only83
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 5,343
- 2,527
Soka letu limejaa wadau makanjanja kama hawa. Mimi ni mshabiki wa Yanga, nilikubali kuwa Mbao FC walitufunga kihalali na walikuwa na nidhamu kubwa ya mchezo siku ile. Tatizo la utawala wa Simba ni kutaka huruma za mashabiki wao kila mara. Aveva na uongozi wake wanatambua kuwa, kama wasipochukua ubingwa wa VPL mwaka huu kibarua chao kitakuwa shakani, wangetamani wachukue FA ili wajifiche kwenye kichaka hiki. Nawashauri Simba, wawabane watawala wao zaidi kuliko kulishwa maneno ya kuwa wanaonewa kila siku. Hivi mechi ikichezewa kwenye 'uwanja huru' kuna shida gani? Hivi ni SIMBA na YANGA ndio wana haki ya kuchezea kila mechi TAIFA au UHURU? Kwanini usichezwe hata KAITABA au NYAMAGANA, au kwingine kokote? Tuwe fair, hakuna mahali palipoandikwa kuwa ni SIMBA na YANGA ndio wana haki ya kuchukua ubingwa wa FA au VPL.