Yaani watu wote wanaokosoa ule utawala wa kimbilikimo ni wezi? Watu kundika juu ya ufedhuli wa kile kipindi cha giza ni kupiga kelele? Ukisikia watu kukosa hoja ndiyo hii! Lakini haishangazi kwani hata kipindi kile hakikuwa kipindi cha kupambanisha hoja; kilikuwa kipindi cha hoja kupigwa rungu! Marehemu alibana wezi wa awamu iliyotangulia ili aweze kustawisha wezi wa awamu ya tano ambao kusema kweli walikuwa waporaji na wabaya mara elfu kuliko wa awamu zote zilizotangulia. Ubaya wa wezi wa awamu ya tano ni kwamba walilenga kuua taasisi na vyombo rasmi vya nchi na kuvipora majukumu yake kwa umma na badala yake vyote vikaelekezwa kutumikia genge la uhalifu, wezi na wanyang'anyi! Ofisi ya CAG ni chombo rasmi cha kikatiba cha kuwezesha nchi kusimamia matumizi mazuri ya rasilmali zake. Aidha Prof. Assad alijipambanua kama mzalendo na mwanataaluma mahiri, asiyeyumba, asiyerubunika na aliyekuwa tayari kuisadia nchi hii kudhibiti wizi wa rasilmali za umma. Nini kilimtokea? Si Katiba ya nchi ilivunjwa ilimradi tu aondolewe ofisini? Vyombo vya habari vina nafasi kubwa sana katika kuibua vitendo vya wizi, ufisadi na ubadhirifu na kuisadia nchi kupambana na matendo hayo; alivifanyaje, si alivifungia na kuvinyamazisha? Asasi za kiraia ni washirika wazuru sana wa serikali makini yenye dhamira ya kupambana na maovu katika jamii ikiwa ni pamoja na wizi wa mali ya umma; aliviua!
TAKUKURU ni chombo cha serikali cha kupambana na rushwa; hatua yake ya kwanza alipoingia madarakani ni kumstaafusha Mkurugenzi Mkuu, kwa kuamini kuwa hataweza kukubali kupokea maelekezo yasiyozingatia dhamana ya taasisi hiyo. Badala yake akapeleka Polisi akijua hao wamelelewa kupokea amru tu. Matokeo yake TAKUKURU ikaacha kupambana na rushwa ikafanya kazi kisiasa. Kifupi, marehemu hakuwa na dhamira hata chembe ya kupambana na wizi na ufusadi; alikuwa anafanya hadaa tu ili aweze kufanya mambo yake! Bahati mbaya raia wengi "wanyonge" walidanganyika sana na kauli nyepesi za rais wa wanyonge, nchi hii imechezewa sana na vitendo vya kutumbua watumishi bila kufuata sheria!
Alifanya nini kuhusu 1.5t/= ambazo zilipotelea hazina na kubainishwa na mamlaka ya kikatiba, yaani CAG? Na sasa tunasemaje kuhusu billions za plea bargain zilizofichwa China. Ipo siku haya yote yatafanyiwa kazi.