SoC01 Kuna funzo kutoka Japan, nchi yenye uhaba wa dustbin lakini safi kimazingira kuliko maeneo yenye dustbin katika miji yetu

SoC01 Kuna funzo kutoka Japan, nchi yenye uhaba wa dustbin lakini safi kimazingira kuliko maeneo yenye dustbin katika miji yetu

Stories of Change - 2021 Competition

mdongooo

Member
Joined
Jun 20, 2019
Posts
8
Reaction score
3
Kwa miaka takriban mitatu niliishi mjini Tokyo, Japan. Ukiachilia mbali maajabu katika mifumo ya usafiri hasa treni katika mji huo, jambo ambalo lilinistaajabisha kila siku ni jinsi mji huo ulivyo msafi ilihali ni nadra sanaa kuona dastibini au mahara pa kutupa takataka katika maeneo ya public. Naweza sema hapa kwetu tuna maeneo mengi sana ya kutupa taka, mengi sana japokua inawezekana jinsi miundombinu hii ilivyodesigniwa ni moja wapo ya chanzo cha uchafuzi wa mazingira na sio utatuzi wa tatizo kubwa la taka mijini.

Swali Kubwa linabaki kuwa:
Ni wapi wajapani wanahifadhi taka, au mifumo yao ya taka ipo vipi? au wanakula mpaka taka ha ha ha, mana watu wa asia huwa tunawasingizia mengi sana jamani?

Mfumo wa Kijapani katika Taka:
  • Nilichojifunza ni kua nchi ya japani ina mfumo madhubuti na wenye ufanisi mzuri katika ukusanyaji taka
  • Kila nyumba au eneo litakalozalisha taka linatakiwa kutenga taka hizo katika makundi matatu 1) Platic 2) Zinazochomeka na 3) zile za vyakula
  • Gari la taka linakuja kwa uhakika bila kukosa, na linakusanya taka tofauti katika siku tofauti ambazo zinatofautiana katika au mkoa mtaa mmoja na mwingine
Utamaduni ulioniacha mdomo wazi:
- Wajapani wanapenda sana baiskeli, na ni kawaida sana kuwaona wajapani wakiweka taka taka ndogo ndogo kama maganda ya pipi, ice cream, chupa na zinginezo watakazozalisha wakiwa kwenye mihangaiko ya kila siku kwenye vikapu vya baiskeli zao au mabegi mpaka pale watakapoingia kwenye maduka a kwenda nazo kabisa nyumbani na kutupa huko (Convenient store) na kutupa humo. Ni Nadra sanaaa, tena sana kuona mtu anatupa tu mahara, haimaanishi hawa kina tomaso hawapo. Na kwakua ni watu wachache sana watatupa taka ovyo, kazi ya wafanya usafi katika miji inakua ndogo sanaa na haiwashindi nadhani.

Swali Langu Kwenu?

Nadhani hili linawezekana hapa kwetu ila maswali yangu ni 1) Ni kwa kiasi gani mfumo huu unaweza fanya kazi hapa kwetu?, 2) na itatugharimu nguvu kiasi gani ikiwa unaweza fanya kazi hapa kwetu?
 
Upvote 2
Mbali na usafi, wajapani nahisi ndiyo taifa linaongoza kwa uadilifu Dunia kitu kinachofanya Passport Yao iwe na nguvu kuliko mataifa mengine.
 
Mbali na usafi, wajapani nahisi ndiyo taifa linaongoza kwa uadilifu Dunia kitu kinachofanya Passport Yao iwe na nguvu kuliko mataifa mengine.
Uadilifu gani wakati Wana igiza x balaa yaani Japanese teens, Japanese mom ndo zimejaa kwenye site
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Yaani unibebeshe taka kwenye mkoba wangu nirudi nazo nyumbani..
Labda sio Mtanzania mimi
 
Uadilifu gani wakati Wana igiza x balaa yaani Japanese teens, Japanese mom ndo zimejaa kwenye site
Nadhani ulipaswa kukumbuka sijasema wajapan ni Malaika. Porno actors hakufanyi jamaa wasiwe number one.
Nb: Sasa hivi unatumia site gan kumcheki hayo madude ama ndiyo meendo wa VPN TU😂😂?
 
Usafi ni imani
Kwa baadhi ya nchi suala la usafi halipo kabisa
Fikiria unaona mpaka ma actor wetu wana act huku wanatupa chupa za maji toka kwenye gari yaani kama ni ufahari vile (hapo unategemea mtoto aelewe nini?

Uchafu watu wanaona ni fahari ya mwafrika
 
Back
Top Bottom