Kuna haja ya kuangalia mavazi ya mtu kwenye usaili wa kazi?

Kuna haja ya kuangalia mavazi ya mtu kwenye usaili wa kazi?

Unajua ndio maana Watanzania wengi hatupati kazi nje ya nchi. Huwa tunadeal vitu ambavyo havina maana kwenye maombi yetu ya kazi.
 
Unachekesha kweli wewe. Kwangu mimi first impression matters na usinichukulie poa. Mengine uliyosema ni bullshit tu
Kwako wewe (USIYE NA AKILI) wenye akili hawawezi kutumia huo mfumo. Kwa maana haupimi akili na uelewa wa mtu bali mwonekano ambao pia sio kigezo cha kumpata mtu mahiri.
 
Kwako wewe (USIYE NA AKILI) wenye akili hawawezi kutumia huo mfumo. Kwa maana haupimi akili na uelewa wa mtu bali mwonekano ambao pia sio kigezo cha kumpata mtu mahiri.
Nisiye na akili ndiye mwajiri sasa. Nawaajiri ninyi wenye akili kwa vigezo vyangu nivitakavyo mfanye kazi kuendana na job description yenu.
 
Kwenye kutafuta ajira kuna mambo mengi sana. Wasakatonge tunahangaika huku na huko kutafuta mrija wa Asali, iwe nje ya nchi au ndani ya nchi, iwe serikali au taasisi binafsi.

Sasa basi nikiwa mmoja wa wasakatonge nilibahatika kuomba hizi kazi za TRA, na mara baada ya kuomba nikafanikiwa kupata Group moja la tulioomba kazi.

Kupitia hili group bhana, juzi usiku nikaona mjadala umeanza, mmoja wa wanagroup alitoa angalizo kuwa iwapo wasailiwa watafanana kwa marks basi kuna kigezo cha mavazi kinatumika katika kuwaondoa au kuwapata best candidate.

Kwamba watu wavaze official, kwenye usaili inakuwa rahisi kupata kazi, na mjadala ukawa mkubwa sana.

Tiliozoea kufanya saili mbalimbali hasa za serikali tukakubaliana yes mavazi ni muhimu sana, na yanachangia kwa asilimia kubwa kwenye kuchaguliwa kupata kazi.

[emoji91][emoji91][emoji91] Hapa sasa akatokea member mmoja akasema kigezo cha Mavazi hakitumiki kwenye kuchagua best candidate kwa maana Mavazi ni kipimo cha utajiri wa mtu au familia. Hivyo kigezo cha Mavazi hakiwezi kuwa sifa moja wapo ya mtu kuajiriwa na kwamba mtu anaajiriwa kwa uwezo wake kichwani.
Na ikiwa umepata ajira basi taasisi husika ndio itakuwa kanuni na taratibu za mavazi ya taasisi hiyo kama mwajiriwa.

Akaenda mbali zaidi akasema kama mavazi yanaamua nani aajiriwe kwanini wasiweke sare maalumu za usaili ili watu wote waende wakiwa sawa kimavazi?

Nilitamani kuona ule mjadala unaendelea nipate kuona namna gani sisi vijana tunaweza kuchambua mambo kisomi na kwa kuzingatia Dunia inavyoenda. Bahati mbaya leo asubuhi nimeingia nimeona group sasa wenye uwezo wa kutuma kitu ni Admins tu.

Binafsi nimeona saili nyingi ma HR wakiangalia mavazi, na wengi wamekosa kazi kupitia uvaaji.

Je wadau tujadili hapa, mavazi yana uhusiano na upatikanaji wa kazi? Na je unakubaliana na hoja ya jamaa kuwa mavazi hayapaswi kuwa kigezo cha mtu kuajiriwa bali weledi na uwezo wake wa kujua mambo?
Hii nchi bado sana, usaili figisu zinakuwa too much
 
Nisiye na akili ndiye mwajiri sasa. Nawaajiri ninyi wenye akili kwa vigezo vyangu nivitakavyo mfanye kazi kuendana na job description yenu.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Ndio maana huna wafanyakazi bora sasa. We ungesema unatafuta kibenten chako hapo fresh not good candidate.
 
Acha dharau aiseee. Ukiishiwa hoja usipende ku attack mtu na vitu vya kipumbavu.
Sasa tumeuliza hoja za msingi hujajibu unakomaa na First impression ndio maana nikasema hujatumia akili yako nzuri uliojaaliwa na mungu.
Kwenye maamuzi yako huwa unaendeshwa na mihemko na sio elimu yako.

Weka hoja yako hapa. Effect ya mtu kuvaa let say Jeans kwenye usaili ni nini kwenye taaluma yake?
 
Mtu mpaka yuko Jf it means ana smartphone na anauwezo wa kununua bando. Kama anauwezo wa kununua bando atashindwa kununua surual na shati??. Surual casual ya mtumba kuanzia 5,000 unapata tukija shati mpaka 3,000 zipo mitumbani.
Auze simu anunue nguo. Na hizo ajira atazionaje sasa, na bando sio kila siku utanunua kwako wew ni rahisi, hilo shati la aftatu nidhahiri huwezi kua smart kumliko mtu mwenye kipato anaenunua nguo mohakwamoja Kwa ajili ya interview husika. Hapo Bado hujavaa viatu utasema viatu Hadi af6 vipo he vya af6 utalibganisha usmart na Cha af35 mpka 70.

Cha msingi watu wawe smart ila tunazidiana maisha jmn
 
Hata muuza vyombo akiamka asubuhi lazima afute vyombo vumbi kuviweka smart! Mbona mkitongoza first date mnakuwa smart. Vijana vaeni smart kwenye interview acheni usasa utawaponza .

Kuna wauza vyombo wanapita mitaani na masufuria wamechomekea vizuri kabisa, wewe unayetaka kazi umeenda umevaa jeans na t-shirt kisa uaangalia Brain. Kama unahela ya kununua jeans unashindwaje kununua surual casual?
 
Lakini kuijua kampuni sio kujua mavazi, bali huduma zake. Unapoambiwa unapaswa kuijua kampuni basi unatakiwa kuijua kampuni au taasisi juu ya shughuli zake. Mavazi haimo kwenye hayo ya kujua juu ya kampuni.

Website ya TRA inaeleza juu ya mavazi? Ila ukiajiriwa utaambiwa sasa sisi utaratibu wetu ni hivi na hivi.

Hii sasa ya kuangalia huyu amevaa hivi ukampa kazi ndio shida ilipo.
Hapa baba nenda na jeans
 
Kuna fani ambazo ukisoma, kazi ndio zinakuwa zinakutafuta wewe; na kuna fani zingine wewe ndio unakuwa unatafuta kazi.

Kwa hiyo, hizi fani ambazo wewe ndio unatakiwa utafute kazi inabidi uongeze 'point' kwenye mavazi; ila kwa hizi fani ambazo kazi ndio zinakuwa zinawatafuta, mavazi huwa hayana 'point' yoyote.​
Fani gani hizo mkuu zinazokutafuta?
 
Sasa hapo kwenye Smartness huoni kwamba kuna watu utawanyima haki? Wale waliotoka maisha magumu mara nyingi hawawezi kuwa smart kama wa mjini. Hapo utakuwa umetenda haki?
Mkuu, ingekuwa vyema Kama ungetofautisha kuwa smart na kutupia(Kuwaka)
 
Mkuu, ingekuwa vyema Kama ungetofautisha kuwa smart na kutupia(Kuwaka)
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Jaribu kutofautisha smart na kuwaka kaka.
 
Kwenye kutafuta ajira kuna mambo mengi sana. Wasakatonge tunahangaika huku na huko kutafuta mrija wa Asali, iwe nje ya nchi au ndani ya nchi, iwe serikali au taasisi binafsi.

Sasa basi nikiwa mmoja wa wasakatonge nilibahatika kuomba hizi kazi za TRA, na mara baada ya kuomba nikafanikiwa kupata Group moja la tulioomba kazi.

Kupitia hili group bhana, juzi usiku nikaona mjadala umeanza, mmoja wa wanagroup alitoa angalizo kuwa iwapo wasailiwa watafanana kwa marks basi kuna kigezo cha mavazi kinatumika katika kuwaondoa au kuwapata best candidate.

Kwamba watu wavaze official, kwenye usaili inakuwa rahisi kupata kazi, na mjadala ukawa mkubwa sana.

Tiliozoea kufanya saili mbalimbali hasa za serikali tukakubaliana yes mavazi ni muhimu sana, na yanachangia kwa asilimia kubwa kwenye kuchaguliwa kupata kazi.

[emoji91][emoji91][emoji91] Hapa sasa akatokea member mmoja akasema kigezo cha Mavazi hakitumiki kwenye kuchagua best candidate kwa maana Mavazi ni kipimo cha utajiri wa mtu au familia. Hivyo kigezo cha Mavazi hakiwezi kuwa sifa moja wapo ya mtu kuajiriwa na kwamba mtu anaajiriwa kwa uwezo wake kichwani.
Na ikiwa umepata ajira basi taasisi husika ndio itakuwa kanuni na taratibu za mavazi ya taasisi hiyo kama mwajiriwa.

Akaenda mbali zaidi akasema kama mavazi yanaamua nani aajiriwe kwanini wasiweke sare maalumu za usaili ili watu wote waende wakiwa sawa kimavazi?

Nilitamani kuona ule mjadala unaendelea nipate kuona namna gani sisi vijana tunaweza kuchambua mambo kisomi na kwa kuzingatia Dunia inavyoenda. Bahati mbaya leo asubuhi nimeingia nimeona group sasa wenye uwezo wa kutuma kitu ni Admins tu.

Binafsi nimeona saili nyingi ma HR wakiangalia mavazi, na wengi wamekosa kazi kupitia uvaaji.

Je wadau tujadili hapa, mavazi yana uhusiano na upatikanaji wa kazi? Na je unakubaliana na hoja ya jamaa kuwa mavazi hayapaswi kuwa kigezo cha mtu kuajiriwa bali weledi na uwezo wake wa kujua mambo?
Ndugu yangu uvaaji wako unatafsiri mambo mengi hata usiyojua.
Huoni wanawake wanaotoboa pua na vikuku wanavyochukuliwa
 
[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji3][emoji3][emoji3] Mpaka mbogo amkubali mtu basi kweli jamaa alikuwa balaa
Chief fikiria tu,mmekaa watu mnajiona kabisa hapa kichwani mpo njema.

Anakuja Mhuni mhuni tu.Kila kona unayopita anaijua.Hapa tunazungumzia utaalamu uliotukuka.
😀😀😀😀😀
Awali jinsi alivyo vaa kila mtu aliona magumashi tu.
Sisemi tuwe wachafu,ila akili zinazojua vitu huwa zipo zipo tu.😀😀😀

Kuna raia wapo njema sana upstairs hapa Bongo.Ni mambo tu ya Kiafrica huku.
 
Vijana mazingira husika hubadili uvaaji.

Kama ni swala la kazi na ukajua unakoenda pakoje si mbaya ukavaa vyema.

Ila kuvaa kuendane na kichwani kwa wakati huo.

Kuna sehemu zingine vaa upendeze kama Malaika,unakutana na wafanya Interview wameshavurugwa na cables huko wanakupa mkazi wa dakika 30 tu.

Hapo utajua tai yako imesaidia nini.

Dunia inahama kwa kasi sana kwa sasa.
 
Back
Top Bottom