Kuna hatua ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike. Mnauza mali zote kulipia matibabu, ndugu anakufa kisha familia inabaki na umasikini wa kutupwa

Kuna vitu vingine kwa sisi waafrika hufanyika kutokana na ujinga wetu. Sasa doctor kakwambia utakufa, mnalazimisha nini? Istoshe asilimia kubwa ndiyo uhamia kwa waganga wa kienyeji na wazee wa upako
 
Hope upo wewe tu, huna watoto, mke/ mume, baba wala mama.

Au kama wote unao basi hizo rabsha zisikukute.
Familia masikini/fukara kuuza nyumba yao ya pekee ni pigo kubwa sana.
 
Hii mada yako inanigusa mimi kwa namna fulani. Kulikuwa na ndugu yangu anaumwa, kwa hiyo nikajikuta nina jukumu kubwa la kulipia matibabu yake kuliko ndugu wengine wote.

Baadaye daktari akasema huyu mgonjwa ana saratani ambayo imekwisha chelewa sana haitibiti hospitali tena; ila akasema tujaribu madawa ya kienyeji.

Mimi nilimwelewa daktari yule kuwa hakutaka kutukatisha tamaa, ila massage yake ilikuwa ni game over. Sasa akaja mtu mmoja anasema kuna mganga wa kienyeji anatibu matatizo hayo haraka sana na kiasi chake cha kuanzia ni kilikuwa ni laki nne tu, halafu mgonjwa akishapona tunamaliziana laki nne nyingine.

Hizo hazikuwa hela nyingi za kuanzia matibabu lakini mimi sikuwa tayari kuzitoa tena kwa vile kulingana na prognosis ya daktari kule hospitali, tatizo hilo lilikuwa ni terminal.

Hivyo nikashauri tu kuwa ukoo wote tuitishe mchango badala ya kunitegemea mimi tu. Kabla ya mchango kukamilika, ndugu yetu yule akatangulia mbele ya haki. Kuna magonjwa ambayo hayatibiki, na ni lazima tukubaliane na hali hiyo!
 
mkuu upo sahihi kwa 50% na upo wrong kwa 50%...incase mhusika anayeumwa zaid mwenye ages above 60 ndo anayemiliki mali ni za kwake ni ngumu kujali chochote zaidi ya uhai wake atauza tu,,ila mkiwa mnamuuguza mtu kwa kila mmoja kutoa donation kumchagia mgonjwa ili apone hayo maelezo yako juu yatakuwa sahihi.
 
Unafikiri ni kwanini mateka hua wanatishiwa kupokonywa uhai na siyo nyumba?
Inaonekana haukusoma andiko langu kuu. Nilichoandika mimi pale ni kwamba;
=====
Ninaandika haya nikijua fika ya kwamba hakuna idadi ya mali au pesa kinachoweza kulingana na uhai wa mwanadamu. Unakumbuka ajali ya MV Bukoba wewe? Unakumbuka ajali ya MV Spice kule Zanzibar?

Ni watanzania wangapi walikufa katika ajali zile? Hivi wakati wa majanga yale uliwahi kusikia hata siku moja watanzania wanalalamika kuhusiana na thamani ya zile meli?

Unajua gharama ya vyombo vile ni mamilioni ya pesa ngapi za kitanzania? Licha ya kuwa ni pesa nyingi sana zilitumika katika kununua/kuunda vyombo vile watanzania bado wakawa wanalilia roho za binadamu wenzao kwa maana kwamba hakuna cha kufananisha na uhai wa mwanadamu.

Hiyo ndio asili ya huruma ambayo Mungu ametupa sisi wanandamu.
 
mkuu upo sahihi kwa 50% na upo wrong kwa 50%...incase mhusika anayeumwa zaid mwenye ages above 60 ndo anayemiliki mali ni za kwake ni ngumu kujali chochote zaidi ya uhai wake atauza tu
Sawa mali ni zake na anauwezo wa kuuza. Sasa hawa watoto wake waliopo darasa la nne na mwingine yupo form one wataenda kuishi wapi wakati nyumba ndio hiyo hiyo moja mkuu?...
 
Inahuzunisha sana mkuu. Pole sana...
 
Wapo wanaopona inategemea na stage yake
 
Kwenye kuumwa na umri unabeba Kinga za mwili na jinsi mtu alivyothamini afya yake hasa ulaji, Sasa Kama mtu ana umri mdogo hata magonjwa makubwa akipambaniwa anapona na umri mkubwa au magonjwa ya uzee yenyewe yanahitaji nguvu kubwa ya kidaktari ambayo ni pesa Sasa Kama mtu miaka 100 anaumwa na anapesa au mali zake na michango ziuzwe tu apate huduma na waliobaki watafute vya kwao huku wakiwa wanakumbuka kuishauri serikali bima za afya kwa wazee maana afya zao zinakuwa hazina Kinga.
 
Ukifika hatua kama hiyo tambua huo siyo ugonjwa Kuna kitu. Kuna Muovu kapanda magugu ndani ya mwili WA binadamu na lengo kubwa kutia umasikini kwenye family hiyo.
 
Kuna familia tumeona, mshua anaondoka na hawajauza kila kitu lakini msoto wanaopitia ni wa uchumi wa kati. Unawaza na wangeuza mpaka kibanda ingekuwaje? Uzuri kuna wagonjwa huwa wanafahamu na kuwakumbuka wanaobaki na kuziria matibabu. Kuna situation hazilazimishwi wakuu.
 
Na ndio maana kuna wagonjwa huwa wanaongozwa na busara kulingana na hali ya ugonjwa alionao na mategemeo hafifu kabisa ya kupona, anamwita mpendwa wake anamwambia ukweli tu kuwa uwezekano wa kupona haupo. Hivyo kile walichotafuta kwa shida kwa muda mrefu kitumike kutunza familia na kusomesha watoto. Hiyo ni kwa wale wagonjwa ambao wanaweza kuzungumza bado.
Labda ili tuweke mambo sawa tujiulize, je wewe utaruhusu mali zenu ziuzwe ili ukatibiwe ugonjwa ambao hauwezi kupona na unajua kabisa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…