Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wa humu JamiiForums.
Ndugu zangu Watanzania;
Kuna stage ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike. Mnauza mali zote kulipia matibabu, ndugu anakufa kisha familia inabaki na umasikini wa kutupwa. Familia masikini/fukara kuuza nyumba yao ya pekee ni pigo kubwa sana kwa watoto wadogo.
Ninaandika haya nikijua fika ya kwamba hakuna idadi ya mali au pesa kinachoweza kulingana na uhai wa mwanadamu. Unakumbuka ajali ya MV Bukoba? Unakumbuka ajali ya MV Spice kule Zanzibar?
Ni Watanzania wangapi walikufa katika ajali zile? Hivi wakati wa majanga yale uliwahi kusikia hata siku moja Watanzania wanalalamika kuhusiana na thamani ya zile meli?
Unajua gharama ya vyombo vile ni mamilioni ya pesa ngapi za Kitanzania? Licha ya kuwa ni pesa nyingi sana zilitumika katika kununua/kuunda vyombo vile Watanzania bado wakawa wanalilia roho za binadamu wenzao kwa maana kwamba hakuna cha kufananisha na uhai wa mwanadamu.
Hiyo ndio asili ya huruma ambayo Mungu ametupa sisi wanandamu. Familia zetu hizi masikini, mali tunazipata kwa tabu sana, ujenzi wa kuungaunga nyumba moja unajenga kwa kudunduliza miaka zaidi ya 9.
Baada ya ujenzi kukamilika, mnaishi miaka yenu 3, alafu ghafla mnasikia baba yenu mzazi anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ini au figo zote zimefeli anapaswa kupelekwa India kwa matibabu zaidi.
Ndugu wanajitahidi kuchangisha kwa jamaa na rafiki zao hapa na pale kiasi hakifikii pesa sahihi inajohitajika kuweza kukidhi gharama za matibabu hivyo wanaamua kuuza mali zao za thamani walizonazo kumpeleka baba yao nje ya nchi (India) kwa matibabu zaidi.
Matokeo yake baba anakufa, mzee wa miaka 69, na mali zote mmeuza. Unaikuta familia iliyotoka kupanga chumba na sembule kisha wakajikwamua kujenga wanarudi tena katika nyumba za kupanga na maisha ya kuomba omba.
Nimemua kuleta mada hii hapa baada ya kukutana na kijana mmoja jina lake ni ****** ambaye nilikuwa ninakaa nao Keko Juu mwaka 2011 ambaye baba yao alifariki mwaka 2014 kwa ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo.
Inasemekana kwamba mzee yule wa miaka 66 hakuwa na matumaini ya kupona, kulingana na taarifa ambazo mmoja wa ndugu yao wa karibu (baba mdogo) alipewa na daktari katika hospitali moja maarufu tu hapa Dar.
Kwa kuwa familia bado ilikuwa inampenda na kumthamini mzee wao wakaona ni bora wauze hata nyumba waliokuwa wanajenga huko Toa Ngoma njia ya Kongowe ili wampeleke baba yao huko India. Matokeo yake ndio kama haya. Wamepoteza vyote, baba pamoja na nyumba.
Mama ndio hivyo tena biashara za kuungaunga za akina mama lishe, dada zake wawili walizaa tu hapo nyumbani yaaani nilipoonana na huyu kijana (ni agemate na mimi) machozi yalitaka kunitoka.
Basi tu kwa kuwa na mimi mwenyewe ni Taxi Driver mlala hoi sina cha kumpa zaidi ya kusimuliana story za zamani tulipokuwa tunacheza mpira (cha ndimu) wote na kwenda kuogelea baharini kule Kurasini tulikuwa tunapaita ZAMCARGO au SAVA.
Ndugu zangu, kuna stage ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike tusizidishe umasikini katika familia.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.