Kuna haja gani kumtazama marehemu ikiwa tunamfahamu na tumeishi naye miaka mingi kabla ya kifo?

Sisi Waafrika tumelogwa na wakoloni na pia utamaduni wao na kuona wa kwetu hautufai.
Angalia majina tunawapa watoto wetu majina ya Kizungu au Kibiblia au Kiqur'an tukidhani Ukristo au Uislamu kumbe yale ni majina ya kwao hata kabla ya Ukristo au Uislamu kuwepo.
Ni majina ya kwao. Sisi tunaoma ukimpa jina John au Hassan ndio kuwa mtu wa dini.
Jina sio dini tutumie majina ya lugha zetu. Tunaweza kuwa majina ya kwetu na tukawa wacha Mungu wazuri

Hatutaki kubadilika, tumechotwa na utamaduni wao tunapuuza hata ya kwetu ingawa tunawasema vibaya hao.
Tuna lugha zetu na majina yenye maana nzuri tu.
 
Mazishi tunahidhuria kwa ajili ya kuwafariji wafiwa pamoja na kusaidiana nao katika kutatua changamoto zinazohusiana na msiba..
 
Mazishi tunahidhuria kwa ajili ya kuwafariji wafiwa pamoja na kusaidiana nao katika kutatua changamoto zinazohusiana na msiba..
Hoja hapa sio wafiwa, hoja hapa je unachokifanya marehemu atajuaje maana hakuoni.

Kama ni kuwafariji wafiwa unaweza kuwafariji hata baada ya kua marehemu amezikwa.
 
Kuaga ni kopi ya tamaduni za ki magharibi zilizoingia kwenye jamii zetu. Ni sawa na mchezaji kufunga goli wakati refa keshamaliza mpira.
Mimi ni mkristo kiiman. Ila ukiifuata biblia sehem zote inaweka wazi watu walifanya maombolezo lakin sio kuuaga mwili.
#Yesu alipokufa hakuagwa
#Musa hali kadhalika
#Daudi pia
Na wengineo wengi
 
Kama kwa bahati nzuri ukifiwa na mwanao uzuie na ukataze watu wasimuage mwanao ,weka utaratibu unaoona unafaa
 
Nimelipenda jina lako! Nsibwene! Cha ajabu wanao utawapa majina hayo hayo ya kizungu au kiarabu 😀 😀
 
Naam!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Mlimuona mara ya mwisho katika uzima, usipo muona katika mauti ubongo hauwezi kumfuta kuwa hayupo tena. Hivyo ni kuujulisha ubongo kuwa hayupo tena na ule muweweseko wa uzima unatoka akilini
 
Hai wastaarabu Sana. Sisi Mila Yetu Ukifa tunaupaka Mwili wako Mafuta mazuri ya nayonukia Kisha tunaondoka na kuuacha fisi waufanye kitoweo!
 
Ukifa kuna haja ya Sisi kuja Kukuaga kwa Kukutizama ukiwa 'Jenezani' wakati kwa zaidi ya miaka 30 Bichwa lako Baya na Nyago ( Sura ) lako baya tunalijua?

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mkuu ndio maana wasema KUTOA HESHIMA ZA MWISHO
 
Hai wastaarabu Sana. Sisi Mila Yetu Ukifa tunaupaka Mwili wako Mafuta mazuri ya nayonukia Kisha tunaondoka na kuuacha fisi waufanye kitoweo!
Sisi wa mjini fisi wanatoka wapi
 
Ni mambo yaliyotungwa na binadamu kumuongezea faraja wakati amefiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…