Kuna haja ya Wizara ya Ulinzi kuundwa upya iwe Wizara ya Ulinzi na Mambo ya Ndani

Kinachoicost Wizara ya Mambo ya ndani ni ubinafsi wa vyombo vyenyewe vilivyoko ndani yake kila chombo kinaataka kijione bora kuliko kingine ndo hata maslahi yao wenyewe yako kibnafisi mjo iila chombo kinapambama kivyake.
 
Soma majukumu ya wizara hizo utaelewa tofauti zao. Pamoja na usiasa mwingi uliopo mpaka wakati mwingine walinzi kuvalishwa magwanda ya wana usalama, wizara hizo huwezi zichanganya ukapata matokeo chanya.
 
Mpaka leo sheria haijabadirishwa na jukumu kubwa la polisi ni kulinda viongozi na mali zao. Ukiona polisi mtaani jua anamtafuta alie jaribu Kuvunja hiyo kanuni, au kuzuia wananchi wasipange Kuvunja kanuni hiyo.
 
Naunga mkono hoja
 
Hiyo itakuwa na kwanza duniani!

Sijawahi kusikia Wizara ya Ulinzi ikichanganywa na mambo ya ndani. Ulinde mipaka yote na ardhi na bahari, halafu uanze kuangaika na panya road wa Chanika!
 
Hiyo itakuwa na kwanza duniani!

Sijawahi kusikia Wizara ya Ulinzi ikichanganywa na mambo ya ndani. Ulinde mipaka yote na ardhi na bahari, halafu uanze kuangaika na panya road wa Chanika!
Hivi hawa ambao wanakaa kambi za mijini na mikoa ya kati huwa wanalinda mipaka gani? Maana huwa naona wanaenda kambini na saa tisa wanarudi majumbani kama watumishi wengine wa umma. Rwanda wana system nzuri ya ku utilize human resources wao, wanajeshi ndo wanaolinda mabenki na taasisi nyingi muhimu, barabarani pia wanazunguka kulinda doria.
 
Wananchi wajue majukumu ya wizara hizo mbili.
 
Wananchi wajue majukumu ya wizara hizo mbili
 
Rwanda wana matatizo ya usalama ndio maana wanajeshi wanalinda mpaka ndani ya nchi. Kwenye mifumo mizuri, wanajeshi hawapaswi kufanya kazi za polisi.

Hao unaosema wanakaa kambi za mijini wana kazi nyingi tu. Hizi kambi za hapa Dar nyingi zina kazi zake mahsusi lakini pia huwa wanafanya rotation na wenzao.
 
Ndani ya wizara ya mambo ya ndani ni kuitoa polisi ianzishwe wizara ya usalama wa raia hapo mambo yataenda sawa.
 
Uko sahihi.
 
Mwanajeshi hawezi kuwa polisi, polisi inahusisha usomi wa sheria na kufanya kazi na mahakama sio manguvu tu.
Mimi nafikiri nafasi ya IGP ndiyo inapaswa kushikwa na mwanajeshi kutoka JWTZ. Akiwekwa Brigedia Jenerali ambaye anahusika ndani ya jeshi katika masuala ya utawala na logostiki atafaa sana kuleta nidhamu na ufanisi katika Jeshi la Polisi.
 
Huwezi changanya polisi na tpdf, polisi ni mijizi Sana hakuna haki kwanza Bora migambo kuliko Taasisi hii ya hivyo ukiwataarifu tukio kwao dili
 
Hilo jipya sasa! Duniani kote wizara ya ulinzi inajitegemea. Ndio wizara pekee ambayo "haichezewichezewi" sana na wanasiasa kama zile nyingine sijui jinsia, sijui mahitaji maalumu (ambayo hayajawahi kuwekwa bayana), sijui vitu gani.
unataka kuchanganya polisi na jeshi la wananchi? NIMEKATAA
 
Heheh, unajua uzito wa hizi wizara. Mzee? Labda Kama utaweka Waziri na manaibu Waziri wanne. Ulinzi ni pana sana na mambo ya ndani nayo no pana mno. Yani Waziri mmoja adeal na majeshi yote kwa maana ya JWTZ, JKT, POLISI, MAGEREZA, FIRE nk na vikosi vyake ndani aisee unaelewa unachoongea kweli??????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…