Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 8,323
- 18,051
Huwezi kuwa na standard ya cost estimate ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mafuta.Mleta uzi anasema nchi za Africa zitumie hela za ndani kukamilisha mradi?! namuuliza, tutumie hela za ndani kujenga bomba litakalosafirisha crude oil nje ya east africa? Si upumbafu huo kaka. Na tukitaka kujenga refinery, kwanza hiyo hela tutatoa kwenye benki zipi? Unadhani mabeberu watatuchekea kwa kukata mrija wao? Yalikuwa maswali kwa mleta uzi. The rest kuhusu Niger delta, Angola, Libya nayajua vema sana.
Ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mafuta unategemea na aina ya matumizi/uhitaji. Je unatengeneza plant ya kuchakata mafuta ili uuze au unatengeneza plant kwajiri ya mafuta utumie ndani ili kupunguza gharama kwa raia wako.
Kwa mfano kwa sisi hapa Tanzania au East Africa tunaweza kuanza na kuchakata mafuta kwaajiri ya kubinya gharama za ndani ili tuweze kuwa na effective prices eneo la nishati badala ya kucheza na bei za hawa mbwa wa magharibi.
Gharama za ujenzi wa plant hiyo hazitaweza kuwa kubwa kutushinda. We worth a mabilioni of dollars plus kuna Urusi na China tunaweza shirikiana nao kuweza kufanya hayo mabadiliko.
Kwann tunakuwa na akili za kinyumbu kuamini kila jambo ni hadi mataifa ya magharibi yatupe Go ahead?
Wao wanaweza pinga mradi sisi tukasema NO tutafanya huu mradi tunashukuru kwa maoni yenu ila tutafanya huu mradi na tutachukua tahadhari juu ya madhara ya mradi eneo la mazingira.
Halafu niwakumbushe tena, umasikini wa sisi watanzania sio matokeo ya kutaka MUNGU au sisi tumekuwa conditioned kuwa masikini. Shida ni CCM na syndicate yake na regime.
Umeona hata magufuri walimchukia sababu alienda against policy yao ya WIZI WA MALI ZA UMA. Ukitaka CCM na nusu ya hili taifa kikuchukie wewe weka sheria na taratibu za kuwabana watu waliopo serikalini na maofisi ya serikali wasiibe hapo utajenga uadui usio na mwisho. Wao wanataka kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake eneo lake.
Tuwatoe CCM, ili tupunguze influence ya watu wanaotetea mifumo ya uharibifu. Tunazidi kuchelewa maendeleo.