Kuna faida gani ya umaarufu wa msanii kama hawezi hata kujitibia hadi achangiwe na wananchi?

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Hawa wasanii Wa bongo wanashida gani? Je; Wanatanguliza maisha ya anasa au ni nini?
Umaarufu wao unafaida gani kama pesa ya kujitibia tu hawana?

Kuna watu wanaleta hoja dhaifu kwamba makampuni wanayo ya promote eti yawe yanawajibika kuwatibia;
Hivi Hamtambui kwamba kuna mikataba, tena baadhi ya wasanii hulipwa pesa zote, lakini huzitapanya kwa anasa?
Umaarufu wao unawasaidia nini kama hawawezi kujitibia?
hilo pia linaenda saambamba na baadhi ya viongozi waliowahi kutumikia nchi hii
 


Nilifikiri kuchangia Matibabu ya mtu ni hiari sikujua kwamba unalazimishwa!
 
Tatizo lao hela wanapata sema hawana utamaduni wa kutunza fedha....wao wakipata hela ni kuwafukunyua wadada tu hela yote wana invest chini huko!
Huku wakijua kesho watapata hela tena kwenye Dili lingine wakati hawajui kuwa maisha siyo Kila siku utaterezaaa tu lazima Ipo siku utapigika

Ova
 
kweli mkuu
 
Kama Wanasiasa Na Wizi Na ma posho Yao yote wakiumwa hawawezi kujitibu ije kuwa wasanii?



Lissu hapa limetembezwa bakuli hatareee

Ndugai huko Kila kitu Serikal
Akina Sitta kule Germany Kila kitu ilikuwa Serikal

Sasa kati ya Wasanii Na Wanasiasa Nani alipaswa kuwa Na hela za kujitibia?
 
Duuh hili nalo neno... Maana majuto ukisema kuhusu mikataba yake anapewa hela ndio lakini hawezi iweka eti akiba kesho anaweza patwa na matatzo.. Yeye anapiga anajua kesho dili nyingne yajaaa..!! So tusiwalaumu sana.. Pia gharama za nje ni kubwaa sana mfano gharama Mil 10 jumla kuipata majuto binafsi si mchezo.. Sanaa yetu INATENGENEZA MASKINI WENYE MAJINA MAKUBWAA...
 
Tatizo lao ndilo la wengi wetu, hatupendi kusoma, kuandika na kuwa imara na makini kwenye mikataba, iwe ya chumba, vyumba, nyumba, ardhi au rasilimali na maliasili ya nchi...
Sisi tunadharau sana mikataba, hata ile kusema basi nimlipe mwanasheria bobezi laki 2 kwenye huu mkataba wa milioni tunakuwa wabahili..
Wasanii karibu wote wameingizwa kingi kwenye mikataba tu, hawawatumii wanasheria husika wala ile kuhangaika ile mikataba iwe na "clauses" nyingi za kuwasaidia...Ujinga wao faida kwa matapeli..
 
Hela wanapata sana tu sema matumizi Yao

Ova
 
kweli kabisa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…