Kuna haja ya kuwa na wasiwasi au akae kwa kutulia?

Kuna haja ya kuwa na wasiwasi au akae kwa kutulia?

Laswell

Senior Member
Joined
Feb 23, 2024
Posts
144
Reaction score
191
Salamu kwenu. Huyu mdada amepambana anavyojua akapata barua ya uhamisho kutoka wilaya X kwenda mkoa na wilaya nyingine mwezi uliopita.Alipotoka amefungashiwa kila kitu na wilaya aliyohamia washampa barua ya kituo chakazi. Tatizo anaogopa kuhamisha mizigo yake akihofia kurudishwa alipotoka.Amerejea watu kadhaa waliorudishwa walipotoka baada ya uhamisho kuonekana wa magumashi.Yeye anadai atahamisha vitu vyake siku ESS yake itakaposoma wilaya aliyohamia. Je, kwahatua alipofikia anahaja yakuogopa kuhamisha vitu vyake au afungashe mazima?
 
kama ameshapokelewa anakoenda hawezi kurudishwa.
Watu wanapokelewa, wanafanya KAZI hata mwaka na bado wanarudishwa walikotoka.
Muhimu ahamishe mshahara, Kama uhamisho ni wa magumashi mshahara utagoma kuhama......mshahara ukihama basi akae kwa kujiachia.
 
Mkuu,mshahara unaweza kuhama baada ya muda gani tangu mtumishi ahame
 
Watu wanachonga vibali vya uhamisho Kama hawana akili nzuri......tumilioni twako tu unapata kibali, Ila likibumburuka ndo balaa.
Kwa hiyo nikiwa Kamilioni kangu naweza hamia TRA au BOT nikimbie huku Harmashauri Mpimbwe?.
 
Watu wanapokelewa, wanafanya KAZI hata mwaka na bado wanarudishwa walikotoka.
Muhimu ahamishe mshahara, Kama uhamisho ni wa magumashi mshahara utagoma kuhama......mshahara ukihama basi akae kwa kujiachia.
Haya ni maajabu 😀
 
Back
Top Bottom