Kuna hatua ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike. Mnauza mali zote kulipia matibabu, ndugu anakufa kisha familia inabaki na umasikini wa kutupwa

Kuna hatua ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike. Mnauza mali zote kulipia matibabu, ndugu anakufa kisha familia inabaki na umasikini wa kutupwa

Kuna vitu vingine kwa sisi waafrika hufanyika kutokana na ujinga wetu. Sasa doctor kakwambia utakufa, mnalazimisha nini? Istoshe asilimia kubwa ndiyo uhamia kwa waganga wa kienyeji na wazee wa upako
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

Kuna stage ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike. Mnauza mali zote kulipia matibabu, ndugu anakufa kisha familia inabaki na umasikini wa kutupwa. Familia masikini/fukara kuuza nyumba yao ya pekee ni pigo kubwa sana.

Ninaandika haya nikijua fika ya kwamba hakuna idadi ya mali au pesa kinachoweza kulingana na uhai wa mwanadamu. Unakumbuka ajali ya MV Bukoba wewe? Unakumbuka ajali ya MV Spice kule Zanzibar?

Ni watanzania wangapi walikufa katika ajali zile? Hivi wakati wa majanga yale uliwahi kusikia hata siku moja watanzania wanalalamika kuhusiana na thamani ya zile meli?

Unajua gharama ya vyombo vile ni mamilioni ya pesa ngapi za kitanzania? Licha ya kuwa ni pesa nyingi sana zilitumika katika kununua/kuunda vyombo vile watanzania bado wakawa wanalilia roho za binadamu wenzao kwa maana kwamba hakuna cha kufananisha na uhai wa mwanadamu.

Hiyo ndio asili ya huruma ambayo Mungu ametupa sisi wanandamu. Familia zetu hizi masikini, mali tunazipata kwa tabu sana, ujenzi wa kuungaunga nyumba moja unajenga kwa kudunduliza miaka zaidi ya 9.

Baada ya ujenzi kukamilika, mnaishi miaka yenu 3, alafu ghafla mnasikia baba yenu mzazi anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ini au vigo zote zimefeli anapaswa kupelekwa India kwa matibabu zaidi.

Ndugu wanajitahidi kuchangisha kwa jamaa na rafiki zao hapa na pale kiasi hakifikii pesa sahihi inajohitajika kuweza kukidhi gharama za matibabu hivyo wanaamua kuuza mali zao za thamani walizonazo kumpeleka baba yao nje ya nchi (India) kwa matibabu zaidi.

Matokeo yake baba anakufa, mzee wa miaka 69, na mali zote mmeuza. Unaikuta familia iliyotoka kupanga chumba na sembule kisha wakajikwamua kujenga wanarudi tena katika nyumba za kupanga na maisha ya kuomba omba.

Nimemua kuleta mada hii hapa baada ya kukutana na kijana mmoja jina lake ni ****** ambaye nilikuwa ninakaa nao Keko Juu mwaka 2011 ambaye baba yao alifariki mwaka 2014 kwa ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo.

Inasemekana kwamba mzee yule wa miaka 66 hakuwa na matumaini ya kupona, kulingana na taarifa ambazo mmoja wa ndugu yao wa karibu (baba mdogo) alipewa na daktari katika hospitali moja maarufu tu hapa Dar.

Kwa kuwa familia bado ilikuwa inampenda na kumthamini mzee wao wakaona ni bora wauze hata nyumba waliokuwa wanajenga huko Toa Ngoma njia ya Kongowe ili wampeleke baba yao huko India. Matokeo yake ndio kama haya. Wamepoteza nyote, baba pamoja na nyumba.

Mama ndio hivyo tena biashara za kuungaunga za akina mama lishe, dada zake wawili walizaa tu hapo nyumbani yaaani nilipoonana na huyu kijana (ni agemate na mimi) machozi yalitaka kunitoka.

Basi tu kwa kuwa na mimi mwenyewe ni Taxi Driver mlala hoi sina cha kumpa zaidi ya kusimuliana story za zamani tulipokuwa tunacheza mpira (cha ndimu) wote na kwenda kuogelea baharini kule Kurasini tulikuwa tunapaita ZAMCARGO au SAVA.

Ndugu zangu, kuna stage ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike tusizidishe umasikini katika familia.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Hii mada yako inanigusa mimi kwa namna fulani. Kulikuwa na ndugu yangu anaumwa, kwa hiyo nikajikuta nina jukumu kubwa la kulipia matibabu yake kuliko ndugu wengine wote.

Baadaye daktari akasema huyu mgonjwa ana saratani ambayo imekwisha chelewa sana haitibiti hospitali tena; ila akasema tujaribu madawa ya kienyeji.

Mimi nilimwelewa daktari yule kuwa hakutaka kutukatisha tamaa, ila massage yake ilikuwa ni game over. Sasa akaja mtu mmoja anasema kuna mganga wa kienyeji anatibu matatizo hayo haraka sana na kiasi chake cha kuanzia ni kilikuwa ni laki nne tu, halafu mgonjwa akishapona tunamaliziana laki nne nyingine.

Hizo hazikuwa hela nyingi za kuanzia matibabu lakini mimi sikuwa tayari kuzitoa tena kwa vile kulingana na prognosis ya daktari kule hospitali, tatizo hilo lilikuwa ni terminal.

Hivyo nikashauri tu kuwa ukoo wote tuitishe mchango badala ya kunitegemea mimi tu. Kabla ya mchango kukamilika, ndugu yetu yule akatangulia mbele ya haki. Kuna magonjwa ambayo hayatibiki, na ni lazima tukubaliane na hali hiyo!
 
mkuu upo sahihi kwa 50% na upo wrong kwa 50%...incase mhusika anayeumwa zaid mwenye ages above 60 ndo anayemiliki mali ni za kwake ni ngumu kujali chochote zaidi ya uhai wake atauza tu,,ila mkiwa mnamuuguza mtu kwa kila mmoja kutoa donation kumchagia mgonjwa ili apone hayo maelezo yako juu yatakuwa sahihi.
 
Unafikiri ni kwanini mateka hua wanatishiwa kupokonywa uhai na siyo nyumba?
Inaonekana haukusoma andiko langu kuu. Nilichoandika mimi pale ni kwamba;
=====
Ninaandika haya nikijua fika ya kwamba hakuna idadi ya mali au pesa kinachoweza kulingana na uhai wa mwanadamu. Unakumbuka ajali ya MV Bukoba wewe? Unakumbuka ajali ya MV Spice kule Zanzibar?

Ni watanzania wangapi walikufa katika ajali zile? Hivi wakati wa majanga yale uliwahi kusikia hata siku moja watanzania wanalalamika kuhusiana na thamani ya zile meli?

Unajua gharama ya vyombo vile ni mamilioni ya pesa ngapi za kitanzania? Licha ya kuwa ni pesa nyingi sana zilitumika katika kununua/kuunda vyombo vile watanzania bado wakawa wanalilia roho za binadamu wenzao kwa maana kwamba hakuna cha kufananisha na uhai wa mwanadamu.

Hiyo ndio asili ya huruma ambayo Mungu ametupa sisi wanandamu.
 
mkuu upo sahihi kwa 50% na upo wrong kwa 50%...incase mhusika anayeumwa zaid mwenye ages above 60 ndo anayemiliki mali ni za kwake ni ngumu kujali chochote zaidi ya uhai wake atauza tu
Sawa mali ni zake na anauwezo wa kuuza. Sasa hawa watoto wake waliopo darasa la nne na mwingine yupo form one wataenda kuishi wapi wakati nyumba ndio hiyo hiyo moja mkuu?...
 
Jii mada yako inanigusa mimi kwa namna fulani. Kulikuwa na ndugu yangu anaumwa, kwa hiyo nikajikuta nina jukumu kubwa la kulipia matibabu yake kuliko ndogu wengine. baadaye dakatri akasema huyu mgomnjwa ana saratani ambayo imekwisha chelewa sana haitibiti hospitali tena; ila akasema tujaribu madawa ya kienyeji. Mimi nilimwelewa dakatarui yule kuwa hakutaka kutukatoisha tamaa, ila massage yake ilikuwa ni game over. Sasa akaja mtu mmoja anasema kuna mganga wa kienyeji anatibu matatizo hayo haraka sana na kiasi chake cha kuanzia ni kilikuwa ni laki nne tu, halafu mgonjwa akishapona tunamaliziana laki nne nyingine.
Inahuzunisha sana mkuu. Pole sana...
 
Yah lazim busara itumike. Kuna maginjwa mengin kwa kwel ...hayatibiki mf mtu ana kansa au hiv hata ufanyaj hawez pona Ila pia. Mzaz akiwa critical lazim mtu ufanye lolote sii kumwach tu coz atakufa. Mf unaweza ukauza nyumb ukanunua Figo mtu akaendelea kusivive na kujijeng upya ..
Wapo wanaopona inategemea na stage yake
 
Kwenye kuumwa na umri unabeba Kinga za mwili na jinsi mtu alivyothamini afya yake hasa ulaji, Sasa Kama mtu ana umri mdogo hata magonjwa makubwa akipambaniwa anapona na umri mkubwa au magonjwa ya uzee yenyewe yanahitaji nguvu kubwa ya kidaktari ambayo ni pesa Sasa Kama mtu miaka 100 anaumwa na anapesa au mali zake na michango ziuzwe tu apate huduma na waliobaki watafute vya kwao huku wakiwa wanakumbuka kuishauri serikali bima za afya kwa wazee maana afya zao zinakuwa hazina Kinga.
 
Ukifika hatua kama hiyo tambua huo siyo ugonjwa Kuna kitu. Kuna Muovu kapanda magugu ndani ya mwili WA binadamu na lengo kubwa kutia umasikini kwenye family hiyo.
 
Kuna familia tumeona, mshua anaondoka na hawajauza kila kitu lakini msoto wanaopitia ni wa uchumi wa kati. Unawaza na wangeuza mpaka kibanda ingekuwaje? Uzuri kuna wagonjwa huwa wanafahamu na kuwakumbuka wanaobaki na kuziria matibabu. Kuna situation hazilazimishwi wakuu.
 
Na ndio maana kuna wagonjwa huwa wanaongozwa na busara kulingana na hali ya ugonjwa alionao na mategemeo hafifu kabisa ya kupona, anamwita mpendwa wake anamwambia ukweli tu kuwa uwezekano wa kupona haupo. Hivyo kile walichotafuta kwa shida kwa muda mrefu kitumike kutunza familia na kusomesha watoto. Hiyo ni kwa wale wagonjwa ambao wanaweza kuzungumza bado.
Labda ili tuweke mambo sawa tujiulize, je wewe utaruhusu mali zenu ziuzwe ili ukatibiwe ugonjwa ambao hauwezi kupona na unajua kabisa?
 
Back
Top Bottom