Kuna haja kubwa ya Watanzania kujifunza English,huyu dereva teksi ametuaibisha

Kuna haja kubwa ya Watanzania kujifunza English,huyu dereva teksi ametuaibisha

Kuna rafik yangu hajui kiswahili ameingia tanzania leo kuja kutalii,ametoka marekani akaenda kwanza Entebe Uganda,kisha Nairobi Kenya leo kafika Dar.
sasa kanipigia simu ananiuliza nimwambie maana ya ten book wameshindwa kuelewana na dereva teksi,amemuuliza dereva teksi kwenda katikati ya mji ni kiasi gani dereva teksi hakajibu teni buku yani anaamanishi buku teni ( 10,000)
na amejiona yuko sahihi.

kuna haja ya kujua vizuri kiswahili na kiingereza pia ni muhimu sana kwa dunia ya sasa hivi kama wewe ni mfanyabiashara.Amesikitisha sana dereva teksi hatuna budi kujua ata vitu muhimu muhimu.

Huyo jamaa yako ndiyo amezidi ushamba, vitu vya kwanza kujifunza kabla hata haujaenda nchi za watu ni salamu na pesa! hajui hata pesa ya bongo inaitwaje, hajui elfu hajui moja hajui kumi ni kilaza tu! Mwambie aende China akaone. Safi sana dreva teksi, tena ungemwambia tu, ELFU KUMI, mbona inaeleweka. Wewe unatuaibisha tu.
 
Eti katoka Marekani nyoko kabisa, mbona sisi tukienda kwao tunakomaa na yeye akomae tu.
 
Si mnakazania kiswahili eti "ni uzalendo?" Vumilieni ila eleweni kuwa NJE YA TANZANIA, MTANZANIA NI BUBU! Not even in Kenya!

Siyo Mtanzania pekee, Hata Mchina, Mjapani, watu wa Latino, Waitaliana, huwezi kujifunza milugha yote ya dunia ndugu yangu. Mwenyeji wa mtu ni pesa, lugha zitagongana hivyohivyo mtaelewana.
 
Uongo huo maana bei haitoi picha halisi ya gharama ya taxi kutoka airport to city centre, kichekesho chako ungekifanya kiendane na hali halisi

nani amekwambia amekuja na ndege akitokea nairobi?
 
Mzungu kaja na Dar Express toka Nairobi. hii buku ten ni kutoka Ubungo terminal mpaka Sinza kwa Remmy. Huyu kaka hana rafiki wa hadhi ya ndege

acha ushamba mtu akipanda bus siyo kwamba hana hadhi ya ndege wetalii wengi upenda bus ili atalii vizuri acha kasumba za ajabu ajabu
 
Mkuu, najaribu kufikiria uhalisia wa scenario nzima.

1. Yaani Dreva tax ALIMUELEWA rafiki yako kwa lugha ya kiingereza ila kujibu ndio ikashindikana?!!!!!!

2. Kwa gharama za hapa Dar nadhani, hii "ten book" wether kutoka Ubungo hadi City Centre au niKutoka Airport hadi City centre ni ndogo(haiendani) HASA kama abiria kweli alikuwa 'mzungu'.

kuhusu ilo la gharama buku ten ndio aliyoambiwa kama mnaona ni ndogo mkate rufaa mahakamani .

mim nahis hiyo ndio ilikuwa rahis kutamka kwake kuliko 15k
 
ungepost kwa kingereza ndo tungejua wewe ni mjuzi kiasi gani..siwez kuamini hili maana madereva wengi hata wa toyo hakuna asiejua hela kwa kingereza usidhani wote ni mbumbumbu kama wewe wengine ni wasomi wazuri tu hupenda kutumia muda wa mapumziko na likizo kujiongezea kipato na magar yao kuliko kulala home..so unavyonianbia et driver tax ameshindwa kusema elf kumi kwa kingereza hata sikuelewi..huu ni uzi tu
 
Mkuu mimi nitakinzana na wewe, na nina sababu kadha wa kadha zenye kunifanya nikinzane nawe lakini kwa sasa nitadokeza hii moja tu.

Unapoamua kutembelea nchi maarufu mathalani hizi ambazo zina umaarufu wa utalii kuna misamiati inakupasa ujifunze ikiwemo hii ya kuulizia bei ya usafiri kama wa taxi.

Ukiwa kama mtalii ingawaje dhumuni kuu ni kutembelea vivutio vya utalii, lakini katika kuifikia nia hiyo kuna mambo ya kitamaduni yahusuyo nchi uiendeayo yakupasa ujifunze.

Nimepata kufika Ethiopia na wakati fulani China na Thailand, raia wa huko ni aghalabu kuwasikia wakiongea Umombo na hata wakiongea basi ni zile sentensi za kubabaisha sana.

Kuna sentensi fupi fupi ilinipasa kujifunza au kutembea na vipeperushi vilivyo na translations za lugha hizo kwa ajili ya kuniongoza.

ata kama utakinzana na mimi kiingereza ni muhimu kujua utambue ilo.

viongoz wanaokomalia kiswahili kitumike watoto wao wanasoma shule za kiingereza.

pia inaonyesha hujanielewa mwishon nilisema watu wajue kiswahili vizuri pia english muhimu
 
Kuna rafik yangu hajui kiswahili ameingia tanzania leo kuja kutalii,ametoka marekani akaenda kwanza Entebe Uganda,kisha Nairobi Kenya leo kafika Dar.
sasa kanipigia simu ananiuliza nimwambie maana ya ten book wameshindwa kuelewana na dereva teksi,amemuuliza dereva teksi kwenda katikati ya mji ni kiasi gani dereva teksi hakajibu teni buku yani anaamanishi buku teni ( 10,000)
na amejiona yuko sahihi.

kuna haja ya kujua vizuri kiswahili na kiingereza pia ni muhimu sana kwa dunia ya sasa hivi kama wewe ni mfanyabiashara.Amesikitisha sana dereva teksi hatuna budi kujua ata vitu muhimu muhimu.

Mbona hujamlaumu mzungu kwa kutojua kiswahili ilhali yupo ktk taifa linaloongea kiswahili 100%
 
ungepost kwa kingereza ndo tungejua wewe ni mjuzi kiasi gani..siwez kuamini hili maana madereva wengi hata wa toyo hakuna asiejua hela kwa kingereza usidhani wote ni mbumbumbu kama wewe wengine ni wasomi wazuri tu hupenda kutumia muda wa mapumziko na likizo kujiongezea kipato na magar yao kuliko kulala home..so unavyonianbia et driver tax ameshindwa kusema elf kumi kwa kingereza hata sikuelewi..huu ni uzi tu

kama unakataa siwez kukulazimisha ukubali.

ila ushike maneno niliyoandika chini watu wajue kiswahili pia kiingereza ni muhimu.

wajue ata vitu muhimu tu.
 
hapo ndipo siku zote napingana na nyerere na mfumo wa kutumia kiswahili ambacho kimetufanya kuishi kwa kujidharau kama siyo kudharauliwa even na majirani zetu

Kwani kutokujua Kiingeleza ni dhambi kubwa, Acha kuwa na mawazo yenye fikra mgando.
 
Nkisikia wanaotetea lugha za wazungu nasikiaje hasira! Ndio tunawadate hey sio sababu ya kuwanyenyekea,ukija nchi zao mbona wao hawasikii aibu eti hujui english.
Yes ni muhimu hii lugha,ila kiswahili chetu tukikazanie,wakiwa wanakuja hata basics muhimu wajue!
Ujue mzungu akiongea broken swahili watu wanaona kama ni swaga,ila sie ukiongea broken english wao hawacheki wanaelewa kuwa hujui ila sisi kwa sisi heheh lazima kinuke!!!utashikiwa bango kama rip Kanumba alivosemahga im closing instead of fasting in bba!!!
English ni muhimu ila wabongo took it in another level!
China wao kama hujui chunchi cha utajijua na english yako ila wao wakienda kwa wageni wanajifunza!
Anyway ten book hahahhaha....theat dude KIlled it!!!so funny ila hata simcheki !
Serikali ibadilishe mfumo swahili from the root,ila wao wakija iwe must kujua basics period!!!
Ok bye nainai
 
English ni muhimu kujua tusijifananishe na china.
China wamejitosheleza kwa kila kitu.mkumbuke tukijua english tunaweza kwenda nchi yoyote duniani na tusipate shida kuwasiliana.

Kaz zenyewe siku hiz unaambiwa lazima ujue english.

Hivo kama hatujui english hali itakuwa ngumu dunia sasa imekuwa kijiji ndio maana Tanzania tunawahofia kenya na uganda kuchukua ajira zetu si kwa sababu elimu ya bora bali lugha ndio sababu
 
ata kama utakinzana na mimi kiingereza ni muhimu kujua utambue ilo.

Umuhimu wa lugha hutegema na uhitaji wa matumizi ya hiyo lugha...

Kuna watu wa kada fulani kujifunza na kufahamu Umombo ni muhimu lakini kuna watu wa kada nyingine si muhimu...

Hivyo huwezi hitimisha kwa kuandika "Kiingereza ni muhimu" pasipo kutaja kwa makundi au kada zipi...

viongoz wanaokomalia kiswahili kitumike watoto wao wanasoma shule za kiingereza.

Kiongozi lazima akomalie lugha ya Taifa lake, hii ni sehemu ya utamaduni wetu na ni urithi wa Utaifa wetu.

Sijui kama umeshawahi kujifunza sifa za Taifa kuwa ni lazima wawe na lugha inayowatambulisha??

Watoto wao wanasoma shule hizo kwa kuwa wanahitaji kujua lugha hiyo, la hasha si lazima uende shule hizo ili ujue kwa uzuri lugha ya Umombo.

pia inaonyesha hujanielewa mwishon nilisema watu wajue kiswahili vizuri pia english muhimu

Nimekuelewa na na hata hiyo sentensi uliyoiandika kama hitimisho nimeiona...

Sijaipa uzito kwa kuwa karibu 90% ya habari yako umesisitiza umuhimu wa lugha ya Umombo...
 
Kuna rafik yangu hajui kiswahili ameingia Tanzania leo kuja kutalii, ametoka marekani akaenda kwanza Entebe Uganda, kisha Nairobi Kenya leo kafika Dar.

sasa kanipigia simu ananiuliza nimwambie maana ya ten book wameshindwa kuelewana na dereva teksi,amemuuliza dereva teksi kwenda katikati ya mji ni kiasi gani dereva teksi hakajibu teni buku yani anaamanishi buku teni ( 10,000)
na amejiona yuko sahihi.

kuna haja ya kujua vizuri kiswahili na kiingereza pia ni muhimu sana kwa dunia ya sasa hivi kama wewe ni mfanyabiashara.

Amesikitisha sana dereva teksi hatuna budi kujua ata vitu muhimu muhimu.

Hata wewe mwenyewe kiswahili kinakushinda, katika paragraph ya pili "............kiasi gani dereva teksi hakajibu...." unamaanisha nini unaposema hakajibu

Pili wasema rafiki yako alikuwa anakwenda katikati ya mji, kutoka Ubungo kwenda city centre ni Tshs 15 - 18 Thousand, unasema toka ubungo kwenda sinza, tangu lini sinza imekuwa katikati ya mji?
 
Unamuongelea dereva wa dala dala/ taxi ambaye elimu yake ni darasa la 7 au form 4. wachache sana wana elimu ya form 6.
Nina mashaka hujafanya kazi kwenye mashirika binafsi na miradi au kampuni za kimataifa ambazo report zote zinaandikwa kwa kingereza na pia lugha kuu ya mawasiliano na viongozi ni kingereza! Utapewa report ya mtu msomi, shahada mbili (Masters) au hata mwenye shahada moja na usielewe kama imetoka kwa msomi. Kingereza kinatupa shida wasomi, itakua dereva taxi? Tunatia aibu sana maofisini! Lakini mabosi wetu wakituzoea wanaelewa kwani si lugha yetu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kuna rafik yangu hajui kiswahili ameingia Tanzania leo kuja kutalii, ametoka marekani akaenda kwanza Entebe Uganda, kisha Nairobi Kenya leo kafika Dar.

sasa kanipigia simu ananiuliza nimwambie maana ya ten book wameshindwa kuelewana na dereva teksi,amemuuliza dereva teksi kwenda katikati ya mji ni kiasi gani dereva teksi hakajibu teni buku yani anaamanishi buku teni ( 10,000)
na amejiona yuko sahihi.

kuna haja ya kujua vizuri kiswahili na kiingereza pia ni muhimu sana kwa dunia ya sasa hivi kama wewe ni mfanyabiashara.

Amesikitisha sana dereva teksi hatuna budi kujua ata vitu muhimu muhimu.

Dereva tax yupo sahihi, hiyo ni lugha yake na anaipenda.
 
Back
Top Bottom