Kuna Genge ndani ya CCM linajiandaa kumuondoa Samia 2025 kwa Mlango wa Nyuma

Sio rahisi, mfumo wa ccm Mwenyekiti ndie mmiliki wa chama. Tuliwaambia waondoe kofia mbili ndio kitanzi chao awataki kusikia.
Mwenyekiti wa chama ndiye pia Mkuu wa nchi na ndiye pia Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya nchi inayoitwa JMT !! ni nani mwenye ubavu wa kufurukuta ??!!
 
Yule alikuwa anatunyonga sisi kwanza
 
siasa njaa mbaya sana hivi wakati wa Magufuli makamu wake alikuwa nani
"Bahati mbaya serikali ya SSH kwasasa imeanza kunukia " udini" hii imekwenda mpaka kwenye Chama, Samia Ni dini Moja na Makamu wake Kinana hii inanung'unikiwa sana kuwa miwani ya SSH haikuliona hilo vizuri."
 
Wacha ukichaa......Philip Mangula aliyekuwa Makamu Mwenyekiti na Mwenyekiti wake JPM upande wa chama walikuwa wanaswali musikiti gani? Wote walikuwa mavaticana! Mbona hukulalamikia udini?
 
Mh. Samia hawezi kuwa rais wa viwango hata kidogo, hapo umenikatisha tamaa kuendelea kusoma, wewe ni miongoni mwa wale wachawi wachache mnao haribu uongozi wa Mama.
 
Wewe ni fungus la kukosa, umeandika utumbo mtupu. Jiandae kisaikolojia kutawaliwa na Samia hadi 2030
 
Bahati mbaya unaandika nadharia tu ila hujui nguvu za Mwenyekiti wa CCM.
 
Kifupi nchi ememshinda. Ila wanangonjera wanaendelea kuimba kumsifu. Subiri tu…
 
Bahati mbaya unaandika nadharia tu ila hujui nguvu za Mwenyekiti wa CCM.
Mwenyekiti hana nguvu kuwazidi vyombo vya ulinzi na usalama, kitu ambacho inaonekana mpaka sasa labda kama ana timiza matakwa ya mafisadi na kama ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama kuna mafisadi. Hata Pakistan ndivyo walivyo, mafisadi walishateka kila kitu. Nchi yetu bado iko mikono salama angalau. Mwenyekiti angekuwa na nguvu Dkt Magufuli wasingemuua kizembe vile.
 
Wanachama wake wana haki zote

Iwe ni genge au magenge

Wananchi pia wanahaki ya mlango wa Kura.

CCM oyeee!
 
Samia tutamlinda Kwa nguvu zote.

Hakuna Udini Wala ukabila. Hatuchagui Imamu Wala Askofu .

Mnaanza kumchukia Kinana baada ya kusema waliohusika na wizi kwenye ripoti ya CAG wawajibishwe mmeficha mabilioni ya pesa ndani . Dawa yenu ni kubadili pesa ili mpate aibu. Kifo Cha JPM kimewanyanganya tonge mdomoni. Kumbe Kuna watu wanategemea Ikulu kuendesha maisha yao. Kuna wengine hata pasipo kuwa na Rais maisha yanasonga bila tabu.
Tunawachukia Wahalifu TU na ndio tunatamani wapigwe hata mabomu ya Nyuklia jamii iwe salama.

Mama Samia atuletee haki TU na katiba mpya. Mengine yatajipanga TU freshi.

Mliopewa Ubunge wa Mchongo na teuzi za kikabila na kikanda mtapata tabu sana.
Mama ameitangaza nchi Kwa kiwango Cha Nyerere ndani ya mwaka mmoja TU.
 
JPM chairman+Mangula vice chairman !!!????
 
Basi subiri SSH aweke demokrasia, Kura zipigwe na kuhesabiwa mchana kweupe. Amin Amin nakwambia utakuja kulalamika kwamba uchaguzi ulikuwa wa ovyo.
Haki siku zote haijifichi Wala haileti ubishi.

Ndio maana mahakama inaogopwa na kuheshimiwa bila kutumia mabavu. Uchaguzi ukifanyika Kwa wazi na Kwa huru hakuna mtu anayeweza kufanya fujo Wala kulalamika.

Kuanzia,kuchukua na kujaza fomu mpaka kampeni hua Jeshi la Polisi na Tume wanajiweka upande wa CCM ili kulinda maslahi binafsi.
Kama ni IGP basi analinda nafasi yake na sio Taifa. Wakurugenzi wanalinda nafasi zao sio haki Wala Taifa. Hali kama hiyo haiwezi kuleta amani kwenye uchaguzi. Nchi imejaa majizi matupu kutokana na chaguzi za wizi.
Kinana atainyoosha CCM ya Majambazi na kukifanya kuwa Chama Cha siasa. Tulipokua tunaelekea siasa zingekua ni uadui na kuuana TU. Uzalendo ulitumiwa vibaya na kuruhusu wauaji kuingia kwenye siasa.
 
Sikweli
 
Kama watanzania hatutaungana 2025 kuing'oa CCM hii ya WEZI titaishi kwa taabu sana,HAKUNA cha maana tena tunachoweza kutarajia kwa CCM HAKUNA hakuna HAKUNA.
Bado Rais Samia ana nafasi ya kuwa Rais Bora sana. Hakuna mpaka Sasa mtu wa kuiongoz hii nchi zaidi ya Samia. Bora tupigane kuliko kumtoa Mama.
Nchi ilikua ni takataka la mauaji ya Siri Siri.
Watu wameuawa na KUPORWA Mali zao walizotafuta tangu miaka ya 80 na Vijana WALIOZALIWA juzi kupora na kujilimbikizia Mali Kwa mgongo wa uzalendo. Noo.
Kila mtu afuate Sheria sio wachache kujiona miungu.
Mabilionea wazawa Kwa muda mfupi walianza kufa vifo vya utata hatutaki Tena Hali hiyo itokee Kwa sababu ya Siasa za kuibeba CCM na woga wa kushindwa
 
Yeye alijua hawezi kushinda na asingemshinda Mwamba Tundu Lissu.
Maka aligokewa kufanya kampeni Kwa uhuru. Mara akataliwe kutumia Helkopta mara tutampiga sindano ya sumu mara azuiliwe alimradi TU asifanye kampeni. Kilikua ni kipindi Cha Wahalifu kwenye siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…