granitized
JF-Expert Member
- Jul 5, 2016
- 4,869
- 11,356
maendeleo anayafanya kwa hela za watanganyika, ijulikane hvo.
Kijana?Sure,
Dr. Mwinyi anafaa kuongezewa muda wa urais kwasababu bado ni kijana mchapakazi na mwenye uwezo mkubwa sana wa kiungozi.
Hakuna mzanzibari anaeweza kupinga jambo hilo muhimu sana na lenye maslahi kwa wazanzibari wote.
naunga mkono 100 kwa 100 Dr.Mwinyi kuongezewa muda wa uongozi wa SMZ
jikite kwenye hoja mezani gentleman bila kumbwelambwela mambo yasiyohuska na hoja 🐒Kijana?
Hebu tafuta 'age-range' ya ujana.
Ongea hivyo ikiwa hakuna muungano na Zanzibar ni nchi inayojitegemea yenyewe bila muungano, elewa watanganyika wanapaswa kuhoji, na wazanzibar vile vile wanapaswa kufanya hivyo.Katiba ni ya Zanzibar, watanganyika wanaingiaje kwenye maswala ya uchaguzi wa Zanzibar?
Sasa mtu hata hujui ujana unaanzia miaka mingapi na unaishia miaka mingapi.......jikite kwenye hoja mezani gentleman bila kumbwelambwela mambo yasiyohuska na hoja 🐒
hiyo sio muhimu sana gentleman,Sasa mtu hata hujui ujana unaanzia miaka mingapi na unaishia miaka mingapi.......
Kwahiyo rekebisha andiko lako kwanza.
Mwinyi anafanya kazi ya kutukuka kabisa.Aongezewe mudaWameanza kutest mitambo.
==============
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamependekeza kufanyika kwa marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ili kumpa nafasi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuendelea kuiongoza Zanzibar zaidi ya ukomo wa mihula miwili ya miaka 10.
Mapendekezo hayo yalitolewa leo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi huko Chukwani, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, wakati wajumbe walipokuwa wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Ikulu kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Wajumbe hao wamesema Dk. Mwinyi ameonyesha uongozi wenye maono, ubunifu na matokeo makubwa ya maendeleo katika sekta mbalimbali, jambo ambalo limeifanya Zanzibar kupiga hatua kubwa kiuchumi na kijamii.
Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni, Hussein Ibrahim Makungu, amesema Zanzibar imepata kiongozi mwenye uwezo mkubwa wa kusimamia maendeleo na kuwaletea wananchi matumaini mapya.
“Rais Dk. Hussein Mwinyi amefanya kazi kubwa sana. Miradi ya maendeleo inaonekana wazi na wananchi wanaendelea kunufaika. Ni maoni yangu kuwa Katiba iangaliwe upya ili apate nafasi ya kuendelea kulitumikia taifa hili,” amesema Makungu.
Mwakilishi wa nafasi ya rais, Taufiq Salum Turky, amesema Dk. Mwinyi ni kiongozi mwenye maadili, msikivu na mwenye dhamira ya dhati ya kuwaletea wananchi maendeleo.
“Tumepata Rais makini, mwenye huruma na anayesisitiza umoja, mshikamano na kuondoa mifarakano ya kisiasa. Huu ni uongozi unaostahili kuungwa mkono,” amesema Turky.
Naye, Mwakilishi Tabia Maulid Mwita amesema Rais Mwinyi ameleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii kupitia sera na mipango yake ya maendeleo.
View attachment 3587158