Kuna hatua ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike. Mnauza mali zote kulipia matibabu, ndugu anakufa kisha familia inabaki na umasikini wa kutupwa

Sure
 
Mada nzuri but kibinadam ni ngumu sana kumsusa mpendwa ndio maana familia hujitoa kwa kila hali, hitimisho lako lilipaswa kuihamasisha jamii iwe na utamaduni wa kuchangia matibabu kama wafanyavyo kwenye masherehe na misiba na sio busara za kususa.
 
Mfano wako sio LIFE & DEATH

Hujafikiwa kukaribia kuwapoteza watu wa muhimu Mama/Baba/Mtoto wako

Ndo Utajua kuwa mbele ya hizo unaita "hisia" nyumba na Mali zote sio kitu. And u would give anything to have them, hata kuwaongezea muda kidogo tu. Hata Daktari akwambie ni stage 11

Mali zinatafutwa, hasara roho
 
Mtu chake mali kazitafuta yeye zitumike tu kumtibia alizitafuta zimfae akifa waliobaki watatafuta zao kama yeye alivyotafuta

Mleta mada una roho ya kivivu nyie ndio hutolea mimacho wagonjwa wenye mali wafe mgombanie kurithi chake

Wewe waonyesha wazi una roho ya kiuaji waweza ua hata mzazi wako ukiona anaumwa sana na gharama za kutibu kubwa ili mchukue chake
Una pepo mchafu
 
Ndiyo maana wachina viumbe dhaifu wanachoma tu sindano ya sumu na kuvipumzisha kwa amani.
 
Ingekuwa jamii yetu ni yenye kujitegemea, kuwa Mzee kachuma na kuwekeza, na Vijana wake nao wameanza kuchuma na kujitegemea na kutafuta mali zao, ningesema Mzee amestahili alichochuma. Kwamba kwa kujenga nyumba, hiyo ilikuwa ndio bima yake, ama akiba yake ya uzeeni. Sijui kama angepona kungekuwa na pesa za ziada kutoka kwenye mauzo ya nyumba, ambazo zingemsukuma mpaka kifo chake, ila hayo hayakutokea.

Jamii zetu zinabweteka, alichochuma baba, hata mjukuu atataka ajibane hapo hapo, badala ya kila mtu kutafuta chake.
 
VIP tangazo letu LA vitabu vya kijerumani silioni siku hizi
 
Kifo kipo kila binadamu ataonja umauti kwa wakati wake, unaweza ukaondoka wewe mzima ukamuacha mgonjwa na ugonjwa.

Tunachowapambania wapendwa wetu ni maumivu makali wanayopitia, hata kama atakufa unasema tumpunguzie maumivu anayopitia kwa Hali na Mali.

Subiri uuguze utaelewa kwa Nini wañauza Mali.
 

Unajua maana ya cancer stage four?
 
Uhai ni bora kuliko mali.
 
Hahahaha ndo maana nikakwambia hata "Stage 11" kama unajua kuchambua ungejua nimekutajia sarcastically, na ungeng'amua kama najua/sijui ngazi zake mpaka Terminal stage

Anyway tukubaliane kutokubaliana

Nini tofauti ya terminal stage and stage four?
 
Hakuna palliative care, ni sawa na tunavyotunza wazee wetu ni jukumu la familia zaidi...ni kama utamaduni hatuwezi kufanya vitu nje ya tulivyovizoea....kikwetu kisaikolojia tunaenda hospitali tutibiwe na kama ikitokea tukipewa majibu tofauti tutafuta na kutafuta hospitali nyingine ambazo tuna perceive kuwa better, kumbe ugonjwa hautibiki...
 
Kwa bahati nzuri tangia ulivyonitukana katik ile mada ya vodacom ya kutuma na ada ya kutolea, nilishakuweka katika IGNORE LIST yangu. Sijui kwanini nime-click kusoma comment yako.
 
Mkuu acha tu, mimi nimepambana mpaka mama yangu mzazi kafariki, kungekuwa na rufaaa hata ya kwenda wapi ningeuza kila kitu nibaki na nguo nilizovaa Ili mradi apone.

Sio rahisi kama unavyodhani, ni ngumu sanaa kusema tusiuze Mali kisa atakufa. Jibu ni hapana lazima tupambane mpaka mwisho tubaki kulia kuwa Mungu kampenda zaidi na sio tumeshindwa kumuokoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…