THE BROKER
JF-Expert Member
- Sep 10, 2014
- 743
- 915
Nimepigiwa simu na Baba Mzazi kutoka huko Moshi Kilimanjaro na kunieleza ya kwamba kuna hatari kubwa ya kuwepo kwa anwani hewa zitakazotokana na zoezi hili la urasimishaji wa anwani za makazi kama ifuatavyo:-
Kwamba, wahusika wanasajili makazi kwa maana ya "nyumba" ambapo Msingi unatafsiriwa kama nyumba hata kama ulishatelekezwa kwa miaka mingi iliyopita, boma/nyumba ambayo haiishi mtu yeyote pia inatambuliwa kama makazi hata kama wakazi wake wote wamefariki dunia au wamehama. Hata maghofu wanatambua kama makazi rasmi na kusajili.
Kutokana na makosa hayo mwisho wa siku tutakuwa na idadi kubwa ya anwani hewa kwenye makazi hewa ambayo hayapo na hayatakuja kuwepo.
Hivyo, naishauri serikali na wanaohusika kupitia tena upya kwenye eneo la kubainisha sifa za makazi yanayopaswa kusajiliwa ili tuepukane na janga la kuwa na anwani hewa kwenye makazi hewa.