Kuna haja kwa Watanzania kumsamehe hayati Dkt. John Magufuli. Nini kifanyike?

Mbowe; Ninakuomba Mh Rais chama chako kisituletee Rais mwingine aina ya mtangulizi wako aliyeumiza upinzani.

Kauli hii ni dhahiri kuwa Magu alisababisha tuvione vyama vya upinzani ni vyama vya usaliti Kwa wananchi.

CDM wawaombe radhi Watanzania Kwa kuwauza Kwa CCM kupitia lugha ya maridhiano.
 
Miaka 2 mtu hayupo lakini mtu anashuka ese hadi page nyingi kwa makasiriko huko si nikujistress tu, maana hata ukifikiri unawakomesha wanaompenda wala huwakomeshi hakuna mtu anampenda mwingine kwa kiwango hicho.

Watu mkitaka mpone wanasiasa na vyeti feki kubalini hakuna namna mambo yatabalika lilishatokea sameheni maisha yaendelee.
 
Unakuta mtu anacommet kwa hasira kama anapigana na simu yake,kumbe anamfokea Marehemu.Kweli huu ni uchizi.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Tuwahurumie ujue sio jambo la kawaida, Ulikua unamshahara harafu ghafla hola, unaanza kuuza genge lazima makasiriko kama yote na kushusha essay kwenye kila thread ya huyo mtu.
 
Kwani baba akikunyoosha ili uwe katika hali nzuri ya maisha anafanya kosa? Kwanza mshukuru, watoto watakaochukia ni wale wavivu na wezi katika familia. Tulio wengi tunashukuru kwa kutuamsha katika usingizi. RIP baba.
 
Ili watu wasahau muacheni msiandike habari zake. Inaonekana kuna watu wanahasira nae akitajwatu wanalipukwa na hasira na chuki za dhahiri.
Mimi mmojawao,nikisikia jina lake tu Mori inapanda
 
The guy is dead and gone kamwe hawezi kurudi.
Tuachane na story zake tusonge mbele tu.
 
Kweli kuna haja ya kusameheana...

Maridhiano ni mpaka kuwe na pande mbili..

Kufanya maridhiano, itamaanisha kuwe na kamati itakayochunguza na kuweka bayana maovu yote ya marehemu, halafu wapatikane walioathirika moja kwa moja, kama vile familia zilizopoteza wapendwa wao ambao waliuawa kwa amri ya marehemu, waliotekwa, waliopotezwa, waliobambikiwa kesi, walioporwa pesa zao, walioporwa kura zao kwenye uchaguzi, n.k.

Unadhani hilo litapunguza au kuongeza hasira?
 
Upande uliohusika ukikiri makosa na kuomba, maridhiano yatakuwepo..KUKIRI MAKOSA.
 
Haitokaa itokee tena, tumejifunza kosa la kumpa mshamba aongoze nchi
 
Kama kuna Watanzania walioumizwa ba JPM kuhamia Ddm, waseme. Kama kuna,walioumizwa na standardgauge nao waseme. Kama kuna walioumizwa na umeme wa Bwawa la Nyerere, nao wajitokeze waseme. Waliomizwa na daraja la Selander Bridge au flyover za TAZARA na Ubungo, waseme. Kama kuna walioumizwa na maji na umeme na lami kila mahali (zamani ilikuwa sehemu chache tu za CHADEMA kupitia watendaji wa kutoka huko waliojaa serkalini na mashirika ya umma), nao waseme. Ila najua kina mbowe walitaka kumuua ole Sabaya ili Nchi iingie taharuki wakakamatwa, au waliokuwa wanaiba nyaraka za siri Mahakamani kuwapa mabeberu wa ndege zetu na makanikia hawo ndio wameumizwa na JPM. Au moneylaundrers walitumiwa na mabeberu kutakatosha hela chafu. It was their privilege, it is now their problem - deal with it, sisi msituhusishe.
 
Then kuwe na aina fulani ya fidia kwa wahanga
 
Wapo walioumizwa na risasi. Wapo walioumizwa na kwa account zao kuporwa fedha. Wapo watanzania walioumizwa kwa kunyimwa haki ya kukusanyika na kusema. Wapo walioumizwa kwa kuvunjiwa nyumba zao bila malipo stahiki. Wapo walioumizwa kwa kuachishwa kazi kinyemela. Wapo walioumizwa kwa ugawaji wa tenda kindugu. Wapo walionyimwa ajira kwasababu hawatoki kanda ya ziwa, etc.
 
....bila kusahau ambao ndugu zao walipotezwa au kuuawa, eg Azory Gwanda, Ben Saanane, wale wa kwenye viroba, nk
 
Angalia hapa utajua cha kufanya 2025
 

Attachments

  • IMG_8954.MP4
    13.3 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…