Kuna faida gani ya umaarufu wa msanii kama hawezi hata kujitibia hadi achangiwe na wananchi?

Kuna faida gani ya umaarufu wa msanii kama hawezi hata kujitibia hadi achangiwe na wananchi?

Hawajitambui, Wala hawatambui thamani ya kazi zao na hadhi zao,
Hawatambui hadhi yao wao kama kioo ktk jamii, Hatambui kama anasa hazijaanza leo,
Hawatambui kama anasa zipo jana zipo leo zipo kesho na zitaendelea kuwepo.

Unakuwa msanii kwa miaka 20, Lakini wakati wa kustaafu hauna hata bajaji moja, Hauna hata kiinua mgongo kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii, Umeutumikia usanii kwa miaka 20 au zaidi lakini hata bima ya afya huna!

Hivi miaka 20 ya usanii wako uliwatumika warembo na pamoja na tumbo tu?
Ni aibu kubwa hii! Ni ujinga!
 
Wawe wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii, NSSF n.k

Walazimishwe na BASATA kujiunga BIMA ya afya.no NHIF card hakuna kazi zako kutambuliwa kisheria, badala ya basata kuwa ya kufungia tu nyimbo ijikite kwenye kuwasaidia hawa so called wasanii/ maarufu.

Umoja wa wasanii filamu na ubongo wa flava uwepo kisheria na kiuchumi zaidi.
 
Mtanzania ni Mtanzania tu!!!!
Hakuna kuwekeza kwenye bima (CHF kwa watu wa kawaida) premium kwa wenye nazo.
Ni kawaida mbunge, msanii, mwana michezo, tajiri (wa kijiji au mtaa) .....kuwa na gari, nyumba vya thamani. Muulize bima ya matibabu ...
 
NHIF waanzishieni wasanii package yao ya Bima ya Afya . Mtawapata wengi na mtawasaidia sana na hizi fedheha za kuomba omba kila siku wakiugua wanatembeza bakuli
 
Matibabu ni gharama sana...

Ndiyo maana kuna kitu kinaitwa Bima ya afya, angalau humpunguzia mtu ukali wa gharama za matibabu...

Kama unapata vijisenti ni vizuri sana ukajiunga na Bima ya afya ili yakitokea yakutokea msaada unao... la sivyo mtihani kweli kweli, siyo tu kwa wasanii, kwa kila mtu...


Cc: mahondaw
 
NHIF waanzishieni wasanii package yao ya Bima ya Afya . Mtawapata wengi na mtawasaidia sana na hizi fedheha za kuomba omba kila siku wakiugua wanatembeza bakuli
NSSF kuna voluntary package na mpaka matibabu unapata lkn hawajiungi
 
Kwa sababu wasanii hawana desturi ya kuweka akiba hii ya NSSF itawashinda mara moja
Sasa kama mtu huwezi hata kuchangia elf 20 kwa mwezi naww ni msanii bora ujifiche pangoni tu
 
Ngoja Wastara atoke kwenye matumizi Sweden...utaskia sijui nyonga sijui nini?
 
Tatizo lao hela wanapata sema hawana utamaduni wa kutunza fedha....wao wakipata hela ni kuwafukunyua wadada tu hela yote wana invest chini huko!
Huku wakijua kesho watapata hela tena kwenye Dili lingine wakati hawajui kuwa maisha siyo Kila siku utaterezaaa tu lazima Ipo siku utapigika

Ova
Wanadumbua kama ruzuku vile!
 
Wanadumbua kama ruzuku vile!
We jiulize Mtu anastafuu analipwa mln 100 na anajipanga kimaisha,hao wasani wanaingiza hela hizo ktk kipindi kifupi tu....tena Syo mara moja tatizo hyo mzee alikuwa anawadukua wadada sana hku akijua atapata deals zingine Hajui maisha hayatabiriki wakati wowote black inaweza kuwa white......mm wasanii siwaoni huruma n'a siwezi wachangia hela

Ova
 
Back
Top Bottom