Sisi Waafrika tumelogwa na wakoloni na pia utamaduni wao na kuona wa kwetu hautufai.Tena kwa kuongezea hapa. Ukishashuhudia unapata faraja kwamba mwamba kaenda na unabaki na amani na unamfuta kichwani na maisha yanaendelea bila kuwaza au kufikiri utamuona tena! na unajifunza one day nitaondoka hapa duniani kama wengine... inarudisha na utu wa kuthamini wengine ukijua wewe ni mpitaji tu kama wengine walipita....
Angalia majina tunawapa watoto wetu majina ya Kizungu au Kibiblia au Kiqur'an tukidhani Ukristo au Uislamu kumbe yale ni majina ya kwao hata kabla ya Ukristo au Uislamu kuwepo.
Ni majina ya kwao. Sisi tunaoma ukimpa jina John au Hassan ndio kuwa mtu wa dini.
Jina sio dini tutumie majina ya lugha zetu. Tunaweza kuwa majina ya kwetu na tukawa wacha Mungu wazuri
Hatutaki kubadilika, tumechotwa na utamaduni wao tunapuuza hata ya kwetu ingawa tunawasema vibaya hao.
Tuna lugha zetu na majina yenye maana nzuri tu.