Kuna haja ya Wizara ya Ulinzi kuundwa upya iwe Wizara ya Ulinzi na Mambo ya Ndani

mavya

Member
Joined
Dec 24, 2021
Posts
31
Reaction score
58
Kwa muda mrefu sana tumeona Wizara ya mambo ndani ikikumbwa na changamoto nyingi sana. Hasa kwa vyombo vya ulinzi vilivyoko wizarani hapa. Police, magereza, uhamiaji, na fire.

Binafsi nilikuwa naona ili kuweka mambo sawa vyombo hivi vipelekwe Wizara ya Ulinzi ili kuvipa nguvu na kuweka Nidhamu ya hali ya juu sana.

Hii itapelekea vyombo hivi kuwa na common command, kufanya kozi kwa pamoja na kushirikiana kwa pamoja kuimarisha Ulinzi na Usalama kwa Taifa letu.
 
Hilo jipya sasa! Duniani kote wizara ya ulinzi inajitegemea. Ndio wizara pekee ambayo "haichezewichezewi" sana na wanasiasa kama zile nyingine sijui jinsia, sijui mahitaji maalumu (ambayo hayajawahi kuwekwa bayana), sijui vitu gani.
 
Kama ndivyo basi wizara ya ULINZI ijumuishe POLISI na JWTZ then Magereza,Uhamiaji na Fire inabaki mambo ya ndani
ULINZI jukumu lao la msingi wanadili na external criminals/enemies na treatment yao ni kuwaua as much as possible wakati Polisi focus yao ni internal criminals ambao treatment yao ni kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

So, kuna utofauti mkubwa sioni wakichangamana.
 
Kwani shida ni waziri? Vyombo hivyo vina autonomy kubwa sana, changamoto zao ni za kihistoria.

Mf. Jeshi la polisi ni lile tulirithi kutoka kwa mkoloni, liliundwa kwa ajili ya kuilinda serikali ya mkoloni na kuwatia adabu watanganyika.

Baada ya kile kilichoitwa 'uhuru', wakolini wetu wapya ambao walikuwa ni waafrika wenzetu chini ya mwamvuli wa uzalendo uchwara uliotukuka wakaamua kuendelea nalo ili kututia adabu tusilete fyokofyoko wala kuwawajibisha wanapovurunda mambo.
 
Wizara ya Ulinzi sio kwamba ipo above law's za nchi ni basi sisi Watanzania tumemeza mno moshi wa ile kitu inayozungukaga nchi nzima, matumizi ya wizara hii ni lazima sisi walipa kodi tujue ila woga wetu ambao tumeurithi generation to generation ndio tatizo, wizara ya Home Affairs ivunjwe na zitengenezwe wizara mbili, wizara ya police (usalama wa raia) na wizara ya mambo ya ndani (uraia &immigrations); idara ya zimamoto rudisha kwa serikali za mitaa na idara ya magereza weka chini ya Justice ministry.
 
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote.

Hapa Nchini raia wa kawaida anaweza kuandika jinsi anavyotaka muundo wa wizara uwe.Hata kama hana utaalamu wowote .Unique just unique.
 
Wizara ya Ulinzi sio kwamba ipo above law's za nchi ni basi sisi watanzania tumemeza mno moshi wa ile kitu inayozungukaga nchi nzima,matumizi ya wizara hii ni lazima sisi walipa kodi tujue ila woga wetu ambao tumeurithi generation to generation ndio tatizo,wizara ya Home Affairs ivunjwe na zitengenezwe wizara mbili,wizara ya police(usalama wa raia) na wizara ya mambo ya ndani(uraia &immigrations);idara ya zimamoto rudisha kwa serikali za mitaa na idara ya magereza weka chini ya Justice ministry.
Umeongea facts mkuu
 
ULINZI jukumu lao la msingi wanadili na external criminals/enemies na treatment yao ni kuwaua as much as possible wakati Polisi focus yao ni internal criminals ambao treatment yao ni kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

So, kuna utofauti mkubwa sioni wakichangamana.
Mbona polisi wanatuua sana tu
 
ULINZI jukumu lao la msingi wanadili na external criminals/enemies na treatment yao ni kuwaua as much as possible wakati Polisi focus yao ni internal criminals ambao treatment yao ni kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

So, kuna utofauti mkubwa sioni wakichangamana.
Ironically wanafanya kinyume chake kabisa hao polisi. Wao ndio wamekuwa criminals kwa kudhuru raia.
 
Wizara ya Ulinzi sio kwamba ipo above law's za nchi ni basi sisi watanzania tumemeza mno moshi wa ile kitu inayozungukaga nchi nzima,matumizi ya wizara hii ni lazima sisi walipa kodi tujue ila woga wetu ambao tumeurithi generation to generation ndio tatizo,wizara ya Home Affairs ivunjwe na zitengenezwe wizara mbili,wizara ya police(usalama wa raia) na wizara ya mambo ya ndani(uraia &immigrations);idara ya zimamoto rudisha kwa serikali za mitaa na idara ya magereza weka chini ya Justice ministry.
Idea nzuri sana, ningekuwa ndio mshauri wa rais ningemshauri ivyo
 
Wizara ya Ulinzi sio kwamba ipo above law's za nchi ni basi sisi watanzania tumemeza mno moshi wa ile kitu inayozungukaga nchi nzima,matumizi ya wizara hii ni lazima sisi walipa kodi tujue ila woga wetu ambao tumeurithi generation to generation ndio tatizo,wizara ya Home Affairs ivunjwe na zitengenezwe wizara mbili,wizara ya police(usalama wa raia) na wizara ya mambo ya ndani(uraia &immigrations);idara ya zimamoto rudisha kwa serikali za mitaa na idara ya magereza weka chini ya Justice ministry.
Couldn't be more precise than this. Tatizo nchi hii waliokuwa na akili ndio hufanywa machizi.
 
Mimi nafikiri nafasi ya IGP ndiyo inapaswa kushikwa na mwanajeshi kutoka JWTZ. Akiwekwa Brigedia Jenerali ambaye anahusika ndani ya jeshi katika masuala ya utawala na logostiki atafaa sana kuleta nidhamu na ufanisi katika Jeshi la Polisi.
 
ULINZI jukumu lao la msingi wanadili na external criminals/enemies na treatment yao ni kuwaua as much as possible wakati Polisi focus yao ni internal criminals ambao treatment yao ni kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

So, kuna utofauti mkubwa sioni wakichangamana.
Hakuna sheria ya kimataifa inaruhusu kuua kama unavyojipbanua!! International criminal's sio kazi ya Jeshi
 
... mafunzo ya JWTZ upande wa shabaha ni kifua na sio pengine popote!
 
Wizara ya kazi maalumu...

Mkuu acha tu ulinzi ubaki kujitegemea kama ilivo sasa
 
Kwa muda mrefu sana tumeona Wizara ya mambo ndani ikikumbwa na changamoto nyingi sana. Hasa kwa vyombo vya ulinzi vilivyoko wizarani hapa. Police, magereza, uhamiaji, na fire.

Binafsi nilikuwa naona ili kuweka mambo sawa vyombo hivi vipelekwe Wizara ya Ulinzi ili kuvipa nguvu na kuweka Nidhamu ya hali ya juu sana.

Hii itapelekea vyombo hivi kuwa na common command, kufanya kozi kwa pamoja na kushirikiana kwa pamoja kuimarisha Ulinzi na Usalama kwa Taifa letu.
Itawezekana wanaume wakianza kuwa wajawazito
 
Itakuwa kubwa Sana si unajua wote wanadili na ulinzi lakini awafanani majukumu
 
Back
Top Bottom