Kuna haja kubwa ya Watanzania kujifunza English,huyu dereva teksi ametuaibisha

Namlaumu sana rafiki yako ambae alishindwa kujua kuwa anakuja ugenini hivyo angehitaji kuwa na mwenyeji yatapotokea madhila kama hayo. Nina mashaka na upeo wake wa kufikiri kwa kweli...
Kujifunza Kiingereza sio lazima, ukizingatia dereva teksi yuko kwao ambako Kiswahili ni lugha yao. Mawazo duni kama haya ndio yanamfanya mtu ashindwe kujiamini kabisa kwa kuwa tu hajui Kiingereza, na pia yanafanya watu washoboke na zuzu kwa kuwa tu anazungumza Kiingereza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…