Salamu kwenu. Huyu mdada amepambana anavyojua akapata barua ya uhamisho kutoka wilaya X kwenda mkoa na wilaya nyingine mwezi uliopita.Alipotoka amefungashiwa kila kitu na wilaya aliyohamia washampa barua ya kituo chakazi. Tatizo anaogopa kuhamisha mizigo yake akihofia kurudishwa alipotoka.Amerejea watu kadhaa waliorudishwa walipotoka baada ya uhamisho kuonekana wa magumashi.Yeye anadai atahamisha vitu vyake siku ESS yake itakaposoma wilaya aliyohamia. Je, kwahatua alipofikia anahaja yakuogopa kuhamisha vitu vyake au afungashe mazima?