Kuna hatua ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike. Mnauza mali zote kulipia matibabu, ndugu anakufa kisha familia inabaki na umasikini wa kutupwa

Kuna watu huwa wanaondoka vizuri Duniani hata kama wanakufa kwa mateso makali ya ugonjwa hasa pale wanapojua wanaowaacha wamewaacha wakiwa na uhakika wa maisha na sio watumwa watarajiwa.
 
Mkuu..hujawahi kufiwa wewe.siku yakikukuta utatamani kuufuta huu uzi wako.

Sisi pia mwaka 2014, maza aliumwa sana, tukatumia gharama kubwa sana kumtibu, tulianza kwa kumpeleka hospital moja maarufu jijini Nairobi, tukakaa nae almost miezi minne kule, wakatushauri tumhamishie India, hapo mzee nae pesa zikawa kama zimemuishia hivi ila akawa yuko tayari kuuza nyumba yake moja ili pesa zipatikane maza apelekwe india na familia nzima tuliridhia hilo, wakati tuko kwenye mchakato wa kuuza nyumba bahati mbaya maza kafariki dunia.
 
Mzee alikuwa na Nyumba ngapi?
 
Hongera kwa wazo zuri, uzi uliojaa busara. Naomba uchunguze na hili - " mercy killing "
 
Ametoa mfano wa mtu mwenye umri wa miaka 69 hapo Busara lazima itumike maana gata akipona atakaa tena miaka mingapi?
 
Unaona ulichoandika? Mzee alikuwa yupo tayari kuuza nyumba yake moja, ina maana nyie mna nyumba nyingi. Vp kama mngekuwa masikini na nyumba hiyo hiyo moja?
 
Ukifika hatua kama hiyo tambua huo siyo ugonjwa Kuna kitu. Kuna Muovu kapanda magugu ndani ya mwili WA binadamu na lengo kubwa kutia umasikini kwenye family hiyo.
Nilikuwa natafuta comment km hii aisee.

Magonjwa mengi yanasabibiswa na nguvu zisizoonekana kwa lengo la kuwarudisha watu nyuma, hili wengi hawalijui.
 
Watu wanauza hadi utu sembuse Mali Ili wapendwa wako wapone, daktari sio Mungu kusema atopona mgonjwa.
Usiombe yakufike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…