.

Magufuli alimteua Salma kikwete
Samia kamteua Ridhiwan uwaziri
Na wengineo.

Haiwezekani na haitakaa itokee Elon kuwq Waziri au Secretary of states kama wao wanavyoita.

Musk ni muumini wa sera za Republican, hataki utoaji mimba na ubadilishaji jinsia. Mbaya zaidi sio muumini wa wanawake katika kutawala ndio maana hana mke japo amezaliwa na mwanamke.
 
U
Kutokana na tajiri namba moja duniani kuwa kwenye timu ya kampeni, na hatimaye kushinda; Je kuna dalili yoyote ya yeye kupewa wizara? Na kama atapewa, itakuwa ni wizara gani?

Ingawa wapo wanao hisi kwamba, kutokana na yeye kushiriki kwenye siasa inawezekana anapalilia njia ya kuwania nafasi ya urais kipindi kijacho.

Wachambuzi, mnalisemeaje hili?​
Ulinzi ama elimu na teknolojia.
 
Trump alisema akiingia madarakani ataunda baraza la kudhibiti/kukagua matumizi ya serikali ambapo mmoja ya wajumbe atakua Elon Musk, na jamaa alisema yupo tayari kuwepo kwenye ilo baraza.
 
Kwa mtazamo wangu tajiri alibeti, kuingia na kujitangawa wazi kwamba anasimama na Trump ilikua ni mbinu ya kibiashara apate faida kubwa sana ama hasara.
Kitendo cha Trump kushinda kimemfanya tajiri kutengeneza faida maradufu ndani ya siku 2/3, hisa za makampuni yake zimenunuliwa na zimepanda maradufu.
Kwasasa sioni kama tajiri atakubali ofa ya teuzi in USA.
Hakika mkuu..Mtu tajiri duniani apate teuzi ya kazi gani? Kama pesa anazo nyingi
 
Haiwezekani na haitakaa itokee Elon kuwq Waziri au Secretary of states kama wao wanavyoita.
Kwa nini isitokee?, na kuna tetesi ameshiriki 'call' kutoka Ukraine kuja kwa mteule.
 
Kutokana na tajiri namba moja duniani kuwa kwenye timu ya kampeni, na hatimaye kushinda; Je kuna dalili yoyote ya yeye kupewa wizara? Na kama atapewa, itakuwa ni wizara gani?

Ingawa wapo wanao hisi kwamba, kutokana na yeye kushiriki kwenye siasa inawezekana anapalilia njia ya kuwania nafasi ya urais kipindi kijacho.

Wachambuzi, mnalisemeaje hili?​
Unataka kumrudisha mtu kwenye umaskin ..kuajiriwa wakati ŵw unaweza kujiajiri ndo laana yenyewe hiyo
 
Sijajua itakuwaje ingawa kuna majadiliano yanaendelea, kwa sababu kwake hela sio tatizo; ngoja tusubiri list ya baraza
 
Back
Top Bottom