Badala ya kuongeza ajira nyie mnazipunguza,
Makanjanja wa stand wakalime,wakajifunze ufundi,biashara nk.Huu mfumo utasaidia kuondoa wimbi la wazururaji pale stand.
Wapiga Debe hawana wanalofanya stand zaidi ya kelele na ghasia.
Kwa taarifa yako mfumo utaongeza ajira.Watu watajisajili kama mawakaka huko mitaani kama tunavyofanya malipo ya shule au ya serikali.Mawakala e- money watajiongezea kipato kwa hio ajira itapanuka katika mfumo rasmi usiokuwa na fujo.
Mfumo huu utawasaidia sana watu wavijijini.
Teknolojia haijawahi kukosea.
Naunga mkono hoja ya mdau kuwa serikali itapata mapato halisi ikisimama kidete hadi daladala zitoe risiti ya EFD mi ntawazonga makondakta wasiotoa risiti mpaka kwa trafiki.Trafiki wawe macho magari yasioyotoa efd.
Ziwekwe namba maalumu za kuripoti gari isiyotoa risiti on the spot.
Lazima tukubali kuhama(Paradigm shift).Yani sekta kubwa ya usafirishaji iendelee kuendeshwa kiholela, unakubaliana na hilo kisa mpiga Debe?
Waafrika tukubali kupokea mabadiriko kwa ustawi wa nchi, sio kila kitu kupinga kisa JIWE yupo madarakani.
Nchi isiendelee kisa kundi dogo la watu watakosa ulaji usio halali, mbona watumishi hewa walitoka na sasa tumesahau maisha yanaendelea.